KWELI Bangi inaweza kutumika kwenye kutibu baadhi ya Changamoto za Wagonjwa wa Saratani

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Inaaminika kuwa bangi inaweza kutibu aina mbalimbali za saratani mwilini, na baadhi ya watu huitumia wakiwa na imani hiyo.

Tunataka kufahamu ukweli wa jambo hili, pamoja na uthibitisho wake kisayansi.

1657969362554.png
 
Tunachokijua
Bangi ni zao lenye mjumuiko wa kampaundi zaidi ya 100 zenye athari tofauti kwenye afya ya binadamu. Kampaundi hizi hufahamika zaidi kama cannabinoids.

Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa na Vyakula ya Marekani (FDA) imeruhusu matumizi ya baadhi ya kemikali za mmea huu katika kutibu kifafa na degedege kinachoanza kwenye umri mdogo ambacho huchangiwa na joto kali la mwili, udumavu, kukosa usingizi mzuri pamoja na ulegevu wa misuli ya mwili.

Hakuna uthibitisho wa moja kwa moja unao elezea uwezo wa kemikali za mmea huu katika kutibu aina mbalimbali za saratani mwilini.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Kituo cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa cha Marekani (CDC), mmea huu unaweza kutumika katika kupunguza maumivu makali ya mwili hasa kwa watu wenye saratani pamoja na kuondoa maudhi ya kutapika, kiungulia na kichefuchefu ambayo husababishwa na dawa wanazotumia.

Kutokana na uwepo wa athari zingine hasi kwa afya ambazo nyingi huanzia kwenye ubongo, Serikali za nchi nyingi duniani huuweka mmea huu pamoja na kemikali zake kwenye jedwali la kwanza la dawa na kemikali zinazohitaji udhibiti mkali wa matumizi.

Aidha, kwa mujibu wa utafiti wenye kichwa cha habari "Cannabinoids in cancer treatment: Therapeutic potential and legislation" wa Barbara Daris et al (2019), kemikali za cannabinoids zinazopatikana kwenye bangi zinaweza kudhibiti ukuaji wa uvimbe wa saratani kwenye majaribio ya maabara.

Huu ni ushahidi wingine unaoonesha umuhimu wa mmea huu unaoweza kutumika kwa faida kubwa kwenye miaka ya mbeleni katika kupambana na janga la saratani duniani.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom