Baadhi ya Vitabu nilivyosoma mwaka 2020 - Zitto Kabwe

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,886
Mwaka 2020 nimejaaliwa kusoma vitabu 16 (2019:34, 2018:49), ni Orodha ndogo sana kulinganisha na miaka ya nyuma. Hii ni kwa sababu shughuli nazo zimekuwa nyingi, ikizingatiwa kuwa ulikuwa Mwaka wa Uchaguzi Mkuu. Muda mrefu tumeutumia barabarani, Vijijini na Mitaani kuzungumza na wananchi. Pia kusoma Taarifa fupi fupi za tafiti za Uchaguzi na pia kuweza kuzalisha Ilani ya Uchaguzi ya Chama ambayo Mwaka huu kwa msaada mkubwa wa Kamati za Ilani tulikuwa na Ilani bora sana kote Jamhuri ya Muungano na Zanzibar.

Vile vile nimesoma ripoti nyingi za Serikali, mashirika ya kimataifa kama Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, IMF na majarida yenye maarifa mengi, Mfano Foreign Affairs ambalo hutoka mara 6 kwa Mwaka. Hata hivyo nashukuru sana nimejikongoja mpaka kufikia vitabu 16.

Mwaka 2020 kilichapishwa Kitabu ambacho kina Sura ambayo nimeandika. Kitabu hicho ni THE NEW SYSTEMS READER: Alternatives to a Failed Economy, Edited by James Gustave Speth na Kathleen Courrier. Sura niliyoandika inazungumzia Ujamaa baada ya Miaka 50 ya Azimio la Arusha (The Arusha Declaration: The Case for Democratic Socialism 50 years on).

Mwaka 2021 nitafanya jitihada kubwa kuandika kitabu kinachosimulia haswa Maisha yangu katika Siasa za Tanzania Katika miaka 15 iliyopita. Ni matamanio yangu kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2022 Kitabu kitakuwa dukani. Mungu atupe uhai, In Sha Allah.

Vitabu vya 2020

Riwaya

Mwaka 2020 nimesoma riwaya 6 tofauti tofauti, za watunzi wa Tanzania na Nje ya Tanzania. 50% ya riwaya hizo zimeandikwa na Watanzania sio tu wanaochipukia Lakini wanaoimarika sana katika uandishi. Naona fahari sana kuwa talanta ya uandishi wa riwaya za kusisimua bado ipo nchini, licha ya mazingira magumu ya Kazi za uandishi. Riwaya nilizosoma Mwaka huu ni Pamoja na;

1. An Orchestra of Minorities: Chigozie Obioma

2. Borderlines: Michela Wrong

3. Beneath Lion’s Gaze: Maaza Mengiste

4. Rafu: Fadhy Mtanga

5. Fumbo: Maundu Mwingizi

6. Tuzo: Fadhy Mtanga, Lilian Mbaga, Maundu Mwingizi, Laura Pettie na Hussein Tuwa

Wasifu (Biographies and Autobiographies)

Mwaka 2019 tulibahatika kupata vitabu vya baadhi ya Viongozi wetu nchini. Rais wa Awamu ya Tatu Marehemu Mzee Benjamin Mkapa aliandika Wasifu wake. Kabla ya hapo Marehemu Mzee Njelu Kasaka, aliyekuwa Mbunge na Katibu wa Kundi la G55 lililotaka Serikali ya Tanganyika alitoa kitabu chake pia.

Mwaka 2020 Wanazuoni waandamizi Prof. Issa GulamHussein Shivji, Prof. Saida Yahya Othman na Dkt. Ng’wanza Kamata walikamilisha Juzuu 3 za Maisha ya Mwalimu Julius K Nyerere, Baba wa Taifa la Tanzania. Juzuu ya 4 ipo njiani. Kazi kubwa na ya kuthaminiwa sana ambayo Wanazuoni wetu wamefanya. Kitabu hiki chenye Juzuu 3 (kimsingi ni vitabu 3 vinavyoweza kusimama vyenyewe) kilitoka wakati muafaka sana kwa kizazi chetu. Sio tu ni kitabu cha kusoma na kumaliza bali ni Kitabu rejea kwa Miaka mingi ijayo.

