Mkunazi Njiwa
JF-Expert Member
- Apr 22, 2023
- 7,451
- 6,570
China ya KIKOMUNISTI ina historia nzuri sana ulimwenguni.
Leo nitazungumzia kisa cha kusitishiwa heshima kwa komredi Liu Zhidan aliyekuwa mtu muhimu ndani ya chama cha CCP.
Kisa cha Liu Zhidan
Alikufa akiwa na heshima na "TITLE" ya mfia nchi na shahidi wa harakati za umma (martyr) lakini kufikia 1962 kukatokea kisa cha kushtusha.
Katika kitabu chake cha maisha yake "shajara" ya hati yake mwenyewe kulikutwa maneno ya KUMZODOA na KUMDOGOSHA komredi wa zamani GAO GANG kwa kumuonyesha kama mtu asiyekuwa wa thamani sana kiharakati kuliko anavyotukuzwa.
Ni nani "aliyemlipua "hayati Liu Zhidan. Ni komredi Kang Sheng, kiongozi mwaminifu wa ndani kabisa wa chama cha CCP, akiwa mkuu wa "internal security and intelligence apparatus".
Kufikia hapo kamati kuu ya chama na wanachama wa CCP wakamuondolea heshima yake aliyozikwa nayo na kuwa tu mwanachama wa kawaida akiwa hukohuko kaburini
Hapa tunajifunza nini?
Balozi Ali Karume bado yuko hai ,heshima yake ni kubwa ndani ya JMT. Ametumia muda mrefu wa maisha yake kujifunza na kuiishi DIPLOMASIA na kuwa faida kubwa kwetu watanzania.
Anakijua vyema CCM na mwendelezo wake wa kumkomboa mtanzania kwa kumfungamanisha vyema na utukufu wa ardhi yake.
Vijana tunashangazwa na maneno yake dhidi ya viongozi wa CCM.
Kufikia kilele cha kushtua anasema kuwa hawezi kufukuzwa chama na "watu wakuja tu"
Hili si dogo. Mtu wa kuja ni nani?
Kweli nchi hii inaweza kuwa na kiongozi wa ngazi yoyote ile wa "sampuli" hiyo?
Tuachilie mbali makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar?
Huku ni "kufurutu ada" kwa kuwadogosha viongozi wa chama ,wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla.
Madhara yake
Siku ile pale uwanja wa uhuru ,umma wa Tanganyika ulishuhudia kushushwa chini kwa bendera ya mkoloni wa kiingereza (Union Jack) na kupandishwa kwa NEMBO ya utu wa watanganyika.
Baba wa taifa akiwa bado ni waziri mkuu alisema kuwa "....tumejikomboa na madhila, mateso na manyanyaso ya wageni. Leo kila aliyekuwepo ndani ya Tanganyika ni mtanganyika, awe MWARABU, MWASIA, MZUNGU, MWAJEMI... wote hao ni SAWA na kila asiye na uhusiano nao wa kidamu....".
Miaka miwili baadaye Zanzibar inapata Uhuru wake kutoka kwa mwingereza...1964 serikali ya waziri mkuu SHAMTE MBONDE inapinduliwa na wazanzibari waliotaka uhuru zaidi kwa kila mmoja na kuondoa "siasa za ubaguzi ,uasili ,urangi".
Tokea miaka hiyo wazanzibari ni WAMOJA na ikumbukwe vile ni visiwa ,kabla ya hapo kulikuwa na watu waitwao WAHADIMU (kutoka huku bara ) kulikuwepo na WANYASA * WAMAKONDE ,WANGAZIJA na wengineo.
Niliwahi kuhudhuria sherehe za MWAKAKOGWA (kuoga mwaka) huko Makunduchi na sahibu yangu kwa jina la utani "Jaje".Huko ni kwao na akaamua kunichukua nikaone ustaarabu wa huko....nilipata kukaa na wazee wa kimakunduchi na ile lahaja yao tamu na ya "kufurahisha" wakanifungua ubongo wa mengi tusiyoyajua vijana haswa wa huku kwetu Tanzania bara.
Karne hii ya 21 na Mapinduzi ya TEHAMA na akili mnemba unathubutu kumbagua mtu kwa ASILI yake ?!!
Tena mtu huyo na wengine ni VIONGOZI wenu wakuu ?!!
Ubaguzi wowote ule ni USHETANI ULIOPITILIZA, uwe ni wa KABILA, RANGI, WAJIHI, RANGI YA NGOZI, UMBILE, DINI, MADHEHEBU ama KANDA.
Ningewashangaa sana CCM kutokumfukuza uanachama mzee wetu komredi Balozi Ali Karume kwa sababu huko CHINA kunakofanyika "FOCAC" huwa HAWAVUMILII yanayofanana na haya ,wao wanafikia hata KUMUONDOLEA mtu heshima kuu aliyokuwa nayo wakati wa uhai wake wa kulitumikia DOLA lao ,wamefanya mengi likiwemo hili la kumfutia TITLE ya "ufia umma- martyr" hayati komredi LIU ZHIDAN akiwa kaburini kwake.
FUNZO KUU
Inashangaza kuona baadhi ya wazee wetu na vijana wenzetu wakikosa HIMA ya kujifunza na kuiishi historia KUNTU ya taifa letu takatifu.
Kutwa kusigana wenyewe kwa wenyewe na mbaya zaidi kutukana VIONGOZI kwa kedi na kiburi cha KUCHUSHA kisa tu kuwa na migongano na ukinzani wa mawazo....hakika inaumiza kwani tukijifanya tunaipenda ARDHI ya JMT tutawabaguaje viongozi wake kwa sababu dhaifu za "asili zao ,makabila yao ,kanda na dini zao " ?!!
Mchanga wa ardhi ya Tanzania ndiyo IMANI ya kwanza kabla ya mambo mengi kwani juu yake ndipo tunapoendesha MAISHA YETU ,SIASA ,kufanya ibada katika misikiti ,makanisa ,matambiko na mizimuni petu.
#Uwe wa kwanza kuipenda Tanzania
#Pinga ubaguzi wa aina zote
#TUHESHIMU VIONGOZI WETU KWANI NDIO NGAO YETU
#Serikali mbili za JMT milele dumu ,aaamin aaaamin