Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 9,321
- 14,826
Netanyahu kama alivyo mwenzake Donald Trump akili zao si za kawaida.Wanajiamini kuwachokoza na kutaka kupigana na kila mtu duniani kwa kujiamini kwa hali ya juu.
Hiyo ni kwa vile Israel kwa sasa imeridhika kuwa waarabu wote ni kama maboya tu.Sasa hivi wamejiamini kuichokonoa Uturuki ambapo hapo jana jeshi la Israel liliendelea kupiga maeneo kadhaa ya Syria hasa hasa zilizokuwa kambi za jeshi za Bashar Al Assad.Njia za kufikia kambi hizo zimebomolewa na makombora kutoka angani ili Uturuki isiweze kuzifikia na kuzitumia.
Israel inafanya hivyo huku ikijua kuwa yenyewe inachukua maeneo ya nchi hiyo na ambayo yapo chini ya makatazo ya maazimio ya Umoja wa mataifa.Imekuwa ikitoa amri kwa watawala wapya wa Syria kutopeleka vikosi vyake maeneo mengi ya kusini mpaka kusini ya mji mkuu wa nchi hiyo.
Inashangaza sana akili za Netanyahu na Trump zilivyo na ambazo zinawachokoza mataifa na kila mtu.Kile wanachopenda wakipate na wanachofanya wao huwa hawapendi wengine wavipate wala kufanya kama wanavyopenda hata kama ni haki na viko chini ya mamlaka zao.