Unajaribu kuwa mtabiri lakini natumia staha kwa kukwambia ni vyema ukauliza kuliko kubashiri kwanza ufahamu hakuna mkataba rasmi kati ya mtoa huduma na mtumiaji kuna kitu kinaitwa SLA nitafafanua SLA ni makubaliano ambayo huwa ni kipengele kidogo katika mkataba kinaitwa service level agreement ...hiki humpa mtoa huduma mamlaka ya bila taarifa kwa mpokea huduma Kubadili kwa tija gharama za utoaji huduma bila kuathiri sheria ya mamlaka ya simu na mawasiliano ya mwaka 2003 ingawaji sheria hiyo imeshafanyiwa marekebisho chungu nzima baada ya TCRA kuwa na mamlaka ya udhiti wa makampuni ya simu.
Turudi kwenye hoja yangu ambayo hukuijibu ya PAYE kukatwa kisha pesa hizo kabla sijazitumia nikatwe tena VAT badala ya bank kukatwa maana ndio mlaji.... kwa sasa hilo na reserve maana waziri wa fedha kupitia Mkurugenzi wa TRA wameshalitolea maelekezo kwa mabank. Bwana MkamaP pamoja na kula samaki uwezo wako wa kupambanua mambo haujakomaa!!!!
SLA -service level of agreement inaweza kuwa part ya mkataba ama isiwepo. SLA ni constraints ktk mkataba ila sio kwamba ni mkataba. SLA, kwa mfano inaweza sema kuwa Uptime iwe 99% ama 10%.
Mkataba ni makubaliano kati ya mtumiaji na mlaji. Naamini huu mkataba upo hata kama ni virtually, ama namna yoyote ile ama kwa maneno ama kwa niaba ya, huu mkataba upo.
Kwenye hoja yako ya awali ya PAYE. Nimekujibu virtually, lakini naona jibu hukuliona ngoja niliweke bayana kuwa, hata mwaka juzi kama PAYE yako ilikuwa inapitia bank ilikuwa inakatwa na BANK, kama ADD-ON services kwa bank. Yani ulipokuwa una draw PAYE yako ama kwa cashier ama kwa ATM PAYE yako ilikuwa inakatwa. Jua kwamba, iwe mwaka juzi miaka 10 iliyopita ulikuwa unakatwa, ila hii PAYE ilikuwa haikatwi tu enzi zile za dirishani.
Sasa kinachokuchanganya nafikiri ni kwanini serikali iidai bank kutoka PAYE yako ambayo imeshakatwa. Nafikiri ujaribu kuelewa demarcation. Demarcation ya PAYE yako ni peer-to-peer ndo inaishia, yani ya wewe na serikali. Lakini kwa vile bank wamefanya biashara na wewe kwa PAYE yako basi peer-to-peer ya bank na serikali ni mlinganyo tofauti. VAT sio point-to multpoint. Hapa ni kwamba, bank ina peers wawili bank-to-PAYE na bank-to-VAT ya serikali. Ama kwa namna nyingine hapa nikujaribu kusema ya kwamba kwa vile PAYE yako imeshakatwa kodi basi ukichukua hiyo pesa ukaenda kununua mihogo na viazi basi huyo mfanyabiashara hatakiwi kulipa VAT maana hiyo hela uliyolipa ilikuwa PAYE na imeshakatwa.
Jaribu kuiona service ya ATM ni product kama mihogo, na pia Bank ni muuza product mihogo ama viazi, put it in that way. Ni wazi hela PAYE yako ikiwa bank haikatwi, ila ukinunua product ya bank kama ATM kwa kuwidhdraw bank inakata pesa yako, kwa kuuzia bidhaa hiyo, na kwa vile wamekuuzia bidhaa basi bank anapaswa kupeleka 18% OUT of aliyokukata. Hili limetolowa maelezo sana na watu na viongozi wenyewe , naamini sihitaj kurudia rudia mziki ule ule.