Bandari za Bagamoyo na Mwambani tusizipuuze

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,983
11,402
Wakati JK anaondoka ikulu aliacha miradi mikubwa miwili mezani ambayo ni mradi wa ujenzi wa bandari mpaya ya Bagamoyo na mradi mpya wa bandari ya Mwambani Tanga. Iwapo miradi hii ikikamilika Tanzania itakuwa na uwezo ma kupitisha tani milioni 27 kwa mwaka ukilinganisha na Kenya wenye uwezo wa kupitisha tani milioni 14 tu na hawana namna nyingine ya kuongeza uwezo huo.

Kwama miradi hii ikifanikiwa basi Tanzania itakuwa na uwezo wa kuhudumia nchi zaidi ya kumi na moja, kwa mapato haya tutakuwa tumefika nchi ya uchumi wa kati na tukikomaa kidogo tunaweza achana na umasikini.
 
Habari njema sana hizi. Sina shaka JPM atakomaa kuhakikisha miradi hii na mingine inakamilika. JPM ana nia ya dhati na pia uwezo anao wa kuifikisha nchi hii kwenye uchumi wa kati. Watz almanusura wafanye kosa katika uchaguzi wa rais lakini walizinduka na kumchagua JPM. Mungu ashukuriwe.
 
Subirini kwanza tuboreshe barabara, reli na viwanja vyetu vya ndege, maana bila kuimarisha hiyo miundombinu mizigo mingi kiasi hicho itasafiri vipi
 
Wapo watu wanaoponda sana hiyo miradi bila kuangalia kwamba Tanzania ya miaka 100 ijayo inapaswa kujengwa sasa! Wapo watakaokuambia hakuna haja na bandari ya Bagamoyo na badala yake ipanuliwe ya Dar es salaam huku wakisahau ukubwa wa bandari ni pamoja na container handling na container handling inategemea ukubwa wa eneo! Hawa ni wale wanaosahau au hawafahamu kwamba pamoja na Bandari ya Dar es salaam kuwa na eneo dogo la ku-handle containers lakini tayari bandari imeshameza maeneo kadhaa ya Kurasini. Kusema ipanuliwe bandari ya Dar es salaam ni sawa na kusema zaidi ya nusu ya wilaya ya Temeke ibadilishwe na kujengwa container terminals!!

Si tu kwamba Dar es salaam imeshaishiwa na maeneo lakini pia mkono wa bahari unaoingia Bandari ya Dar es salaam wala hauoenekani kwamba utakuwa na uwezo wa ku-handle 21st century megaships! Hata Bandari ya Mtwara, so longo as itatumika sana na tankers; then the rational decision is to leave Mtwara Port na mimeli yake ya gas manake na yenyewe ile huwa ikifunga nanga; mnasahau kwahiyo haipaswi kuingiliana na non-tankers ships.

Solution ya yote hayo ni kuwa na alternative location na tukiweka siasa pembeni, Bagamoyo panafaa zaidi.
 
Subirini kwanza tuboreshe barabara, reli na viwanja vyetu vya ndege, maana bila kuimarisha hiyo miundombinu mizigo mingi kiasi hicho itasafiri vipi
barabara ya Arusha moshi tanga hadi dar ni mpya na ya kisasa kabisa, barabara ya arusha babati singida nayo ni mpya kabisa, barabara ya chalinze hadi rwanda nayo lami, kimsingi nchi zote washirika wanafikiwa kwa barabara ya lami.
 
