GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,948
- 119,240
Naona sasa kila nikipita nawaona " yange yange " yaani askari Police wa barabarani a.k.a Matrafiki wakiwa wameshikilia zile mashine zao za EFD ambazo sasa wanazitumia katika kuwalipisha Madereva mbalimbali wenye makosa katika Vyombo vyao vya usafiri.
Binafsi nilijiaminisha kuwa sasa baada ya ujio huu wa hizi EFD machines sasa ule mtindo wa baadhi ya askari Police wa usalama barabarani ( Matrafiki ) hawachukui tena rushwa kama hapo awali kumbe naambiwa " najidanganya " na Kazi ipo pale pale.
Cha kushangaza pamoja na " ujanja " na " utundu " wangu wote wa " ufukunyuku " nimejitahidi kwa hali na mali kutaka kujua kama kweli Matrafiki wetu sasa wanaendelea kuchukua " mitonyo " humu barabarani na nimeambulia patupu ila bado tu Wataalam wa mambo wanasema kuwa bado rushwa ipo na tena sasa baada ya huu ujio wa hizi EFD machines sasa Matrafiki ndiyo wanachukua rushwa " kiurahisi " mno kuliko hata Kamanda " Asiyepinga " anavyodhani.
Hivyo basi kama kuna Member yoyote humu anajua njia mpya au mtindo mpya au mfumo mpya wa uchukuaji rushwa kwa hawa Matrafiki wetu huku barabarani naomba atuwekee hapa ili nasi tuujue kwani kuna " mkoko " wangu mbovu sana tena " Lori " nataka nilivushe leo kutoka Tegeta kulipeleka gereji Mbagala Kizuiani hivyo nikiwekewa hapa hizo njia na bei za rushwa mtakuwa mmenisaidia sana ili nijipange vizuri.
Na nasikia sasa Matrafiki wana mfumo wao mpya wa uchukuaji rushwa ambao Wataalam hawa wanasema Matrafiki wa humu mijini huuita 4-4-2 na nasikia kuna mingine miwili Matrafiki wa Mabasi ya Mikoani sasa wanaiita " Mourinho " na " Guardiola " styles.
Karibuni " mtiririke " nayo kama mnaijua tafadhali.