Baada ya Kuzuiwa kufanya mikutano ya kisiasa mkoani Dodoma, CHADEMA Kwenda Mahakamani

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
KUZUIWA kufanya mikutano ya kisiasa mkoani Dodoma, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahaki, anaandika Dany Tibason.

Kutokana na hatua hiyo, Chadema kimepanga kuwafikisha mahakamani Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (RC) pamoja na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini (OCD).

Chama hicho kimetoa tamko hilo leo mkoani humo kutokana na kupigwa marufuku kuendesha mikutano ya hadhara wakati wa vikao vya Bunge.

Kauli hiyo imetolewa leo na Jella Mambo, Mwenyekiti wa Chadema, Mkoa wa Dodoma alipozungumza na waandishi wa habari kutokana na madai ya kuchoshwa na unyanyasaji unaofanywa na viongozi wa mkoa kuzuia mikitano yao ya siasa ya wapinzani.

Mambo amesema kuwa, chama hicho kimepigwa marufuku na uongozi wa Mkoa wa Dodoma kufanya mikutano ya hadhara wakati wa vikao vya bunge.

Amesema, uongozi wa Chadema mkoa unakusudia kuwapeleka watu hao mahakamani ili mahakama iweze kutafusiri sheria na kasha kubaini kama kuna sheria yoyote ya masuala ya siasa kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa vikao vya bunge.

Mbali na hilo amesema, wanataka kujua kama kuna haki ya kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa vikao vya Bunge na iweze kufafanua kama sheria inahusu Mkoa wa Dodoma tu au na mikoa mingine.

“Utamaduni wa kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa vikao vya Bunge ulianzishwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi jambo ambalo alilenga kufifisha upinzani Dodoma baada ya kuona kasi ya upinzani inapamba moto,” amesema Mambo.

Wakati wa Dk. Nchimbi, aliiandikia barua Chadema iliyokataza kuendesha mikutano ya hadhara katika kipindi cha Bunge na kwamba, inapingana na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992.

“Lengo hapa ni kukandamiza upinzani ambao unaonekana kupanda chati kila siku, hivyo wanatunyima kufanya mikutano yetu kwa visingizio vya Bunge.

“Lakini ukiangalia sheria ya vyama vya siasa inasema kuwa moja ya majukumu ya vyama vya siasa ni kufanya mikutano na mambo mengine kama hayo bila kujali kuna bunge au hakuna,” amesema Mambo.

Amesema kuwa, lengo la kwenda mahakani ni kutaka kupatiwa tafsili ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 ambayo itawasaidia kuondokana na kero hiyo ambayo imekuwa ikiletwa na watawala wa mkoa wa Dodoma ambao ni wateule wa chama cha mapinduzi.

“Huku ni kutaka kuipunguza nguvu chadema pamoja na upinzani kwa ujumla kwani wamekuwa wakitusumbua sana.

“Wengine tunapigwa na polisi lakini pia tunafunguliwa kesi zaidi ya tatu na tunashinda sasa hatutakiwi kuendelea na hali hii ndiyo maana tunataka kwenda mahakani ili kuweza kupatiwa tafsiri ya sheria hii,”amesema Mambo.

Amesema kuwa, kitendo cha Joshua Nasari Mbunge wa Arumeru mashariki kutolewa bungeni kwa kuvutwa kama mwizi alipotoa hoja ya msingi ya kutaka kujadiwa kuondolewa kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ni unyanyasaji wa kijinsia na kumkosea adabu mtu ambaye ni mwakilishi wa wananchi.
 
Hii ni njia sahihi kabisa, hata wakati wa msiba wa Kamanda Mawazo walibana mahakama ikatusaidia
 
Hela za kuendeshea kesi watatoa wapi?? Maana mkwanja wote umekatwa kwa sababu walifukuzwa bungeni. Na hao wanaosign na kutoka dawa yao inakuja
 
.....

......Katiba ya nchi inaruhusu vyama Vingi na shughuli zake ....aisehhh ELIMU ELIMU ELIMU
 
Duu.... Kumbe hadi mikutano wamepigwa ban! Sasa watafutukutia wapi hawa jamaa jamani
 
Me nlidhan wamejifunza kutoka kwenye msiba wa Mawazo, kumbe bado? Magu nae yupo tu wala hata hakemei upuuzi huo... Kweli CCM kimezeeka vbaya... Haya yetu macho na masikio.
 
KUZUIWA kufanya mikutano ya kisiasa mkoani Dodoma, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahaki, anaandika Dany Tibason.

Kutokana na hatua hiyo, Chadema kimepanga kuwafikisha mahakamani Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (RC) pamoja na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini (OCD).

Chama hicho kimetoa tamko hilo leo mkoani humo kutokana na kupigwa marufuku kuendesha mikutano ya hadhara wakati wa vikao vya Bunge.

Kauli hiyo imetolewa leo na Jella Mambo, Mwenyekiti wa Chadema, Mkoa wa Dodoma alipozungumza na waandishi wa habari kutokana na madai ya kuchoshwa na unyanyasaji unaofanywa na viongozi wa mkoa kuzuia mikitano yao ya siasa ya wapinzani.

