Barabara ya Dar - Chalinze kujengwa na muwekezaji

jerrytz

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
5,975
4,264
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesitisha mpango wa kugharamia ujenzi wa barabara ya Dar - Chalinze (itakayokuwa na njia sita yenye urefu kilometa 142) na badala yake imeamua kuwakaribisha wawekezaji kujenga, kuendesha na kukabidhi ( Build, Operate and Transfer (BOT) basis.)

Hapo awali mradi huo ulipangwa kufanyika kwa pesa za serikali lakini kutokana na gharama kubwa za mradi huo wameamua ufanywe na mwekezaji ambapo gharama hizo zitarudi kwa watumiaji wa barabara kwa kulipa tozo kama inavyofanyika kwa daraja la Mwalimu Nyerere(Kigamboni bridge).
Katibu mkuu Mhandisi Joseph Kamhanga amesema kuwa mradi huo haujasitishwa wala kusahauliwa ila kwa sababu ya ukubwa wake serikali Inahitaji muda wa kuweka kila kitu sawa.

Barabara hiyo itaanzia Bandari ya Dar kupitia Mbagala kuelekea Pugu, Kisarawe, Kibaha na kufika Chalinze. Nyamhanga alisema pia mradi huo utakamilika katika kipindi cha miaka minne.

The Guardian 7th January 2017
 
tumeshauza madini na kila kitu,sasa tunauza na barabara!!

aliyenadi serikali yake ni ya wanyonge na maskini na hana urafiki na matajiri yupo wapi??

Nauli za mabasi itakuwaje? Huo utaratibu kwa barabara nyeti na moyo wa nchi ni ufisadi usiokubalika,daraja la kigamboni tu wanalia ughali wakati ni almost 2km tu,je 150km?!
 
Kwahiyo wanakimbia hiki kipande cha barabara ya Morogoro? Mh Rais alisema wamepata fedha za ujenzi wa barabara kutoka Kimara hadi Kibamba. Leo unatajwa mradi mwingine.
Anyway, uwekezaji kama huo kwa barabara hiyo, labda target ni magari ya mizigo. Na gharama siku ya mwisho zinakwenda kwa mlaji hizo watakazolipa wenye magari.
Lakini pia na ule mpango wao wa treni kushushia mizigo Ruvu sijui umefutwa au vipi.
Nchi hii kwa mipango!!!!
 
Hatukatai ubia na mashirika binafsi lakini umakini unahitajika ila kulipisha tozo kwa kila mtumiaji itakuwa ni mzigo kwa wananchi na tutalipa kwa miaka mingapi na kwa riba ipi isijekuwa mikataba ya kilaghai
 
Wajenge tu, gharama watalipia wenye mahitaji kama ilivyo kwa daraja la kiga na njia za mwendokasi
 
Eti mwekezaji katika barabara,tumejaa up mba v, bora tusiwe na serikali tu apewe mwekezaji akusanye kodi na afanye ujenzi wa miundombinu na mengineyo yote yanayoihusu serikali kwa wananchi.
 
Hizi ni dalili za serikali kufilisika hadi inakimbia majukumu yake ya kimsingi. Ile barabara nyembamba ya Dar to Chalinze imeua watu wengi sana (RIP Regia Mtema) bora serikali ingefanya mradi huu kwa awamu ili kupunguza msongamano na athari za kiuchumi
 
Kungekuwa na taasisi inayotoa cheti kwa nchi yenye mipango mizuri, Tanzania tungeongoza
 
Eti mwekezaji katika barabara,tumejaa up mba v, bora tusiwe na serikali tu apewe mwekezaji akusanye kodi na afanye ujenzi wa miundombinu na mengineyo yote yanayoihusu serikali kwa wananchi.

Kuwekeza kwenye barabara hua unaleta maendeleo NA Mara nyingi hua haungiliani NA barabara za wananchi, mara nyingi hua ni Barabara mbadala.

Tunayo barabara ya kawaida ambayo haina malipo , sass iwapo unataka njia ya mkato basi Hizo za kulipia zinakuwa mbadala.

Barabara za serekali ni lazima zipitie sehemu nyingi ili kuhudumia jamii nyingi za vijijini.
 
"Tanzania ya Magufuli itakuwa Tanzania ya viwanda"; baada ya kuapishwa na kuwa Rais, "Mifuko ya hifadhi za jamii iache kuwekeza kwenye majengo ijenge viwanda".

"Serikali yangu itajenga barabara ya njia sita kuanzia Kimara mpaka Chalinze"; baada ya kuapishwa kuwa Rais, "Tunatafuta muwekezaji ajenge barabara ya njia sita mpaka Chalinze".

Pumzi inakata taratibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…