JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,227
- 5,281
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mette Nørgaard Dissing-Spandet ameitembelea JamiiForums (JF) na kufanya mazungumzo na Uongozi na Watendaji wake ikiwa ni pamoja na kujionea maendeleo ya Taasisi akiwa kama Mshirika muhimu wa JF.
Pia, Balozi amefika JF kwa lengo la kuaga rasmi ikiwa ni baada ya kumaliza utumishi wake nchini. Balozi Mette na Serikali ya Denmark wamekuwa wadau muhimu kwa JF katika shughuli mbalimbali.
JF inamtakia kila la heri Balozi Mette katika majukumu yake mengine atakayokwenda kuendelea nayo baada ya kuondoka Tanzania.