Baada ya siku 100: Tunapoachana kwenye Mataa na Rais Samia

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
31,635
41,670
Mama Samia huko uliko pokea salamu hizi.

Katika siku 100 zako za mwanzo ulianza vizuri ukitupa matumaini mapya nasi tukakupongeza. Lakini baada ya hizo kupita ghafla umetubadilikia.

Ama kwa hakika unayoyafanya sasa si mageni hapa duniani na huu wimbo unakuhusu:

"Neema alimwambia Chidumule yule bwana aliyezaa naye kaja. Hivyo asifike nyumbani kwake wala kazini asimfuate. Hata akimwona njiani asimsalimie."

Tuna habari kuwa wenzetu serikalini kwa gharama zetu, nyie na jamaa zenu tayari mmeshapata chanjo tena ile adimu kabisa ya Pfizer kwa gharama zetu.

Kwa kuchanjwa kwenu sasa Corona ni suala la historia. Kwani hata mkiambukizwa, kwamba mtahitaji hata kufika hospitali tu, uwezekano huo ni mdogo sana. Corona haiwahusu tena na kimsingi sasa kwenu Corona haipo.

Bila shaka mliyezaa naye sasa yupo. Kama ilivyo kuwa kwa Neema hamtuhitaji tena. Kwa vitendo na hata kwa maneno mmeonyesha hivyo:

1. Mmetuongezea mzigo wa gharama za maisha kwa kuongeza kodi za mafuta ya magari.
2. Mmetuletea tozo mpya kwenye miamala ya simu:

IMG_20210715_213635_704.jpg

3. Vigogo nyie kulipa kodi tu hakuwahusu.
4. Kuna wabunge 19 kinyume cha katiba mzigo wa malipo yao mmeuweka kwetu.
5. Wizi wa pesa tunazokamuliwa kama ripoti kadhaa za CAG zinavyoonyesha umeamua kuufumbia macho.
6. Mashirika yanayozalisha hasara mnazotuvisha sisi unaendelea kuyakumbatia.
7. Wenzetu mnaendelea kupeana takrima za magari na majumba ya mabilioni ya pesa kwa gharama zetu.
8. Waraka huu sasa unatuhusu sisi, bila shaka mnapopanga kutuokotezea chanjo kanjanja zisizowahusu nyie:

IMG_20210717_105102_441.jpg

9. Ninyi mnapotumbua kwa gharama zetu:

IMG_20210716_183804_119.jpg

10. Sisi ni mwendo wa kugumia:

IMG_20210716_183826_638.jpg

Kwani uzalishaji unaongezeka au umeongezeka? Vipi basi hata mkaongeze kodi na tozo mpya mpya kama kuna janga linalotuhusu sote, achilia mbali kutokudhibiti matumizi ya vilivyopo?

Tumekuelewa mama yetu. Yule bwana yupo. Hata njiani tukikuona hatutakusalimia.
 
Magufuli naye mlituambia alishachanjwa chanjo ya China ndio maana akawa haogopi corona hivyo alikuwa anatutoa kafara wananchi, ila alipofariki ni nyie tena mnatuambia kafa na corona.

Mama alikuwa anaoneka anajali ana upendo na anatumia njia za kisayansi kukabiliana na corona ila sasa anaoneka mbinafsi hajali tena wananchi et kachanja chanjo kisirisiri hivyo hajali tena wananchi wake kuhusu corona.
 
Kulalamika ni sifa ambayo watanzania tuna kila sababu ya kuweika kwenye CV ya kuombea kazi. Hakuna kiongozi mwenye kuweza kumridhisha kila mtu kwa kufanya kila kitu.

Naamini awamu ya sita yenye kuongozwa na Mama inatamani sana shida zote tulizonazo ziondolewe maishani mwetu, kutamani ni kitu kimoja kuweza kuifanya tamaa hiyo ikatimia ni kitu kingine tofauti kabisa.
 
Hata iwapo hayo hayatatimia watuondolee uhuni hui wanaofanyowa wa tanzania, kwa baadhi ya kikundi cha watu kuona ndio wamiliki wa Tanzania, Katiba mpya kwanza mengine baadae.
 
Ipo tofauti baina ya kulalamika na kuyaeleza ya moyoni.

Kuna Corona imekamata. Kwa uchumi upi kuhalalisha kodi zaidi na tozo zaidi au haya?

IMG_20210716_182538_628.jpg

Mkuu unatokea kanda ipi? Kiswahili kilizaliwa Pwani.

Au wewe ni mnufaika baina ya wasiolipa kodi?
 
Ipo tofauti baina ya kulalamika na kuyaeleza ya moyoni.

Kuna Corona imekamata. Kwa uchumi upi kuhalalisha kodi zaidi na tozo zaidi au haya?

View attachment 1856822

Mkuu unatokea kanda ipi? Kiswahili kilizaliwa Pwani.

Au wewe ni mnufaika baina ya wasiolopa kodi?
Mkuu maadam moyo wako bado unapumua jifunze kukubaliana na hali halisi. Kodi ndio zimeshapitishwa na bunge kama sehemu ya bajeti ili kuzisitisha ni mpaka bunge lijalo likae.