Mwaka huu pia Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Steven Bwana alichapisha kitabu cha Maisha yake. Kitabu hiki kinasimulia Maisha ya Jaji Bwana kuanzia Kijijini kwao mpaka ustaafu na maono yake kuhusu Tawi la utoaji haki (judiciary) katika Ujenzi wa Taifa. Mwaka 2020 umemalizika kwa kazi iliyosubiriwa kwa hamu kubwa ya Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama. Kitabu kizuri Sana kuhusu Mweusi huyu wa kwanza kuwa Rais wa Taifa kubwa duniani.

Wasifu niliosoma Mwaka huu ni Pamoja na;

7. Julius Nyerere, A Biography: Saida Y Othman, Ng’wanza Kamata na Issa G Shivji

8. Maisha Yangu, Utumishi Wangu: Steven J Bwana

9. A promised Land: Barack Obama

Nilisoma pia Mchanganyiko wa vitabu mbalimbali kama kawaida. Ni katika kuongeza maarifa na kuendelea kujifunza kutoka sehemu mbalimbali za Dunia. Pia katika kujifunza makosa ya wengine ili kutorudia makossa hayo. Vitabu mchanganyiko mwaka huu ni pamoja na;

Vitabu Mchanganyiko

10. Asia aspirations, Why and How Africa Should Emulate Asia -- and What It Should Avoid: Greg Mills, O Obasanjo Et al

11. The Naked Diplomat, understanding Power and Politics in the Digital Age: Tom Fletcher

12. Taxing Africa, Coercion, Reforms and Development: Mick Moore, et al

13. Homo Deus, A brief history of tomorrow: Yuval Noah Harari

14. The Promise of Canada, People and Ideas that have shaped our country: Charlotte Gray

15. How to lose a Country, The Seven Steps from Democracy to Dictatorship: Ece Temelkuran

16. The Room Where it Happened, A White House Memoir: John Bolton

Mwaka 2020 ulikuwa mwaka wenye changamoto nyingi sana zitokanazo na janga la COVID 19 (Korona) mpaka Uchaguzi mbovu kabisa kupata kutokea katika historia ya Tanzania. Hakika hapakuwa na Uchaguzi kwa maana ya Uchaguzi bali operesheni Maalumu ya kusaga saga demokrasia ya Vyama vingi Nchini. Kwangu Binafsi namshukuru Mungu kwa kunisuru na ajali niliyopata Oktoba 7, 2020. Ilikuwa miujiza. Mungu mkubwa Sana.

Nawatakia kheri katika kumaliza mwaka 2020 na kila la kheri katika mwaka 2021. Nawashawishi kupata muda wa kujisomea japo kitabu kimoja kila mwezi. Kusoma ni kurutubisha ubongo. Tunaoweza kuandika pia tuandike.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Dar es Salaam
Disemba 26, 2020

7FC72DC9-CEF1-4E98-BC71-5724D5619636.jpeg
60A64503-6F9A-41A6-A77A-1CBB2695D3DD.jpeg
100B5168-28C5-47AA-8DED-3CAA8CEAF8E7.jpeg
D00ED105-2340-4338-A363-E4886AC9CA79.jpeg
319D631C-85F5-4BC3-A49C-630A5A5644B4.jpeg
982351D9-D0E5-470B-A893-1DB187F7766E.jpeg
92B9666C-F798-4CD8-8310-26BAF20C6C06.jpeg
880556DA-D433-4091-9BDB-2AB25E57DAD7.jpeg
733630AC-24D5-430D-9F91-2236A7BBCA9E.jpeg
4E318E95-E7CE-4F2C-BC4C-8F9BE2BF9BA4.jpeg
 
Hongera sana Mr. Zitto. Tulio wengi tunatamani kusoma vitabu, ila namna ya kuvipata ndiyo ngumu.
Hata hivyo nimepata kitu cha kuondoka nacho, miaka ijao panapo majaaliwa, tutashindana kwa idadi ya vitabu vya kusoma na kuandika.
 
Hongera sana Mkuu.

Ni matumani yangu kwa uzoefu wako sasa wa kusoma vitabu na michzkato kadhaa ya kimaisha na uchumi, utaibuka na kutuletea kitabu ama vitabu mahususi vya kutuwezesha kujikwamua kiuchumi kwa nchi yetu na nchi nyingine zilizolingana na nchi yetu katika uendeshaji wa masuala ya uchumi.

