Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,330
- 4,692
Waziri wa fedha, Mwigulu Nchema amesema bajeti inapendekeza kuondolewa kwa ada kwa wanafunzi wanaopangiwa vyuo vya kati na Serikali wakimaliza kidato cha nne, vyuo hivyo ni, DIT, MUST na AITC.
Waziri wa fedha amesema serikali imefikia uamuzi huo ili kuzalisha wataalamu wengi wa fani mbalimbali.
Kumekuwepo na mjadala hapa JamiiForums.com kuhusu wanafunzi wanaopangiwa vyuo na serikali kwend akusoma ufundi kuwa gharama inakuwa kubwa kwa wazazi kwani walitakiwa kuwalipia ada watoto wao katika vyo ivyo ambavyo wamepangiwa na srikali.
=====
Waziri wa Fedha na Mipango amependekeza kuondolewa Ada kwa Wanafunzi waliomaliza kidato cha 4 na kupangiwa kujiunga na Vyuo Vikuu vya DIT, MUST na Arusha Tech kwa lengo la kuongeza idadi ya Wataalamu wenye ujuzi unaohitajika katika azma hizi za Mapinduzi ya 4 ya Viwanda.
Amependekeza kuanzishwa kwa Programu ya Mikopo kwa Wanafunzi wanaochaguliwa na Serikali kujiunga na Vyuo vya Kati vya Elimu katika Fani za Kipaumbele ambazo ni Sayansi, Afya, Ufundi na Ualimu ili kuaanza na Wanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa masomo kwa mwaka 2023/24.
Aidha, Serikali imeendelea kutenga Fedha kwa ajili ya kugharamia Programu ya Elimumsingi na Sekondari Bila Ada ambapo hadi Aprili 2023 jumla ya Tsh. bilioni 661.9 zimetolewa.
Moja ya mjadala wa kutaka kufutwa kwa ada: DOKEZO - Hii biashara ya serikali na vyuo vya elimu vya kati mnayofanya bomu lake linakuja