N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,569
- 11,155
Wiki hii Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, alihutubia wajumbe wapya wa Bodi ya Chai inayoongozwa na Banker Abdulmajid Mussa Nsekela.
Katika hotuba yake, Waziri Bashe alimwelekeza mwekezaji na mfanyabiashara maarufu, Mohammed Dewji, kushirikiana na Bodi hiyo kwa lengo la kufanikisha kufufuliwa kwa viwanda vya chai vya Chivanjee na Msekela, vilivyopo katika Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
Viwanda hivi ambavyo kwa sasa vimefungwa pamoja na mashamba yake makubwa vipo chini ya Mo.
Kufufuliwa kwa viwanda hivi kunalenga kuwasaidia wakulima wadogo wa chai kuuza mazao yao, kuleta ajira mpya, pamoja na kupanua wigo wa mapato ya fedha za kigeni, huku pia kikiwa ni kichocheo cha maendeleo mengine mengi ya uwekezaji.
Vijiji vingi vya maeneo haya kwa sasa watu wake wanaolima chai wamekuwa kwenye wakati mgumu kutokana na kufungwa kwa viwanda hivyo viwili kwani walikuwa wakiuza majani mabichi ya chai kwenye viwanda hivi na vijana kwa wazee kwa mamia mengi walikuwa wakipata ajira kwenye viwanda na mashamba.
Historia inaonyesha kuwa viwanda vya Chivanjee na Msekela, pamoja na mashamba makubwa ya chai, vimekuwa nguzo muhimu ya uchumi wa Rungwe kwa muda mrefu, hasa tangu enzi za uwekezaji wa George Williamson Tanzania Tea Co. Ltd.
Viwanda hivi vimechangia pakubwa ukuaji wa miji midogo ya Ushirika, Tukuyu, Kiwira na Kyela.
Hata hivyo, kwa sasa vifungwa. Matokeo yake ni kupungua kwa ajira, kushuka kwa mapato ya wakulima na kudorora kwa uchumi wa wilaya hiyo.
Je, tutarajie kwa kauli hii ya Waziri Bashe, matumaini mapya yameanza kuchipuka miongoni mwa wakazi wa Rungwe. Je, Mo atavifufua hivi viwanda kweli? au apewe mwekezaji mwingine?.
Bashe amesema wanataka sekta ya chai Tanzania kuanzia sasa ijikite kuzalisha chai yenye ubora wa hali ya juu, hii ina maana uwekezaji unatakiwa kuja na teknolojia mpya ya kisasa ya usindikaji. Je, Mo yuko tayari kuwekeza hiyo teknolojia mpya ya kuzalisha chai ya kisasa itakayouzika duniani kwa urahisi zaidi? Je, viwanda vingine inakuwaje kuhusu eneo hili la ubora?
Wengi wanajiuliza iwapo Mohammed Enterprises wataweza kutimiza agizo hili kwa haraka na kwa ufanisi. Wananchi wanatarajia mabadiliko makubwa ikiwa viwanda hivyo vitaimarika tena, hasa kwa kuongeza bei za majani ya chai, kutoa ajira zaidi, na kufufua uchumi wa eneo lao.
PICHA: Kiwanda cha Chai cha Chivanjee
Je, agizo hili la Waziri litatekelezwa kwa vitendo, au litabakia kuwa maneno matupu?
Pia soma: Kwanini MO Dewji anataka kufunga kiwanda chake cha chai Nchini Tanzania? Bashe amgomea!
KUSAYA: KUSITISHA KAZI VIWANDA VYA CHAI SHAMBA LA TUKUYU HAKUKUBALIKI
Serikali yavibana viwanda vya chai vya Mo Dewji