Baadhi ya tabia za mama mjamzito zinaweza kuhamia kwa mume wake?

Bob12

JF-Expert Member
Feb 27, 2017
11,422
58,788
Habari za muda huu wakuu,

Hivi karibuni hapa mtaani kwetu kuna jamaa huwa namuona mara kwa mara akila michele na maembe mabichi,baada ya kuuliza wadau wakanambia mke wake ana mimba so kamuambukiza hivo vijitabia,nilibaki nikistaajabu.

Je ni kwel inatokea mume kuambukizwa na mke wake hizo tabia?
 
ni kweli,mie pia nimewahi kuzishuhudia hizo tabia kwa baadhi ya watu wangu wa karibu
 
Hii inaweza tokea richa ya kuwa ni nadra sana kutokea

Inakuwaje?
Mwanamke anachachu (hormones) ambazo ndo zinazofanya maintaining ya ujauzito ambazo ni oestrogen na progesterone wakati mwanaume anahormone iitwayo testosterone lkn ktk utengenezwaji wake ni lazm ipitie stage ya oestrogen ndipo ifikie kuwa testesterone

Kama wanyama wengine walivo mwanaume huvutwa na hormone hiz kwa nia ya ashiki hii tutokana na kuvuta harufu na wakati dushe likivinjari.
Kwa hiyo oestrogen inaweza kuwa nyingi kiasi kwamba kuibadirisha kuwa testosterone inakuwa kiwango cha chini hivo mwanaume ataanza kubehave tabia za kike kbs

Kutokana na mwanamke mjamzito kuwa juu sana hiz hormone kulinganisha na asiyemjamzito, mwanaume huweza kuzivuta kwa njia ya hewa na wakat dushe likikamua na kama convention ya kuwa testosterone iko chini mwanaume huathirika na tabia za kike
 

Hapo umeeleweka mkuu
 
mke wangu alipokuwa mjamzito aliniambukiza tabia ya kupenda maembe mabichi, kila nikitoka kazini anapiga simu niyapitie sokoni na nikifika nyumbani ananilazimisha kula, na unajua tabia za mjamzito ukikataa tu anasusa
 
Inatokea sana,mie nikiwa na mimba mume wangu anachagua sana vyakula,hali chakula bila ndimu embe,au kutapika ndio hua mpaka namuonea huruma ila hua nampenda ajabu sitaki hata aende kazini,nataka 24/7 awe karibu yangu hua chakula lunch nampa driver ampeleke kazini lakini nikiwa na mimba naenda mwenyewe mpaka kumlisha namlisha yani sijui namuonaje..lol
 
mke wangu alipokuwa mjamzito aliniambukiza tabia ya kupenda maembe mabichi, kila nikitoka kazini anapiga simu niyapitie sokoni na nikifika nyumbani ananilazimisha kula, na unajua tabia za mjamzito ukikataa tu anasusa
Duh,hongera sana mana research inaonesha ni mpaka uwe karibu nae sana,na hiyo mimba ilikupenda
 
Wewe......
 
Hormone kwa njia ya hewa ... Duuuh hii itakuwa tecnolojia mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…