Baada ya kufanikiwa kudhibiti mishahara hewa, sasa tulitazame suala la vyeti feki

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,400
Moja la jambo alilofanikiwa Rais Magufuli na serikali yake ni kudhibiti suala la mishahara hewa. Kwa hili anahitaji pongezi za dhati..

Baada ya hilo, basi ni vyema serikali ikalitazama tena suala la vyeti feki. Naamini na ni jambo la wazi kuwa katika ofisi za serikali kuna maelfu na maelfu ya watu wanatumia vyeti feki...

Mh. Rais, mawaziri wa utumishi tilieni mkazo katika hili ili kuondoa wote wanaotumia vyeti feki.... Na vijana waliosota kusoma wapate ajira...
 
Mkuu narudia kusema hii ni Vita kubwa zaidi ya ufisadi nakuhakikishia kuna viongozi wengi wanavyo kumbuka kitabu cha mafisadi Wa elimu cha msemakweli kama wafanyakazi hewa ni elfu kumi ña wenye vyeti feki ni zaidi sitashangaa kuona familia nyingi wazazi wakiwa watashinda majumbani na watoto peke yao kuwa ndio wanaotoka asubuhi hii Vita ikifanikiwa itaongeza ajira kwa vijana waliomitaani na wana elimu mzuri tu
 
Unataka serikali ijivue nguo uanze kuicheka?

Taasisi nyingi za serikalini vyeti feki vimetamalaki na undugulization kwenye taasisi nyeti, hii ni kutokana na mfumo mbovu na dhaifu ya serikali ya chama cha kijani,
Atleast kwenye makampuni binafsi naweza kusema wako makini kidogo, lakini serikalini hell BIG NOO!

Mtoto wa kaka kaishia form 4 post human resource..."kamlete"

mjomba wako yupo form six anataka kuwa accountant......"akimaliza mlete ajishikize kwa muda"

Shemeji yangu amedisco chuo ila semisster ya kwanza alifaulu vizuri.....'Usihofu shemeji mwambie aje kwenye interview jmos hapa Ofisi ya makamu wa rais."
.
UHAKIKI WA VYETI FEKI UANZIE OFISI NYETI SERIKALINI...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…