Mambo amesema kuwa, chama hicho kimepigwa marufuku na uongozi wa Mkoa wa Dodoma kufanya mikutano ya hadhara wakati wa vikao vya bunge.

Amesema, uongozi wa Chadema mkoa unakusudia kuwapeleka watu hao mahakamani ili mahakama iweze kutafusiri sheria na kasha kubaini kama kuna sheria yoyote ya masuala ya siasa kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa vikao vya bunge.

Mbali na hilo amesema, wanataka kujua kama kuna haki ya kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa vikao vya Bunge na iweze kufafanua kama sheria inahusu Mkoa wa Dodoma tu au na mikoa mingine.

“Utamaduni wa kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa vikao vya Bunge ulianzishwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi jambo ambalo alilenga kufifisha upinzani Dodoma baada ya kuona kasi ya upinzani inapamba moto,” amesema Mambo.

Wakati wa Dk. Nchimbi, aliiandikia barua Chadema iliyokataza kuendesha mikutano ya hadhara katika kipindi cha Bunge na kwamba, inapingana na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992.

“Lengo hapa ni kukandamiza upinzani ambao unaonekana kupanda chati kila siku, hivyo wanatunyima kufanya mikutano yetu kwa visingizio vya Bunge.

“Lakini ukiangalia sheria ya vyama vya siasa inasema kuwa moja ya majukumu ya vyama vya siasa ni kufanya mikutano na mambo mengine kama hayo bila kujali kuna bunge au hakuna,” amesema Mambo.

Amesema kuwa, lengo la kwenda mahakani ni kutaka kupatiwa tafsili ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 ambayo itawasaidia kuondokana na kero hiyo ambayo imekuwa ikiletwa na watawala wa mkoa wa Dodoma ambao ni wateule wa chama cha mapinduzi.

“Huku ni kutaka kuipunguza nguvu chadema pamoja na upinzani kwa ujumla kwani wamekuwa wakitusumbua sana.

“Wengine tunapigwa na polisi lakini pia tunafunguliwa kesi zaidi ya tatu na tunashinda sasa hatutakiwi kuendelea na hali hii ndiyo maana tunataka kwenda mahakani ili kuweza kupatiwa tafsiri ya sheria hii,”amesema Mambo.

Amesema kuwa, kitendo cha Joshua Nasari Mbunge wa Arumeru mashariki kutolewa bungeni kwa kuvutwa kama mwizi alipotoa hoja ya msingi ya kutaka kujadiwa kuondolewa kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ni unyanyasaji wa kijinsia na kumkosea adabu mtu ambaye ni mwakilishi wa wananchi.

Ananichanganya eti kumtoa Nasari kwa nguvu ni unyanyasaji wa kijinsia?
 
Hela za kuendeshea kesi watatoa wapi?? Maana mkwanja wote umekatwa kwa sababu walifukuzwa bungeni. Na hao wanaosign na kutoka dawa yao inakuja

Bibie hujambo? Nikiona avatar yako huwa inanikumbusha mbali sana. Na pia ninapata viashiria kwamba hiyo avatar inakufanana hasa kwa ndani na nje. Unajua huwa ninakumbuka nini? Wakati fulani nilikuwa Tunduru nikitokea Msumbiji. Hata hivo wenzetu walituonya kabla kuhusu kulala katika kile kijiji. Kulikuwa na tatizo usiku wanasikika watu wakitoa sauti za kuomba msaada. Lakini watu wakitoka, wanakuta ni watoto wa kike wakitafuta kampani. Ki ukweli hawakuwa binadamu. Siku moja katika kutaka kuona, mimi na mwenzagu tukatoka kutaka kuona ukweli wa habari. Tulikuta mbibi mzee mmoja ambaye anasura kama hiyo avatar yako. Akiomba ffedha akijua tumetoka kule basi tuna fedha. Kumwangalia vizuri hakuwa na sehemu iitwayo magoti na kama alikuwa nayo basi yalikuwa yako sehemu ya juu sana karibu na kiuno ambako kulikuwa kumefunikwa. Kwa hiyo sehemu ya kutoka chini hadi juu sana palikuwa na miguu kama migagi. Alivaa kofia kama yako hapo. Jamaa yangu akashtuka na kuwa mkali kwa yule bibi. Kofia ikadondoka. Akabakia na uso kama wako ila kichwa cha kenge!. hadi shingoni. Nitasimulia siku nyingine kama nitapata moyo huo kwa kuw ahapa si mahala pake.

Ninahisi na wewe ni kenge kichwani na moyoni!. Sijui kama una magoti ama ni kama yule bibi,huna!. Viumbe kama wewe huwa si wakawaida.
 
Eeh! Hii nayo ni shughuli.
 
Kuna vitu vingine havistahili hata kutajwa kwenye nchi huru kama hii, mnawazuia nini wakati mlitakiwa muwalinde wakaongee na wananchi hicho wanachokitaka? Wapeni uwanja kabisa na vifaa ikibidi na hamasisheni watu waende wakasikilize, kama ni unafiki na uongo si wananchi watawacheka? Na kama mambo yote yako vizuri sasa mnaogopa nini kuwaacha wakabwabwanye huko, wapeni onyo la kutojaribu kifanya fujo na kudhuru basi.
 
Back
Top Bottom