Bajeti ya Wizara ya Madini Imegusa Kila Sekta Hasa Wachimbaji Wadogo wa Madini Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,616
1,196

MHE. MASACHE KASAKA: Bajeti ya Wizara ya Madini Imegusa Kila Sekta Hasa Wachimbaji Wadogo wa Madini Nchini

"Serikali imewasilisha bajeti nzuri ya Wizara ya Madini maana imegusa kila sekta hasa kwa wachimbaji wadogo. Mimi natokea Wilaya ya Chunya palipo na Wachimbaji wadogo nimeona Serikali imewekeza kufanya utafiti maeneo ya wachimbaji wadogo na kutenga maeneo ili baada kuwapa vifaa na mitaji kuweza kuwainua wachimbaji wadogo" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa

"Serikali kupitia Wizara ya Madini inaenda kuimarisha maabara zitakazoweza kuwasaidia wachimbaji wadogo na wa kati kuhakikisha wananchi waweze kunufaika. Mimi kama Mbunge naendelea kuiambia Serikali ipunguze kodi na tozo mbalimbali zinazoendelea kuwaumiza wachimbaji wadogo" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa

"Wachimbaji wadogo wanazalisha lakini ukiangalia maisha wanayoishi hayaendani na kile wanachozalisha. Tunaendelea kuishauri Serikali iweke mazingira mazuri zaidi ili tozo na kodi ziweze kupungua ili wachimbaji wadogo waweze kunufaika" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa

"Kwenye wachimbaji wadogo hakuna msemaji wa mwisho, anaweza kwenda mtu wa Zimamoto (Fire) akasimamisha uzalishaji, au OSHA au Mwenyekiti wa Kijiji. Hili jambo haliwezekani, hao wengine wote ni wadau kwenye sekta ya madini. Serikali ihakikishe ikiona mapungufu waende kwa Afisa Madini Mkazi ili yeye awe na maamuzi ya mwisho" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa

"Kumekuwa na changamoto ya utoroshaji madini, eneo la Chunya mara kadhaa limeripotiwa watu wamekamatwa lakini tumeiambia Serikali mbinu wanazotumia kuzuia waangalie kiini cha utoroshaji ni nini. Ukienda BoT kuuza dhahabu wanakutaka TIN, NIDA. Mtu akileta madini yake wewe nunua mengine yaendelee, sehemu zingine haya mambo hayapo ndiyo maana utoroshaji unaendelea" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa
 

Attachments

  • y2mate.com - Habari za Saa Saa Saba na Dakika 5530 Aprili 2024_1080p.mp4
    90.6 MB
Back
Top Bottom