Hakuna maendeleo yasiyo na gharama zake. Hao ambao wamekuwa wakijazilizia bajeti zetu kwa miaka mingi tangu tupate uhuru ni watu wanaofahamu maana ya kubana matumizi.

Huwezi kutaka uishi vizuri halafu wakati huo huo ukataka upate bure bure tu, lazima kuumia kukuhusu ili maisha yaboreshwe.
 
Hata iwapo hayo hayatatimia watuondolee uhuni hui wanaofanyowa wa tanzania, kwa baadhi ya kikundi cha watu kuona ndio wamiliki wa Tanzania, Katiba mpya kwanza mengine baadae.

Katiba iliyopo ndiyo msingi wa matatizo yote haya kwetu na manufaa kwao. Usisahau matatizo haya kwao ni manufaa.

Hawawezi kutuondolea Uhuni huu wao. Waondoe vipi wakati wao ni wanufaika?

Hawa ni wa kuvaa head on. Hiyo ndiyo lugha pekee wanayoweza kuielewa. Lugha za kuwaomba zibakie huko makanisani na misikitini.
 
Mama Samia huko uliko pokea salamu hizi.

Katika siku 100 zako za mwanzo ulianza vizuri ukitupa matumaini mapya nasi tukakupongeza. Lakini baada ya hizo kupita ghafla umetubadilikia.

Ama kwa hakika unayoyafanya sasa si mageni hapa duniani na huu wimbo unakuhusu:

"Neema alimwambia Chidumule yule bwana aliyezaa naye kaja. Hivyo asifike nyumbani kwake wala kazini asimfuate. Wala akimwona njiani asimsalimie."

Tuna habari kuwa wenzetu serikalini kwa gharama zetu, nyie na jamaa zenu tayari mmeshapata chanjo tena ile adimu kabisa ya Pfizer kwa gharama zetu.

Kwa kuchanjwa kwenu sasa Corona ni suala la historia. Kwani hata mkiambukizwa, kwamba mtahitaji hata kufika hospitali tu, uwezekano huo ni mdogo sana. Corona haiwahusu tena na kimsingi sasa kwenu Corona haipo.

Bila shaka mliyezaa naye sasa yupo. Kama ilivyo kuwa kwa Neema hamtuhitaji tena. Kwa vitendo na hata kwa maneno mmeonyesha hivyo:

1. Mmetuongezea mzigo wa gharama za maisha kwa kuongeza kodi za mafuta ya magari.
2. Mmetuletea tozo mpya kwenye miamala ya simu:

3. Vigogo nyie kulipa kodi tu hakuwahusu.
4. Kuna wabunge 19 kinyume cha katiba mzigo wa malipo yao mmeuweka kwetu.
5. Wizi wa pesa tunazokamuliwa kama ripoti kadhaa za CAG zinavyoonyesha umeamua kuufumbia macho.
6. Mashirika yanayozalisha hasara mnazotuvisha sisi unaendelea kuyakumbatia.
7. Wenzetu mnaendelea kupeana takrima za magari na majumba ya mabilioni ya pesa kwa gharama zetu.
8. Waraka huu sasa unatuhusu sisi, bila shaka mnapopanga kutuokotezea chanjo kanjanja zisizowahusu nyie:

9. Ninyi mnapotumbua kwa gharama zetu:

10. Sisi ni mwendo wa kugumia:

Kwani uzalishaji unaongezeka au umeongezeka? Vipi basi hata mkaongeze kodi na tozo mpya mpya kama kuna janga linalotuhusu sote, achilia mbali kutokudhibiti matumizi ya vilivyopo?

Tumekuelewa mama yetu. Yule bwana yupo. Hata njiani tukikuona hatutakusalimia.

1626513738303.png
 
Katiba iliyopo ndiyo msingi wa matatizo yote haya kwetu na manufaa kwao. Usisahau matatizo haya kwao ni manufaa.

Hawawezi kutuondolea Uhuni huu wao. Waondoe vipi wakati wao ni wanufaika?

Hawa ni wa kuvaa head on. Hiyo ndiyo lugha pekee wanayoweza kuielewa. Lugha za kuwaomba zibakie huko makanisani na misikitini.
Wasisubiri msemo ule wa kizaramo ukafanya kazi,"mwana kulitafuta mwana kulipata"
 
Mkuu maadam moyo wako bado unapumua jifunze kukubaliana na hali halisi. Kodi ndio zimeshapitishwa na bunge kama sehemu ya bajeti ili kuzisitisha ni mpaka bunge lijalo likae.

Hakuna maendeleo yasiyo na gharama zake. Hao ambao wamekuwa wakijazilizia bajeti zetu kwa miaka mingi tangu tupate uhuru ni watu wanaofahamu maana ya kubana matumizi.

Huwezi kutaka uishi vizuri halafu wakati huo huo ukataka upate bure bure tu, lazima kuumia kukuhusu ili maisha yaboreshwe.

