Baadhi ya Taasisi za Serikali zimekaa kiupigaji zaidi badala ya kutoa huduma bora kwa wananchi

Pantosha

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
538
813
Kwanza nianze kwa kukiri kwamba watanzania ni watu wanaojituma sana kuhakikisha mkono unaenda kinywani na kujipatia maendeleo.

Ila inasikitisha kuwa jitihada za watanzania wengi zinazimishwa na watu wachache wanaoanzisha taasisi au mifuko kwa lengo la kujineemesha kwa kutumia pesa za wananchi.

Serikali imeanzisha taasisi nyingi ili kuwahudumia wananchi wake ipasavyo ila kwa bahati kuna baadhi ya taasisi kwa maoni yangu imekaa kiupigaji zaidi badala ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

Baadhi ya taasisi ni pamoja na NHIF na NSSF.

NHIF: Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
Lengo: Kuhakikisha upatikanaji bora wa huduma za afya kwa wanachama wake.

Kinachotokea Mtaani:
  • Hospitali, zahanati na vituo vya afya binafsi vingi havipokei kadi ya NHIF.
  • Bima inashindwa ku cover dawa nzuri, badala yake wametoa muongozo wa dawa za hali ya chini kwa ubora. Nimeambiwa mara nyingi tu hospitalini kuwa kwa ugonjwa huu, dawa sahihi ni hii ila bima yako hailipii hizi dawa. Afu ungonjwa wenyewe ni kama malaria, UTI, typhoid 😅
  • Bima hazilipii upasuaji labda kama ni kukata kucha au kufunga bandage kidonda.
Nini kifanyike?
 
Siajua nia ya NHIf ni nini!! Imagine kwenye hospitali ya ngazi ya wilaya gharama za kumuona daktari ilikuwa 10,000 kwa sasa wameshusha mpaka 7000. Dawa zimeshushwa gharama kwa asimia 50. Hospital binafsi lazime zife kifo cha mende. Hospitali za serikali hazina shida maana mishahara inatoka hazina kuu.
 
Siajua nia ya NHIf ni nini!! Imagine kwenye hospitali ya ngazi ya wilaya gharama za kumuona daktari ilikuwa 10,000 kwa sasa wameshusha mpaka 7000. Dawa zimeshushwa gharama kwa asimia 50!! Hospital binafsi lazime zife kifo cha mende. Hospitali za serikali hazina shida maana mishahara inatoka hazina kuu.
Hawa jamaa wanachokifanya ni kukusanya pesa za watanzania tu. Wanakozipeleka wanajua wenyewe. Mtu mweusi ni hatari kwa afya yako.
 
TUZINGATIE:

1: Ukitaka kumtafuta nyoka, anza kumlika miguuni, tujisahihishe wenyewe kwenye sekta husika kabla ya kurukia wengine.

2: Ukianguka, angalia ulipoanzia kuteleza na si ulipoangukia. Utakipata chanzo cha anguko au kuteleza kwako.

3: Kiburi si uungwana, utakuja kukumbuka shuka kumekucha. Kutakuwa hakuna umuhimu kwa kadri ilivyotarajiwa na kuhitajika utakapogutuka usingizini.

4: Asiesikia la mkuu huvunjika guu.
Madhira huwa makubwa kwa kadri tunavyotanguliza kiburi chetu cha ubinadamu. Tutaathirika wengi. Hii ni kwa kuiumiza sekta ya afya kwa ujumla na kuirudisha nyuma.

Mengine yote ni mbwembwe tu zisizo na mwendelezo wa kudumu(si suluhisho) na zitakazoenda kuumiza mtanzania wa kawaida(mwekezaji binafsi vs mhudumiwaji(mgonjwa na asiye mgonjwa vs mfanyakazi sekta ya afya hasa private).

Yote haya yanaletwa na hulka ya U-mimi na kutokujali maslahi ya watu wa kawaida na Taifa kwa ujumla.

Muda ni mwalimu mzuri.
 
Back
Top Bottom