A
Anonymous
Guest
Bandari ya Dar es Salaam ina changamoto kubwa ya mizigo kuchelewa, hii ni kero ambayo imekuwepo kwa miezi kadhaa sasa na Serikali na mamlaka zipo kimya, kiasi kwamba imefikia hatua baadhi ya watu wenye meli kubwa wanaamua kwenda Mombasa.
Mimi ni mmoja wa waathirika wa changamoto hiyo, kuna mazingira ya urasimu yanayoendelea Bandarini.
Kwa kawaida mzigo unatakiwa kutozidisha wiki moja au au mbili lakini kwa sasa kukaa zaidi ya mwezi au miezi miwili au mitatu.
Kampuni ninazofanya nazo kazi kwa ajili ya kutoa mizigo zimekuwa zikilalamika kuzungushwa na wanaohusika, inavyoonekana kuna mchezo wa kukomoana.
Kuna ndugu yangu naye ameagiza mzigo umefika Bandarini tangu Novemba 2023 na alitarajiwa kuutoa Desemba 2023 lakini hadi sasa Januari inaelekea Februari 2024 mzigo haujatoka na hakuna maelezo anayopata ya maana kama ninayopata mimi.
Baadhi ya Maafisa wengine wanadai makontena ni mengi ndio maana hata mchakato wa kutoa unakuwa taratibu.
Jambo lingine ni kuwa baadhi ya Maafisa wa Bandari wamezidisha tabia ya kuiba vifaa na mali zinazoingizwa kwa kigezo kuwa wanakagua na kupima ubora.
Wamekuwa wakifungua baadhi ya mizigo kwa lengo la kukagua, kinachotokea baada ya hapo wakiondoka na sample hiyo hawarudishi, hivi wanadhani sisi tunapewa bure huko zinazotoka.
Pia, soma: Bandari ya Dar Es salaam sasa inafanya kazi 24/7
2. Mkurugenzi wa Bandari ya Dar asema "Hali ni shwari Bandari ya Dar es Salaam, operesheni zinaendelea"