Baadhi ya mambo ambayo Freeman Mbowe ameshindwa kuyasimamia

Mushkov

JF-Expert Member
Feb 16, 2024
316
598
1. Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019.
Katika uchaguzi huu, Wagombea wote wa CHADEMA walienguliwa. Freeman Mbowe hakuongoza mapambano ya kufa na kupona ili kupigania haki( Mfumo ulimpa chake, akakaa kimya)

2. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Mfumo wote wa uchaguzi uliharibiwa. Freeman Mbowe hakuongoza mapambano ya kufa na kupona ili kupigania haki.(Mfumo ulimpa chake, akakaa kimya)

3. Uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.

Karibu Wagombea wote wa CHADEMA walienguliwa. Mbowe hajaongoza mapambano ya kufa na kupona ili kupigania haki.(Mfumo umempa chake, atajifanya kupiga mkwara lakini baadaye kidogo atakaa kimya)

Kiongozi wa chama anatakiwa kuwa strong na creative. Angekuwa yupo na CHADEMA kweli kweli asingekubali hayo yote.

Freeman Mbowe hawezi hata siku moja kuongoza mapambano ya kweli ya kufa na kupona kwa sababu anakula kotekote. Kwenye mfumo na kwenye chama.

Mwanamapinduzi wa kweli ni Tundu Lissu.

Huyu ndo anayeogopwa na mfumo kwa kiwango cha juu sana.
Kuthibitisha hilo ni pale ambapo:-

1. Alipigwa risasi kadhaa, lakini FAM hajawahi hata kupigwa hata Kofi moja.

2. Alipotangaza tu kuwania umwenyekiti alipata vitisho, lakini Freeman Mbowe hajawahi kupata vitisho vyovyote.

Kwa nini Mbowe hakupigwa risasi ila Lissu, na kwa nini Mbowe hajapata vitisho alipotangaza kuwania Uenyekiti ila Lissu . Ni kwa sababu Mbowe yupo ndani ya mfumo.
 
Kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji kuna maeneo ambayo cdm waliweka watu wa hovyo sana wagombee
Kwa sasa chama kimepoteza dira na mvuto kimekuwa cha walamba asali
 
Lete mchango wako kwenye hayo MAPAMBANO......

NO REFORM NO ELECTION
FAM ni bingwa wa maneno, si matendo. Hiyo NO REFORM NO ELECTION anaisema tu saa hizi ili kuwaaminisha wanachama, lakini nimjuavyo mimi FAM, hiyo ndo imekwisha hivyo. Hajawahi kusimamia agenda mwanzo mpaka mwisho. Ni bingwa wa kuanzisha agenda na kuiacha hewani.
 
Haya Mkuu jirushe Nungwi sisi mpaka dakika ya MWISHO
 
1. Alipigwa risasi kadhaa, lakini FAM hajawahi hata kupigwa hata Kofi moja.
Mwaka 2020 alivunjwa mguu au mmeshasahau ?
1000017651.jpg
 
Kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji kuna maeneo ambayo cdm waliweka watu wa hovyo sana wagombee
Kwa sasa chama kimepoteza dira na mvuto kimekuwa cha walamba asali
Kwa nini wanaenguliwa??
 
Mwaka 2020 alivunjwa mguu au mmeshasahau ?
View attachment 3182807
Lakini ndugu, kuvunjwa mguu na kupigwa risasi 16 mwilini( siyo mguuni) unaweza kulinganisha?
Lakini pia nimesema, TAL alipotangaza tu nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti tayari ameshapata vitisho isipokuwa FAM hajapata vitisho vyovyote.
Nani amemtisha TAL baada tu ya kutangaza nia ya kugombea? Nani huyo?
 
Ulisema hajawahi kupigwa hata kofi moja, mimi nilikuwa naweka rekodi sawa tu.
 
Ulisema hajawahi kupigwa hata kofi moja, mimi nilikuwa naweka rekodi sawa tu.
Sawa, sikuwa na maana kwamba hajawahi kupata shida hata kidogo. Nilimaanisha ukubwa wa shida aliyopata TAL kwa ajili ya siasa ndo inayotafsiri kwamba TAL ndo mwanamapinduzi wa kweli kabisa kuliko FAM.
 
Ilitakiwa tushtuke tokea alipoaihirisha maandamano ya UKUTA ghafla watu wakiwa kwenye ari ya kuandamana.

Ndio maana mfumo unapendelea yeye aendelee kubaki kama Mwenyekiti maana akiingia Lissu CDM itakuwa chama cha upinzani kamili.
 
Achaneni na sacoss ya wenyewe. Alowadanganya kuwa walikuwa kwa maslahi ya watanzania ni nani?
 
Ilitakiwa tushtuke tokea alipoaihirisha maandamano ya UKUTA ghafla watu wakiwa kwenye ari ya kuandamana.

Ndio maana mfumo unapendelea yeye aendelee kubaki kama Mwenyekiti maana akiingia Lissu CDM itakuwa chama cha upinzani kamili.
Lissu ni king'ang'anizi. Hawezi kuanzisha jambo likaishia hewani. Lissu ni ama ZANGU ama ZAKE mpaka kieleweke.
 
Lissu ni king'ang'anizi. Hawezi kuanzisha jambo likaishia hewani. Lissu ni ama ZANGU ama ZAKE mpaka kieleweke.
Wanamjua vyema, ndio maana walipoona hawawezi kukabiliana naye walitaka kumpoteza mazima.
 
Back
Top Bottom