ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 62,253
- 72,512
Kwa mujibu wa jarida la The Standard likinukuu taarifa Kutoka The Ports of Africa ni kwamba Bandari ya Dar imezidiwa na meli kiasi kwamba hadi jumanne ya wiki hii ya Disemba kulikuwa na meli 38 zinazosubiria kushusha mzigo.
Aidha imefikia mahala muda wa kusubiria unafikia siku 30 jambo ambalo limeleta hofu ya gharama za kukomboa bidhaa.
Kutokana na Hali hiyo, meli nyingi ambazo zilikuwa zitie nanga kwenye Bandari ya Dar zikiwa na mzigo wa Tanzania na Nchi majirani zimelazimika kuanza kwenda kushushia mizigo Bandari ya Mombasa Kenya ambayo inaonekana Ina nafasi.
Ikumbukwe hii ni disemba ambayo Huwa na mizigo Mingi sana Kwa Ajili ya matumizi ya msimu wa mwisho wa mwaka lakini TPA hawafanyi jitihada za kukabiliana na seasoned cargo volumes.Huku ni Kuchezea Uchumi wa Nchi kama sio hujuma.
Swali Kwa Mamlaka na TPA.
Hivi mumeshindwa kabisa kuondoa tatizo la msongamano ambao unaongea gharama za bidhaa na kutatuza Ufanisi wa Bandari yetu?
Kama tatizo ni nafasi ndogo ya Hiyo Bandari, Serikali inajivita vuta Kwa nini kuanza Ujenzi wa Bandari kubwa ya Bagamoyo?
Uchumi unazidi kukua wa ndani ya Nchi na Nchi jirani aelfu ya mizigo yatalazimika kupita hapo Sasa mbona sioni jitihada za kuwa mbele ya mda badala yake tunafanya kazi ya zima moto?
Kama shida ni uchache wa gati na space ndogo ya Bandari sitarajii Ufanisi wowote kutoka DP World Kwa sababu tatizo la msingi ni ufinyu wa nafasi.
Ni jambo la kusikitisha kwamba tunafukuzana na wauza mikaa,mama ntilie nk wakati tunachezea Uchumi wa Jiografia Kupitia Bandari zetu.
Inasikitisha sana.
View: https://twitter.com/StandardKenya/status/1732724180854993029?t=QEC5GMSCcoQNO8FW0fWYnw&s=19