Baadhi ya watumishi wa umma wakaidi agizo la Makamu wa Rais

Binti Msichana

Senior Member
Oct 9, 2016
109
249
Kitendo kinachoonekana dharau na ukaidi wa maagizo ya serikali bbaadhi ya watumishi wa umma bila ya sababu za msingi wamekaidi agizo la Mama Samia Suluhu la kufanya mazoezi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, nimepitia maeneo mbalimbali na kukuta mwitikio mdogo wa watumishi kufanya mazoezi kwa faida ya afya zao.

Labda nivipongeze vyombo vya ulinzi na usalama kwa kujitokeza kwa wingi katika kufanya mazoezi.

Hata mimi siku nyingine napaki gari langu na kutembea kwa miguu ingawa nanyonyesha.
 
Sasa unapoleta huu umbea mtoto ananyonyeshwa na nani? Au ulitaka tujui umenunuliwa baby walker?
 
Apeleke muswada bungeni kulazimisha mazoezi,nchi inaongozwa na sheria.....hakuna sheria ya kuwataka watu wafanye mazoezi.

Kuna siku ambao hawajaoa watapangiwa siku fulani ya wiki wahakikishe wametongoza
 

Binti,umechanganya matamko bhana.
Jumamosi ya mwisho wa mwezi ni usafi kitaifa(agizo la Baba Jesca); agizo la mama Samia ni kila jumamosi ya PILI ya mwezi.

Haya rekebisha sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…