Unachosema ni sahihi, bandari ya tanga inaweza kuwa maalumu kwa mizigo ya uganda, bandari ya mwambani ikawa maalumu kwa rwanda burundi congo na banadri ya bagamoyo ikawa maalumu kwa zambia zimbabwe na dar ikabaki kwa local supplies.
 
barabara ya Arusha moshi tanga hadi dar ni mpya na ya kisasa kabisa, barabara ya arusha babati singida nayo ni mpya kabisa, barabara ya chalinze hadi rwanda nayo lami, kimsingi nchi zote washirika wanafikiwa kwa barabara ya lami.
Mzigo mkubwa kama huo ukitumia barabara tu utaharibu barabara katika muda mfupi tu lakini pia gharama za kusafirisha ni kubwa ukilinganisha na reli
 
Mzigo mkubwa kama huo ukitumia barabara tu utaharibu barabara katika muda mfupi tu lakini pia gharama za kusafirisha ni kubwa ukilinganisha na reli
tayari reli ipo chini ya uongozi wa Kadogosa na sasa mambo yanaenda vizuri, limeongezwa jembe jingine RAHCO, bado ujenzi wa reli ya SGR uko palepale.
 
tayari reli ipo chini ya uongozi wa Kadogosa na sasa mambo yanaenda vizuri, limeongezwa jembe jingine RAHCO, bado ujenzi wa reli ya SGR uko palepale.
Sasa ndiyo maana nasema tuwape muda waboreshe vizuri miundombinu ndiyo waanze ujenzi wa bandari au kama pesa ipo vyote viende pamoja
 
Unachosema ni sahihi, bandari ya tanga inaweza kuwa maalumu kwa mizigo ya uganda, bandari ya mwambani ikawa maalumu kwa rwanda burundi congo na banadri ya bagamoyo ikawa maalumu kwa zambia zimbabwe na dar ikabaki kwa local supplies.
Mchina ameingalia mbali zaidi ya hapo... yeye lengo lake ni kuhodhi biashara Afrika na ili kufikia hayo ameamua kuigawa Africa into different ocean gateways ili ku-handle business ndani ya eneo husika. Anachoangalia Mchina ni kwamba East Africa(including Rwanda & Burundi) pamoja na Zambia, Malawi, na DRC lote ni eneo moja kibiashara ambalo ili kupunguza transportation and logistic costs basi mzigo kwa ajili ya nchi zote hizo ufikie sehemu moja! Kwahiyo anachotaka mzigo wake yeye kama yeye (Mchina); anafungasha mamilioni ya tani kutokea huko kwao kisha unakuja kumwagwa Bagamoyo. Kutokea Bagamoyo, mzigo wa Zambia utaenda Zambia... wa Uganda utaenda Uganda, wa Rwanda utaenda Rwanda n.k!

Shipping Lines zingine zooooote wataamua wenyewe.... kama ni kupitia Tanga, Dar es salaam, au hata Mtwara! Lakini yeye kama yeye (Mchina) ana ndoto za kuwa na one point of exchange ambayo si tu ina harbor mzuri lakini pia kuna eneo la kutosha kuweza ku-handle cargo ya ukubwa wowote. Na hili kuhakikisha efficiency, ndio maana kila anapotupia jicho; suala la ujenzi wa reli ya kisasa linakuwa ni part of the program. Kutokana na ukweli huo; ndio maana sijui umshawishi vipi Mchina hadi aka-opt kuichagua Bandari ya Dar es salaam.

So, Mchina akifanikisha Bagamoyo, serikali nayo ikafanikisha Tanga (pale kuna projects 2) kitakachotokea ni alternative za kutosha kulingana na karne iliyopo. Wapo watu wanaodhani kwamba bandari 3 au 4 ni nyingi sana huku wakisahau kwamba hata hii bandari iliyoelemewa inahudumia mataifa masikini yenye low purchasing power. Wanasahau purchasing power ikiongezeka, imports na exports nayo itaongezeka automatically kwa sababu shida haitakuwa tena umaskini bali a chain of products available in the market! Watu wanasahau kwamba, leo hii ukisema ugawe Sh. 10 Million kwa kila Mtanzania basi kwa haraka haraka angalau Smart TV 1,000,000 zitanunuliwa within one month thus demanding more importation and thus, more transportation of Smart TVs kuja Tanzania!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…