Salaam, shalom!!
Viongozi tulikuwa tukiwaonya kupunguza viburi, mlikuwa mkitamba Kwa kauli za kejeli kuwa " Hata msipoipigia CCCM kura Bado itaunda Serekali"
Wengine wakaenda mbali na kudai kuwa " CCM kamwe haitatoka madarakani Hadi ipende yenyewe kama ambavyo
Pascal Mayalla amekuwa akidai,
Viongozi wetu mkashindwa kujua kuwa kauli zenu ni sawa na kumshika mkono kipofu wakati mnamwibia chakula chake,
Matokeo ya kauli zenu, wananchi wamestuka, wamesusa,wamepuuza wamekaa pembeni.
Sasa Kuna Ile KANUNI ya ushindi wa mazingira, kuwa, wakijitokeza wapiga kura waliojiandikisha, unaongeza na za wizi Ili ionekane chama kimeshinda Kwa HAKI,
Sasa watu hawajiandikishi, wamegoma, mtaiba kura zipi ilhali watu hawajitokezi!!
Sasa uhalali wa kuongoza utatoka wapi ikiwa wananchi wamegoma kushiriki chaguzi sababu ya wizi na viburi vyenu?
Suluhu pekee iliyobaki mbeleni ni kubadili mgombea wa nafasi ya juu kuliko zote Ili angalau Nchi ipumue, chama kiendelee kuwepo japo Kwa miaka 10 ijayo, tofauti na hapo, yajayo...
Wana chi Si wajinga, mkae mkijua Hilo.
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.
Karibuni 🙏