Nazungumzia uchumi ambao Tanzania ama nchi nyingine itakuwa na uchumi wa kutohitaji misaada kutimiza malengo ya bajeti zake kutoka kwa nchi "wahisani"!.

====
Nitafurahi zaidiukijibu hoja yangu hii kwa vitendo
 
Zitto hongera sana kwa kupenda kusoma vitabu, lakini ungeanza thread yako walau na salaam tu "Habari za wakati huu ndugu zangu" hakika ingependeza.
Kwa wafuatiliaji wa maandishi yake, ni nadra sana kutumia neno 'labda' ama 'nadhani'.

Wafuatiliaji wanasema ukosefu wa maneno haya unaonyesha kuna tatizo na ni kiashiria cha kujiamini kupitiliza kiasi kuwa hakosei, kujisikia, ujeuri, ubora kuliko wengine na kadhalika.

Binafsi bado natilia shaka maoni ya wafuatiliaji hawa.
 
Mwaka 2020 nimejaaliwa kusoma vitabu 16 (2019:34, 2018:49), ni Orodha ndogo sana kulinganisha na miaka ya nyuma. Hii ni kwa sababu shughuli nazo zimekuwa nyingi, ikizingatiwa kuwa ulikuwa Mwaka wa Uchaguzi Mkuu. Muda mrefu tumeutumia barabarani, Vijijini na Mitaani kuzungumza na wananchi. Pia kusoma Taarifa fupi fupi za tafiti za Uchaguzi na pia kuweza kuzalisha Ilani ya Uchaguzi ya Chama ambayo Mwaka huu kwa msaada mkubwa wa Kamati za Ilani tulikuwa na Ilani bora sana kote Jamhuri ya Muungano na Zanzibar.

Vile vile nimesoma ripoti nyingi za Serikali, mashirika ya kimataifa kama Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, IMF na majarida yenye maarifa mengi, Mfano Foreign Affairs ambalo hutoka mara 6 kwa Mwaka. Hata hivyo nashukuru sana nimejikongoja mpaka kufikia vitabu 16.

Mwaka 2020 kilichapishwa Kitabu ambacho kina Sura ambayo nimeandika. Kitabu hicho ni THE NEW SYSTEMS READER: Alternatives to a Failed Economy, Edited by James Gustave Speth na Kathleen Courrier. Sura niliyoandika inazungumzia Ujamaa baada ya Miaka 50 ya Azimio la Arusha (The Arusha Declaration: The Case for Democratic Socialism 50 years on).

Mwaka 2021 nitafanya jitihada kubwa kuandika kitabu kinachosimulia haswa Maisha yangu katika Siasa za Tanzania Katika miaka 15 iliyopita. Ni matamanio yangu kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2022 Kitabu kitakuwa dukani. Mungu atupe uhai, In Sha Allah.

Vitabu vya 2020

Riwaya

Mwaka 2020 nimesoma riwaya 6 tofauti tofauti, za watunzi wa Tanzania na Nje ya Tanzania. 50% ya riwaya hizo zimeandikwa na Watanzania sio tu wanaochipukia Lakini wanaoimarika sana katika uandishi. Naona fahari sana kuwa talanta ya uandishi wa riwaya za kusisimua bado ipo nchini, licha ya mazingira magumu ya Kazi za uandishi. Riwaya nilizosoma Mwaka huu ni Pamoja na;

1. An Orchestra of Minorities: Chigozie Obioma

2. Borderlines: Michela Wrong

3. Beneath Lion’s Gaze: Maaza Mengiste

4. Rafu: Fadhy Mtanga

5. Fumbo: Maundu Mwingizi

6. Tuzo: Fadhy Mtanga, Lilian Mbaga, Maundu Mwingizi, Laura Pettie na Hussein Tuwa

Wasifu (Biographies and Autobiographies)

Mwaka 2019 tulibahatika kupata vitabu vya baadhi ya Viongozi wetu nchini. Rais wa Awamu ya Tatu Marehemu Mzee Benjamin Mkapa aliandika Wasifu wake. Kabla ya hapo Marehemu Mzee Njelu Kasaka, aliyekuwa Mbunge na Katibu wa Kundi la G55 lililotaka Serikali ya Tanganyika alitoa kitabu chake pia.

