Baada ya punguzo la kodi, Magufuli sasa kufanyia kazi ongezeko la mishahara

blogmaster

Senior Member
Aug 15, 2015
167
74

Katika kuadhimisha siku ya wafanyakazi, Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametangaza kupunguzwa kwa kodi ya mapato PAYE kutoka asilimia 11% hadi asilimia 9% huku hiyo ikimaanisha kuwa kila mfanyikazi atapata ongezeko la mapato yake kwa asilimia 2%.

Magufuli alitangaza kauli hiyo kufuatia ombi la wafanyikazi kupitia kwa katibu mkuu bwana Nicholus Mgaya la kutaka wanusuriwe makali ya mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu.

Aidha Rais Magufuli alisema anatimiza ahadi aliotoa kwa wapiga kura wakati wa kampeni kuwa endapo watamchagua angefanya kila jitihada kuwapunguzia mzigo wa kodi wafanyikazi wa Tanzania.

Kuhusu ongezeko la mshahara wa chini zaidi atakaolipwa mtanzania bw Magufuli amewasihi wampe muda kidogo akomeshe rushwa na kuimarisha uchumi wa taifa kisha atatoa tangazo.

Pamoja na uamuzi huo, Rais Magufuli pia amewaahidi wafanyakazi kuwa baada ya kupunguza kodi katika mishahara ya wafanyakazi, serikali yake itafanyia kazi mapendekezo ya kuongeza mishahara

Aidha, amewataka wafanyakazi kuunga mkono juhudi za kuwafichua wanaozalisha wafanyakazi hewa, huku akibainisha kuwa mpaka kufikia jana tarehe 30 Aprili, 2016 jumla ya wafanyakazi hewa waliobainika walikuwa 10,293 ambao kwa mwezi mmoja tu wamelipwa shilingi bilioni 11.6.

Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, ikulu Dodoma Gerson Msigwa ilisema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…