Baada ya Kumsikiliza Feitoto na Interview yake na Clouds FM leo Kisaikolojia Feitoto hayuko mbali kutoa SIRI nzito

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
60,453
120,812
Katika hili GENTAMYCINE niko Serious na naweka Utani ( Ucharuraji ) wangu wa Usimba na Uyanga na naomba upesi sana haya yafuatayo yafanyike kwani kwa Saikolojia yangu Kali na Maono yangu Makali ya Kinabii naona tunakoelekea kuna Mtu anaweza kupotezwa mazima Kipumzi na Klabu pamoja na Ligi Kuu yetu hadi Taasisi ( TFF ) Kuchafuka vibaya mno....

1. Naomba Uongozi wa Yanga SC ( hasa Rais Injinia Hersi Said na Tajiri Gharib Said Mohammed ) wajitathmini, wajirudi na wamuite Mchezaji Feisal Salum Feitoto wayamalize.

2. Namuomba Mama Mzazi wa Mchezaji Feisal y Feitoto na Mchezaji Mwenyezi Wasamehe yote, wakae chini na Viongozi wa Yanga SC na Wamalizane kwa Amani.

3. Klabu ya Yanga SC iwapige marufuku upesi sana Msemaji wao Ali Kamwe na Mhamasishaji Wao ( sasa Mfungwa wa Soka ) kulizungumzia hili na Kumnanga Mchezaji kwani laweza Kuchochea Hasira kwa Mchezaji na akayasema Makubwa Mawili ambayo GENTAMYCINE nimeyahisi ila kwa sasa Kayaficha / Kayahifadhi.

4. Vyombo vya Habari ( Media ) viache Mara moja kuchukua upande juu ya hili Sakata na limwachie Mchezaji na Uongozi wa Yanga SC katika Kulimaliza.

5. Kama ikiwezekana Watafutwe Wazee / Watu wa Hekima ( GENTAMYCINE nikiwemo ) tuweze Kukaa na Mchezaji na Uongozi wa Yanga SC ili tulimalize kwa Afya ya Mpira Wetu Tanzania.

6. Viongozi Waandamizi wa Serikali ( walioko Madarakani na Waliostaafu ) wakae mbali na hili Sakata ili wasije Kuchafuliwa na Heshima yao Kupotea kwa Wananchi wanaowaamini na Wasiowaamini.

7. Mashabiki tusikurupuke / wasikurupuke katika Kulishadadia hili Jambo kwa Hisia Kali za Kimichezo bali tujikite zaidi katika Kusikiliza, Kuliekewa, Kulitafakari, Kulichambua kwa Kina na mwishoni tuwe ni sehemu Kuu ya Kulitatua kwa Afya ya Mpira Wetu na siyo Kuuchafua Mpira Wetu.

Najua GENTAMYCINE nasomwa na Wakubwa wengi wa Yanga na Simba, Mashabiki bila kusahau na Wadau Wengine wa Michezo ( hasa Soka la Tanzania ) hivyo naomba huu Ushauri wangu ufanyiwe Kazi upesi kwani kuna HATARI fulani ya Soka la Tanzania ( hasa Ligi Kuu yetu ya NBC ) Kuchafuka, TFF Kuchafuka na huenda hata huko mbeleni Wachunguzi wa CAF na FIFA pamoja na PCCB wakalazimika Kufanya Kazi Maalum ya kujua Ukweli wa Jambo fulani ikizingatiwa Mchezaji Feisal Salum Feitoto pia alikuwa ni Mmoja wa Manahodha wa Yanga SC hivyo piga ua yako mengi tusiyotakiwa kuyajua anayajua na si ajabu hata na Ushahidi wa baadhi anao.

Akhsanteni nitashukuru mkinielewa.

Cc: Bila bila, cocastic na SAGAI GALGANO
 
GSM na Eng wako zao Algeria wakiipambania timu kujaza vikombe na medali, hawana muda wa kijibu pumba za anayefundishwa cha kuongea.
 
Whos the https://jamii.app/JFUserGuide is femtoto,
Msitujazie ujinga hapa.
Hataki kucheza mpira avae makobazi yake na kanzu akale urojo.
Timu zipo tu daily.
Mnatuchosha hapa na mada za mpuuzi mmoja aliyeamua kuharibu future yake mwenyewe.
 
Watajua wenyewe bana. Mimi nasubiri tarehe 3/6/23 basi.
 
Hahahaha, mnajuana eeeh, waumbuke tu
 
Naunga mkono hoja yako,wayamaliza kimila tu haya mambo kila mtu ashike hamsini zake,kuna aibu naiona inakuja.
 
Ni tahira na mpuuzi ndiye anayeweza kusapoti utahira wa huyo kijana, eti hana tatizo na Yanga wala hana tatizo la maslah bali ana tatizo la manyanyaso?.

Mwanzo wa sakata hili alitoka hadharani na kusema ameomba kuborehewa maslah yanga wakakataa, alisema hawezi kurudi yanga saizi anasema anaweza kurudi endapo Hersi ataondo! Huyu kijana amekuwa mpuuzi kiasi hiki?. Anashinda na Rais?, Kwenye mkataba Jana anasema ameongezewa mwaka mmoj wakati mkatab halisi ni miaka 2? Hivi siku anasaini huu mkataba kwani yanga hawakutoka hadharani na kusema ni mkataba wa miaka 4? Alikuwa wapi kwa kipindi chote kudai kuongeza mkataba pasina makubaliano?.
Kama mkataba wake unahusisha miaka miwili na sio 3 au 4 inayosemwa anachokifanya saizi chakutaka kuvunja mkataba anavunja mkataba upi asiyoutambua?, Kwanini asipeleke malalamiko ya kuongezewa muda wa mkataba na apeleke ombi la kuvunja mkataba?. Kupitia mahojiano ya jana hakuna mtu mwenye akili timamu asiyeendeshwa na mihemko akawa upande wake hata waliokuwa wanamsapoti wameona aibu wao.

Yanga shikilia mpini tuone mwisho wa upuuzi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…