Baadhi ya maneno katika saikolojia

Translator

JF-Expert Member
May 19, 2017
286
297
Kila fani ina msamiati wake (jargon).

Yafuatayo ni baadhi ya maneno yanayotumika kwenye saikolojia:

1. Fakali (faculties)
2. Haiba (personality)
3. Fadhaa (neurosis)
4. Kumbukumbu limbiko (cummulative records)
5. Majikwezo (superiority complex)
6. Matilaba (motive)
7. Mnafsi/mbinafsi (egoist)
9. Mndani (introvert)
10. Msondani (extrovert)

Kiswahili kina hazina yake ambayo haijafukuliwa bado.
Uzuri ni kuwa wapenda makinikia hawawezi kuihamishia ughaibuni.
 
Kitivo kinatumika zaidi kwenye taasisi kama vile vyuo. Lakini pia si wazo baya mkuu.
 
Daaa sikuwahi kujua kumbe matilaba ndio motive! Hili neno nililisikia mara ya kwanza kwenye wimbo wa Nasma Hamisi (R.I.P) unaitwa 'Mahaba ya dhati'. Anasema,"aja nipokea wangu mahbuba, upate sikia yangu matilaba...".
Daaa shukrani sana mkuu, nimeongeza msamiati.
 
Fakali = ni kama vyumba mbalimbali ndani ya akili ya mwanadamu vyenye kazi tofauti ---- utashi, kumbukumbu, utambuzi, ubunifu, nk Daby . Ndio maana nikakuunga mkono wazo lako kuhusu "kitivo" maana, in a way, unaweza kusema kitivo cha kumbukumbu, cha utambuzi, nk
 
Usijali mkuu. Kidogokidogo ndio mwendo wa uhakika.
 
Me simuelewagi mtu anayeitwa honi sigara maneno anayosema ni mapya kabisa na mengi sijawahi kuyasikia anatuambia ndio kiswahili hicho
 
Me simuelewagi mtu anayeitwa honi sigara maneno anayosema ni mapya kabisa na mengi sijawahi kuyasikia anatuambia ndio kiswahili hicho
Mkuu Edwin, lugha ina malaki ya maneno lakini wataalamu wanasema wewe na mimi tunatumia kwa wastani maneno kama 30,000 tu. Kwa hiyo, ni kawaida kabila kama utasikia neno jipya kila siku maishani mwako mwote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…