Balozi Ami Mpungwe anapata wapi ujasiri kuwaita wengine "majipu"?

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Balozi Ami Mpungwe,mwanadipolomasia na mtumishi wa umma wa miaka mingi.Alikuwa balozi wetu wa kwanza wa Tanzania nchini Afrika Kusini,Ami Mpungwe ndiye aliyekabidhiwa na chama cha ANC kukaa na Nelson Mandela week nzima Manyara National Park wakati Mandela akiwa kwenye mfadhaiko mkubwa wa ndoa yake na Winnie Mandela.

Kwa ukweli Balozi Ami Mpungwe katika harakati na ukombozi wa kusini mwa Afrika hakuna asiyemfahamu,Jongwe Robert Mugabe,Thabo Mbeki,Comrade Pohamba,Jacobo Zuma na kina Kenneth Kaunda ni moja ya watu wanaomfahamu Mpungwe kama mmoja wa "vijana" wa Mwalimu Nyerere aliyepigania ukombozi wa nchi zao na kuufukuzia mbali ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini.

Lakini ukisema utaje watu waliotumbukiza nchi hii katika matatizo ya "uwekezaji wa makaburu" basi jina la mwana Ifakara Balozi Ami Mpungwe halikosi kuwepo,juzi ameonekana kwenye TV na wameitisha kipindi Maalumu ITV kuelezea kupanda kwa bei ya sukari,na kuwaelezea watu wanaoingiza sukari toka nje kama ni "Majipu yaliyoiva muda mrefu na kukosa kutumbuliwa",kauli hii si ya kutolewa na Balozi Mpungwe huyu tunayemfahamu.

Balozi amekuwa kama wakala wa wawekezaji "wanyonyaji" huku yeye akiwekwa kama "Non-Executive Director" ili kulinda maslahi ya wawekezaji hao.

Mfano wa Mashirika ambayo Mpungwe amewekwa kama "Buffer zone" yao dhidi ya Serikali ni kama:
-Tanzanite One
-Multi Choice Tz
-Illovo Sugar hawa wanamiliki Kiwanda cha Kilombero
-Tanzania Breweries
-NBC Tanzania Ltd(1997)
Air Tanzania Ltd(Hii aliiuza kwa South Africa Airways matokeo yake shirika letu likafa kifo cha mende
African Gem Resources
-TANESCO(Ndio aliwaleta Net Group Solutions kwa mtutu na wakaiharibu Tanesco).

Na kwasasa ni mwenyekiti wa Wazalishaji wa Sukari Tanzania,katika mashirika yote hayo aliyokaa hali kwa wazawa ilikuwa mbaya,kule Tanzanite One tumeona jinsi wafanyakazi walivyodhulumiwa na kuishi kwa tabu,mpaka sasa Tanzanite ikaonekana inatoka Kenya na S.Africa.

Sisi washabiki wa mpira tunajua jinsi DSTV ya Multi-Choice ilivyotulipisha kwa dola badala ya shilingi,wafanyakazi wa Kilombero na ugumu wa mazingira ya kazi.

Tunajua jinsi Air Tz ilivyochomekwa ndani ya South Africa Airways na kuiua kabisa,sasa South Afrika ndege yao inakuja mara mbili kwa siku Dar es Salaam wakati ATCL ipo mahututi,"Ujanja Ujanja" huu wa Comrade Mpingwe aligunduliwa na Balozi Abas Sykes wakati huo Sykes ni Mwenyekiti wa bodi ya ATCL akanusa jinsi Mpigwe anavyotaka "kuliuza" shirika,Kwa uchungu Sykes alisema "Mpigwe ni kijana wetu,tumemtuma Afrika Kusini akawe muwakilishi wetu,lakini amegeuka kuwa wakala wa makaburu na kutka kuliuza shirika letu,vijana wa sasa wanawaza maslahi yao badala ya maslahi ya Taifa",matamshi haya yalimfanya Balozi Mpingwe amfungulie kesi Balozi Abasi Sykes na Gazeti la Mtanzania,kesi iliunguruma Mahakama kuu kwa muda.

Huyu ndio balozi Mpingwe,Mwanadiplomasia wa kweli,Jongwe wa kusini mwa Afrika katika harakati za Ukombozi,mwana Ifakara kindakindaki na "wakala" wa makampuni yote ya makaburu Tanzania,anapata wapi kuwaita wengine "majipu" wakati yake mengi watu bado hawajayafumua??
 
Achana na Tanzania mkuu, kama marope anaweza kumponda JK na utawala wake ni kipi hakiwezekani!?
...mind you, na JK naye nasikia etui anataka kutumbua majipu.
 