1. Vigogo kutolipa kodi kunanifanya vipi kuishi vizuri?
2. Kodi niliyolipa kutumbuliwa kwa takrima za magari na majumba kwa vigogo zinanifanya miye vipi kuishi vizuri?
3. Kodi ninayolipa kutumbuliwa bungeni wakiwamo wabunge batili inaninufaisha vipi?
4. Ufisadi mkubwa unaokumbatiwa serikalini kwa mujibu wa CAG unaninufaisha vipi?
5. Hasara za makampuni ya serikali zinaninufaisha vipi?
6. Nk nk.

Nisiseme ninapoona mambo hayako sawa eti kuwa wewe utaona nina CV ya kulalamika?

Nadhani nitakuwa nimekutendea haki nikikutambua una CV ya uchawa uliopitiliza. Yaani mwendo wa kusifia tu hata unapodhulumiwa mchana kweupe.

Hii lakini, kama wewe si mnufaika wa moja kwa wa janja janja hizi za kina Madelu.
 
Samia kaenda na ule msemo wa wema usizidi uwezo, mwanzo alifanya ili kurudisha imani kidogo kwake toka kwa wapinzani, na kweli wapinzani wakaingia kingi wakaanza kumsifia anaupiga mwingi.

Ila alipoona inatosha sasa ameamua kuanza kukaba tena, anajua akiwaachia moja kwa moja mtasababisha nguvu zake na chama chake zipotee na kuufufua upya upinzani.
 
Sasa kurudia njia mbaya tuliyokuwa tukiifuata na kutambua kuwa ilikuwa njia mbaya,je kwa hiyari tutairejea?
 
1. Vigogo kutolipa kodi kunanifanya vipi kuishi vizuri?
2. Kodi niliyolipa kutumbuliwa kwa takrima za magari na majumba kwa vigogo zinanifanya miye vipi kuishi vizuri?
3. Kodi ninayolipa kutumbuliwa bungeni wakiwamo wabunge batili inaninufaisha vipi?
4. Ufisadi mkubwa unaokumbatiwa serikalini kwa mujibu wa CAG unaninufaisha vipi?
5. Hasara za makampuni ya serikali zinaninufaisha vipi?
6. Nk nk.

Nisiseme ninapoona mambo hayako sawa eti kuwa wewe utaona nina CV ya kulalamika?

Nadhani nitakuwa nimekutendea haki nikikutambua una CV ya uchawa uliopitiliza. Yaani mwendo wa kusifia tu hata unapodhulumiwa mchana kweupe.

Hii lakini, kama wewe si mnufaika wa moja kwa wa janja janja hizi za kina Madelu.
Kulalamika kila kukicha hakuongezi tija serikalini.

Mengi uliyoandika ni hisia tu, unao ushahidi kwamba wewe na mimi tusipolipa kodi bado serikali itashindwa kununua magari yanayotumiwa na viongozi wa serikali?.

Tatizo letu ni kujipatia haki mpaka kupitiliza, kwamba mimi na wewe tusipolipa kodi basi wale wabunge maisha yao hayataendelea kuwa kama yalivyo!. Naielewa concern yako kama mlipa kodi lakini maisha yanaendelea pasipo mimi na wewe kuwa sehemu ya walipa kodi.

Ufisadi upo tangu enzi za Yesu na Mohamed, sio jambo la kumalizika leo eti kwa mimi na wewe kuwa na uhuru wa kuhoji. Hasara za makampuni zipo dunia nzima, zipo kwenye mataifa yote.

Kodi hazikwepeki hata kama mimi na wewe tunaweza kuwa na mchango mdogo sana katika kuzilipa. Mataifa yote duniani hayawezi kujiendesha pasipo ukusanyaji wa kodi. Huo ndio ukweli na siku zote huwa unauma ukiutafakari kwa kina.
 
Nadhani ni vizuri pia ukawaacha watu walalamike! Inawezekana hii ndiyo dawa pekee inayo wasaidia kuendelea kuwa kondoo mpaka leo!

Ukitaka kulazimisha wafiche malalamiko na manung'uniko yao, kwenye mioyo yao, utawasababisha wageuke kutoka kuwa makondoo chini ya huu utawala dhalimu wa ccm miaka nenda, na kuwa wanyama wakali! Na siku ya kutokea hivyo, basi hayo Ma V8 yote yataishia tu kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali.
 
Nadhani ni vizuri pia ukawaacha watu walalamike! Inawezekana hii ndiyo dawa pekee inayo wasaidia kuendelea kuwa kondoo mpaka leo!

Ukitaka kulazimisha wafiche malalamiko na manung'uniko yao, kwenye mioyo yao, utawasababisha wageuke kutoka kuwa makondoo chini ya utawala dhalimu wa ccm miaka nenda, na kuwa wanyama wakali! Na siku ya kutokea hivyo, basi hayo Ma V8 yote yataishia tu kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali.
Uzuri mmoja ni kuwa nchi hii ina msingi wa maelewano tofauti na baadhi ya mataifa ya afrika.

Mtanzania ni muelewa siku zote hata akilalamika siku au wiki nzima.

Naamini awamu ya sita haina nia mbaya.
 
Back
Top Bottom