BAHARI YA MAHABATI.
1)bahari inanimeza.
Wakti mwezi wa chomoza.
Nahisi rufu ya viza.
Bani unanifukiza.
Mchana tena wa kiza.
Bahari ya mahabati,mapenziyo yanishika.
2)mahabati wayo nipa.
Siyo kipande cha papa.
Ukweli mimi naapa.
Kwako sitokagi kapa.
Karibia na nenepa.
Bahari ya mahabati,mapenziyo yanishika.
3)we nuru ya machu yangu.
Na mboni ya jicho langu.
Uwapo karibu ya yangu.
Wafurahi moyo wangu.
Laazizi pambo langu.
Bahari ya mahabati,mapenziyo yanishika.
4)itunze yako ahadi.
Usiharibu miadi.
Mbona wanipa midadi.
Na joto kwenye baridi
Sitokwacha nakwahidi.
Bahari ya mahabati,mapenziyo yanishika.
5)cheka nione kicheko.
Kizuri kilicho chako.
Nifarijike mwenzako.
Faraja kutoka kwako.
Pekee na ipo kwako.
Bahari ya mahabati,mapenziyo yanishika
Shairi=BAHARI YA MAHABATI.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha
0624010160.
iddyallyninga@gmail.com