Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 56,915
- 30,960
Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti likiwemo la baba kumuua mtoto wake mwenye umri wa miaka mitatu kisha na yeye kujinyonga.
Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, amesema tukio hilo limetokea Julai 28 mwaka huu katika kijiji cha Sayaka wilayani Magu ambapo mtuhumiwa ambaye pia ni marehemu kwa sasa Kisumo Emmanuel (38) alimuua mtoto wake huyo kisha kuuutupa mwili wa mtoto huyo kwenye kisima cha maji.
Kwa mjibu wa Kamanda Mutafungwa mwanaume huyo alifikia uamzi huo baada ya kumtuhumu mkewe kuzaa watoto na wanaume wengine.
Kamanda Mutafungwa amesema baada ya tukio hilo baba huyo alijinyonga kwa kutumia kipande cha shuka alichokifunga kwenye mti umbali wa kilomita moja kutoka nyumbani kwake.
"Kabla ya tukio hilo la mauaji Julai 26 baba huyo alimpokea mtoto wake aitwaye Lukonys Kisumo kutoka kwa mama ambaye jina linahifadhiwa kwa sababu za kiusalama na Julai 28 ndipo alipopata nafasi ya kuongozana na mtoto huyo umbali wa mita 500 kutoka nyumbani kwake na kutekekeleza mauaji hayo,"amesema DCP Mutafungwa.
Furaha FM