Azam Tv mihemko itawapeleka shimoni

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
17,034
7,590
Jana nilishtushwa kuona mnashindwa kujua uzito wa habari, kubalansi, kutawaliwa na mihemko zaidi ya kujua umuhimu wa vipaumbele kwa watu na nchi yetu.

Hakuna namna unaweza kunishawishi nikaelewa kwamba ni bora zaidi kuongelea "personality" tena kwa dakika5 kuliko kuongelea namna nchi yetu inavyoliwa na kuibiwa tukio lililokuwa likimhusisha raisi. Kwamba kukamatwa makontena 20 yenye kuhisiwa yanatoroshwa yakibeba dhahabu si habari nzito kwenu. Kwamba Nape ni habari nzito na muhimu kwenu kuliko mali na utajiri wa nchi yetu.

Lakini pia, hivi unaanza habari gani kwa siku, ya raisi ama ya aliyefukuzwa uwaziri? Tena mlivyo wa hajabu wakati mkitoa dakika 5 na kukaribisha wazungumzaji kwa tukio la mtu, upande wa pili mnatoa dakika1 halafu mnafukia as if anayeongea ni balozi wa nyumba kumi na kilichotokea ni kama mtu kutema mate.

Yawezekana hao wanaotuibia mali zetu waliwaambia msiwaoneshe sana ili wananchi wasipige kelele dhidi yao na badala yake muonesheni fulani ili wananchi wapige kelele dhidi ya utawala. Kama na nyie mlikubali hili na mkauvaa mkenge basi anzeni kujichunguza kabla, nchi yetu inaliwa na sote tunajua ila nyie hamuoni kama la kuliwa nchi yetu ni hoja. Mnatakiwa kuelewa hao wezi hawamuibii JPM tu, hawamwibii fulani tu, wanatuibia sisi sote na tunapopoteza wakati wenzenu wanapata ni kuihujumu nchi yetu. Ni kuhujumu serikali kwa kile inachojaribu kukifanya katika maendeleo, msivimbe vichwa mkajiona tayari.
 
Ikifika mda mkaitwa kupewa honyo na makalipio msije kujiuliza wala kulaumu. Kuanza kufanya kazi kama whatsap ama mmegeuka Face book ni kuanza kupoteza "umahiri" wenu. Kwenye hiyo mitandao ya hovyo kule hakuna umahiri, weledi, hekima wala kubalansi. Kule ni kelele, na mihemko tu bila kusahau mapenzi. Kule hakuna utaifa wala taifa, ni ghiriba, udaku, udakuzi na unyambilisi.
 
Hayo maelekezo peleka TBC. Yaani unawalazimisha kuonyesha mazingaombwe bandarini?
 
Unahararisha matumizi rasmi ya "Uhuru" TBC ndo viwe vyombo vya habari za Tz ila hivi vingine viandike andike tu?
Unahararisha umuhimu wa kuviondoa vingine na badala yake kazi ya kuhabarisha umma juu ya masuala ya nchi yao ianze kufanywe na Uhuru na TBC na wengine amtaia wafungiwe ama wakachukue kutoka Uhuru na TBC?
Unamaanisha ile sheria ya kuvibana vingine ilikuwa sawa kwasababu hawako kitaifa zaidi?
 
Hv tbc wanafanya kazi gani!? Si ndo tv ya serikali hyo ilitakiwa iwe na coverage ya kutosha...punguza munkari..kunywa maji..usiingilie kazi za watu
 
Mimi napenda habari kweli ila sio zile za kutengeneza, kwanza kuna watu wananikwaza sana nikimuona tu sura yake kwenye TV ndiyo kwanza naaza kuumwa na kichwa!! Nafikiri Azamu ameliona hilo... Afadhali kuangalia katuni kuliko story za kutengeneza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…