Achana na Tanzania mkuu, kama marope anaweza kumponda JK na utawala wake ni kipi hakiwezekani!?
...mind you, na JK naye nasikia etui anataka kutumbua majipu.
Mkuu lukindo tunaondokaje hapa kwenda hatua moja mbele??
 
Chenge mwenyewe anatumbua majipu hii ndio TZ mkuu wangu.
 
Mie sioni tatizo mtu kubainisha majipu anayoyafahamu ili yatumbuliwe katika.serikali imara.isiyo na simile na majibu,hapa kazi tu
 
Nimesoma sakata la TBL kweli hii nchi anaehubiri uzalendo hakuna..
 
Duh@Barafu upo Detailed...Aisee ndio maana huyu mzee Tajiri saana amejenga bonge la 'home' ufwekeni mwa bahari karibu na LAMADA Hotel kawekewa mpaka mtaa wa kuingia kwake...Duh...alichukuwa mkopo FBME wa 2billion kwa ajili ya hotel yake huko kilombero akaa kaa kama miaka mitatu halipi na kuchangia katika kuimaliza hiyo benki inayoweza kufungwa wakati wowote kuanzia sasa...aisee ili zaidi ya JIPU....
 
Mkuu umenena vyema.
Ila kwa kuongezea katika hayo mazuri kumhusu balozi mpungwe ni pamoja na ukweli kwamba ni Balozi wa "kwanza" Tanzania kustaafu kazi hiyo akiwa katika kituo cha Afrika kusini huku akiwa na umri wa miaka 48.

2. Wakati huo katikati hadi mwisho wa 1900) magazeti la Rai na Mtanzania enzi za akina Ulimwengu na Dr shoo, Rweyemamu na Mbwambo walikuwa hawaivi naye hususan namna ATCL ilivyouzwa kwa makaburu.

3. Serikali ya Che Nkapa ilikuwa katika vifganja vya mkono wake huku akichagua akune wapi, lini na nani
 
Mkuu lukindo Tunaondokaje hapa kwenda hatua moja mbele??
Haya maneno hapa chini nadhani umaweza kumjua aliyeyasema kwa kuangalia picha yake mkuu barafu. Hebu hapo kwenye 'white man' weka 'ccm'.
Ni kwa njia hiyo tu tunaweza walau kuanza kwenda mbele. Hivi we fikiria, mkakati wa JPM ni kupambana na rushwa lakini akiwa ndani ya ccm hiyo hiyo, anashirikiana (sijawa na uhakika) na wenzake kuzuia UKAWA wasipate umeya wa majiji ili kubaini ufisadi na ikiwezekana kuuondoa.


 
Ukiwa timu moja na Magufuli hata kama wewe ukiwa fisadi papa sio jipu, tena kuna mengine kama Simbachawene ya yenyewe yanatumbua majipu mengine. Hii dhana ya kutumbua majipu ni kwa wale wasio timu Magufuli, hutakaa kusikia Mwakyembe au Muhongo anatumbuliwa. Sisi cha muhimu turudishiwe hela zetu haijalishi zimetoka wapi
 
Kama wanakuambia Magufuli ni mtu wa watu mchapakazi rais wa wote huku wanapiga makofi wana ukawa utafikiri ni wa kutoka nchi jirani, hii nchi ni kichwa cha wendawazimu full.
 
Ukishiba dhuluma dhambi na laana huwa vinaandamana nawe kokote uendako na ndivyo alivyo huyu mtu! amekuwa KUWADI wa mali, maisha na urithi wa wa TZ bila aibu hata kidogo!
 
Mkuu lukindo nimeyaona maneno ya Malcom X,nimeuelewa mfano wako...kuwa huyu anayepinga ufisadi na kujinasibu kuwa tumuombee kwa Mungu,ndio huyo yuko kimya pale wakati wabunge na madiwani wa chama X kisicho chake wanapotaka kupewa mamlaka ili wamsaidie kutumbua majipu,yeye anazuia upatikanaji wa hayo mamalaka
Nyuma ya pazia anapanda jukwani anasema "Nitafanya kazi na watu wote,iwe CUF,iwe CHADEMA na hata wasio na vyama".....Akipigiwa makofi anaongeza anasema "Mimi ni Rais wa Watanzania wote,bila kujali vyma vyao"....halafu kesho anasema "Nataka nifutilie mbali vyama hivi vya hivyohovyo vya siasa,kusiwepo tena na upinzani".....anasahau jana alisema "Mimi ni Rais wa CCM na Upinzani,na nitakuza demokrasia kwa kushirikiana na vyama vya upinzani sabbu lengo letu ni moja,kumletea Mtanzania maendeleo"
 
Mpungwe ni fisadi kma chenge amekwiba sana cnc 1995 hku tanzaniteone ndio mahali kapata hela nyingi sana hayo majumba yke ni tanzanite yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…