PakiJinja

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
10,347
22,543
Naona Simba wameamua kutengeneza timu watakayoipitisha njia ya Clement Mzinze. Kila mashabiki wa Yanga walipojaribu kumlaumu Mzinze, utetezi uliotumika kuwapooza mashabiki hao ni kwamba bado mdogo, anakua hivyo apewe muda.

Mashabiki wa Simba wenyewe pia wameandaliwa kisaikolojia kama ilivyokuwa kwa wenzao wa Yanga, ingawa tofauti na Yanga walikuwa na Mzinze, Simba wana timu karibu yote wanayotakiwa waivumilie na kuipa muda sababu bado ni wadogo na wanakua.

Kukua watakua, je watasalimika kwa Mashangingi ya mjini? Kama muonavyo , Aziz Ki karukaruka ameishia na udogo wake kunasa kwa limojawapo, matokeo yake uwanjani anapeperusha mikono tu. Ile fitness, creativity, commitment na hustle yake haionekani kuwa na consistence tena,, inaonekana kama imeanza ku decelerate na ku faint.

Kuna uenyeji na kuijua mitaa ya Jiji na viunga vyake na viota vya starehe, je watasalimika? Kuna jeuri ya mafanikio pale watakapoanza kuhitajika na timu nyingine. Kuna kuhitaji special attention na kujidekeza, je yote hayo mmeyazingatia?

Yanga walianza kuijenga timu huku wakizoa vikombe.

Bado wadogo, wanakua hivyo tuwavumilie.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom