kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,506
- 13,988
Unyanyapaa ni kosa sawa na makosa mengine, hasa likifanywa na taasisi
Wafanyakazi wa ndani ni kundi kubwa sana kwenye jamii zetu, ambao kazi zao ni muhimu sana. Kazi Yao inawaingizia kipato lakini pia inasababisha utulivu mkubwa maofisini miongoni mwa watumishi wenye watoto wadogo nyumbani kwakuwa ndio wanaoachiwa kazi zote za kulea watoto, usafi, upikaji chakula, kufanya manunuzi na hata ulinzi wa mali za mabosi wao. Watu hawa wanastahiki kuheshimiwa kama watu wengine.
Faida nyingine ya watumishi wa ndani ndio wanaotumia umeme nyumbani mchana kutwa kuangalia TV na video na kusikiliza radio nyakati za mchana (faida kwa tanesco na serikali) wakati mabosi wao wako kwenye majukumu yao ya siku.
Pia wafanyekazi hawa ni ndio wadau wakubwa wa channel ya Azam tv ya Sinema zetu, watanunua kifurushi japo Cha wiki ili waangalie Sinema zetu. Hivyo ni faida kwa Azam media.
Hoja Iko hapa: Nasikia kuwa Kuna tamthilia inayokwenda kwa jina la Beki 3 inaenda kuonyeshwa kwenye channel ya Simema zetu Azam tv. Kama ni kweli jina hili la "Beki tatu" halileti heshima kwa jamii hii ya watumishi wa ndani. Jina hili ni kejeli kwa watumishi wa ndani, hivyo sio vizuri kutumika kwenye TV kubwa kama Azam tv.
Napinga jina/title lakini sipingi mafundisho/ujumbe yaliyomo kwenye hiyo tamthilia.
Mimi nitakuwa wa kwanza kwenda mahakamani kuuliza tafsiri ya Beki tatu, na kama ni sawa hawa watu kuitwa Beki 3 na Azam tv, wasanii na wadau wengine au la!.
Heshima ni kitu Cha bure.
Nawasilisha.