B Dozen (B12) achukua nafasi ya Captain G Habash kwenye Jahazi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,819
Screenshot_2024-05-08-09-20-33-236_com.instagram.android-edit.jpg

Kituo cha Redio cha Clouds FM kimetangaza kuwa Mtangazaji wa Show ya Mchana (XXL), Hamis Mandi (B Twelve) atamrithi aliyekuwa Meneja na Mtangazaji wa Show ya Jioni ya Jahazi marehemu Gadner G. Habash aliyefariki wiki chache zilizopita.

Ikumbukwe, B 12 ni zao la Gadner kwenye utangazaji ambapo alipata nafasi kufanya kazi na Clouds wakati akiwa kidato cha 6 jijini Arusha.

Mkuu wa Maudhui wa Clouds Media Group Sebastian Maganga leo kupitia Power Breakfast ya CloudsFM ameutaja urithi wa Marehemu Gadner G. Habash kwenye kipindi chake cha Jahazi alichokua akikifanya kwa miaka mingi kabla ya kufariki mwezi April 2024.

Urithi huo ni Watangazaji wataoliendesha JAHAZI ambapo amewataja kuwa ni Mwenyeji George Bantu, Hamisi Mandi ( BDozen), Adam Mchomvu na DJ D Ommy huku Watayarishaji (Producers) wakiwa ni Musa Memba na Big Chawa.

Screenshot_2024-05-08-09-28-12-243_com.instagram.android-edit.jpg
 
Back
Top Bottom