Mwaka 2020 Wanazuoni waandamizi Prof. Issa GulamHussein Shivji, Prof. Saida Yahya Othman na Dkt. Ng’wanza Kamata walikamilisha Juzuu 3 za Maisha ya Mwalimu Julius K Nyerere, Baba wa Taifa la Tanzania. Juzuu ya 4 ipo njiani. Kazi kubwa na ya kuthaminiwa sana ambayo Wanazuoni wetu wamefanya. Kitabu hiki chenye Juzuu 3 (kimsingi ni vitabu 3 vinavyoweza kusimama vyenyewe) kilitoka wakati muafaka sana kwa kizazi chetu. Sio tu ni kitabu cha kusoma na kumaliza bali ni Kitabu rejea kwa Miaka mingi ijayo.

Mwaka huu pia Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Steven Bwana alichapisha kitabu cha Maisha yake. Kitabu hiki kinasimulia Maisha ya Jaji Bwana kuanzia Kijijini kwao mpaka ustaafu na maono yake kuhusu Tawi la utoaji haki (judiciary) katika Ujenzi wa Taifa. Mwaka 2020 umemalizika kwa kazi iliyosubiriwa kwa hamu kubwa ya Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama. Kitabu kizuri Sana kuhusu Mweusi huyu wa kwanza kuwa Rais wa Taifa kubwa duniani.

Wasifu niliosoma Mwaka huu ni Pamoja na;

7. Julius Nyerere, A Biography: Saida Y Othman, Ng’wanza Kamata na Issa G Shivji

8. Maisha Yangu, Utumishi Wangu: Steven J Bwana

9. A promised Land: Barack Obama

Nilisoma pia Mchanganyiko wa vitabu mbalimbali kama kawaida. Ni katika kuongeza maarifa na kuendelea kujifunza kutoka sehemu mbalimbali za Dunia. Pia katika kujifunza makosa ya wengine ili kutorudia makossa hayo. Vitabu mchanganyiko mwaka huu ni pamoja na;

Vitabu Mchanganyiko

10. Asia aspirations, Why and How Africa Should Emulate Asia -- and What It Should Avoid: Greg Mills, O Obasanjo Et al

11. The Naked Diplomat, understanding Power and Politics in the Digital Age: Tom Fletcher

12. Taxing Africa, Coercion, Reforms and Development: Mick Moore, et al

13. Homo Deus, A brief history of tomorrow: Yuval Noah Harari

14. The Promise of Canada, People and Ideas that have shaped our country: Charlotte Gray

15. How to lose a Country, The Seven Steps from Democracy to Dictatorship: Ece Temelkuran

16. The Room Where it Happened, A White House Memoir: John Bolton

Mwaka 2020 ulikuwa mwaka wenye changamoto nyingi sana zitokanazo na janga la COVID 19 (Korona) mpaka Uchaguzi mbovu kabisa kupata kutokea katika historia ya Tanzania. Hakika hapakuwa na Uchaguzi kwa maana ya Uchaguzi bali operesheni Maalumu ya kusaga saga demokrasia ya Vyama vingi Nchini. Kwangu Binafsi namshukuru Mungu kwa kunisuru na ajali niliyopata Oktoba 7, 2020. Ilikuwa miujiza. Mungu mkubwa Sana.

Nawatakia kheri katika kumaliza mwaka 2020 na kila la kheri katika mwaka 2021. Nawashawishi kupata muda wa kujisomea japo kitabu kimoja kila mwezi. Kusoma ni kurutubisha ubongo. Tunaoweza kuandika pia tuandike.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Dar es Salaam
Disemba 26, 2020

View attachment 1659446View attachment 1659447View attachment 1659448View attachment 1659449View attachment 1659450View attachment 1659451View attachment 1659453View attachment 1659454View attachment 1659455View attachment 1659456
Mbona hivi vitabu vyote vimetungwa na mabeberu?? Halafu utaniambia vitakuwa na mtazamo mzuriii kwa Africa ?. Kwanii hamsomi vya watunzi wa kiafrica??
 
Back
Top Bottom