Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,500
- 3,698
TAARIFA KWA UMMA
Kufuatia Utenguzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania uliofanywa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 23 Julai, 2024, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Jerry William Silaa (Mb) kwa mamlaka aliyonayo amevunja Bodi ya Mawasiliano Tanzania kuanzia tarehe 02 Agosti 2024.
Kufuatia Utenguzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) uliofanywa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 23 Julai, 2024, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Jerry William Silaa (Mb) kwa mamlaka aliyonayo amevunja Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kuanzia tarehe 02 Agosti 2024.
Kufuatia Utenguzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta (TPC) uliofanywa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 23 Julai, 2024, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Jerry William Silaa (Mb) kwa mamlaka aliyonayo amevunja Bodi ya Shirika la Posta kuanzia tarehe 02 Agosti 2024.
Utenguzi: Maharage Chande wa Posta, Ulanga wa TTCL na Justina Mashiba wa UCSAF watumbuliwa
Safi sana fagio linaendelea kupita👇👇 --- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi waliotenguliwa ni kama ifuatavyo:- i. B.i...
www.jamiiforums.com