Awamu ya Tano yafanya makubwa kwa kipindi kifupi

JOYOPAPASI

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
250
409
UKWELI AMBAO WANANCHI WENGI WANAUTAMBUA CHINI YA SERIKALI YA AWAMU YA 5.

Katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tano wananchi wameweza kuyaona mambo ambayo awakuyatarajia yafanyike ndani ya muda wa miaka 5 pekee. Mambo hayo yanayo washangaza wengi ni pamoja na yafuatayo:

SEKTA YA MAJI
1. Wananchi wa maeneo ya Chalinze, Ubena Zomozi, hadi Bwawani wote walikuwa hawana maji ya kunywa na kuteseka sana kwa shida ya maji licha ya kuwepo kwa mradi wa maji wa wami ambao ulikuwa kama mapambo tu. Leo hii wananchi walewale walio teseka miaka yote wanapata maji chini ya Serikali ya awamu ya tano.

2. Wananchi wa Makurunge, Fukayosi, hadi Kiwangwa Wilayani Bagamoyo wameteseka miaka yote lakini ndani ya miaka 5 ya Serikali ya Awamu ya Tano wanapelekewa mradi mkubwa wa maji kutoka chanzo cha maji cha Ruvu chini.

3. Wananchi wa Kisarawe toka Wilaya ya Kisarawe ilipoanzishwa mwaka 1907 walikuwa hawajawahi kuona maji ya bomba licha ya mto Ruvu kupita ndani ya Wilaya yao lakini ndani ya kipindi kifupi cha Serikali ya Awamu ya Tano wananchi hao wameona muujiza wa kupata maji ya bomba.

4. Wananchi wa Mkuranga miaka yote wameteseka lakini ndani ya muda mfupi wa Serikali ya Awamu ya Tano wanapata maji ambayo ambayo ayakuwepo kabisa katika ndoto zao.

5. Jiji la DSM lilikiwa na uhaba mkubwa wa maji ambapo kuna maeneo kulisambazwa mabomba kwa muda mrefu maarufu kwa jina la mabomba ya Mchina lakini Serikali ya Awamu ya Tano imewezesha kupatikana kwa maji mengi ya kutosha kutoka chanzo cha Ruvu juu na Ruvu chini hivyo kuyafanya mabomba hayo na maeneo mengine kuweza kupata maji ya kutosha kwasasa.

6. Kupitia visima virefu vya Kimbiji na Mipera vinakwenda kuondoa kabisa shida ya maji kwa wakazi wa Kigamboni, Mbagala, na Maeneo ya Wilaya ya Mkuranga kupitia mradi mkubwa unao tekelezwa na DAWASA.

7. Wakazi wa Simanjiro wameteseka miaka yote lakini ndani ya miaka 5 mradi kubwa wa maji hadi Olkesmet umekamilika

8. Wakazi wa Korogwe , Same, hadi Mwanga wanakamilishiwa mradi mkubwa wa maji wa kihistoria katika Wilaya hizo tatu.

9. Jiji la Arusha limenufaika na mradi mkubwa wa maji wa zaidi ya shilingi bilion 520

10. Mradi kubwa wa maji unao endelea kutoka Ziwa Victoria ambapo wakazi wa Nzega,Igunga, Tabora, hadi Sikonge wanapatiwa maki kwa mradi unao gharimu Dola za Kimarekani milion 268.35 (zaidi ya shilingi bilion 600 pesa za Kitanzania)

11. Miradi mikubwa ya maji kwa maeneo ya Lamadi, Bukoba, Kigoma, Lindi, Longido, na maeneo mengi nchini imekuwa ukombozi kwa wananchi ambayo yote inatekelezwa chini ya serikali ya Awamu ya Tano.

SEKTA YA ELIMU
1. Serikali imeweza kuwawezesha watoto wa ki-Tanzania kupata elimu bila kubaguliwa kwa kuwawezesha utoaji wa zaidi ya shilingi bilion 23.86 kila mwezi hivyo kuwawezesha hata watoto wa kutoka familia masikini kuweza kupata elimu

2. Utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu

3. Zoezi kubwa la Ukarabati wa shule zote 89 Kongwe hapa nchini ambapo shuleni 73 tayari zimekamika na shule 16 zilizobaki zinaendelea na hatua mbalimbali za maboresho

4. Ujenzi wa mabweni, mabwalo, madarasa, matundunya vyoo, na nyumba za walimu unaendelea Nchi nzima kwa shule za msingi na Sekondari. Na kwasasa serikali imepeleka zaidi ya shilingi bilion 170 kwaajili ujenzi wa miundombinu mipya katika shule za msingi na Sekondari

5. Kila Afisa Elimu mkoa (REO) amepewa gari jipya kwaajili ya kusimamia elimu hapa nchini

6. Waratibu elimu kata (WEO) wamepewa pikipiki mpya kila mmoja kwaajili ya kusimamia elimu katika shule zao ndani ya Kata wanazo zisimamia

7. Taratibu za manunuzi ya magari kwa maafisa Elimu (DEO) wa Wilaya zote unakamilika

8. Vifaa vya maabara vimenunuliwa na kusambazwa kwa lengo la kuwajengea vijana uwezo wa kusoma kivitendo masomo ya sayansi

9. Zaidi ya walimu elfu 21 wa shule za msingi na Sekondari wameajiriwa na kusambazwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini

10. Hosteli nyingi za wanafunzi pamoja na majengo ya maktaba, maabara, na vyumba vya midahalo vimejengwa katika vyuo mbalimbali hapa nchini vikiwemo Chuo Kikuu cha DSM, SUA, MUST, Mkwawa, na vyuo vingine vya umma.

11. Kuongezeka kwa kiwango cha fedha za mikopo pamoja na wanufaika wa mikopo, n.k

SEKTA YA AFYA
Katika Sekta ambayo imefanyiwa mapinduzi makubwa hapa nchini ndani ya miaka 5 ni Sekta ya Afya. Mafanikio yaliyo patikana ni kama ifuatavyo:

1. Ujenzi wa vituo vya Afya 487 vyenye uwezo wa kufanya huduma ya upasuaji ikilinganishwa na vituo vya Afya 115 vilivyokuwa na uwezo wa kufanya huduma ya upasuaji mwaka 2015.

2. Ujenzi wa hospitali mpya 99 za Wilaya ikilinganishwa na hospitali 77 za serikali tulizokuwa nazo kabla ya serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani. Ikumbukwe kwamba serikali ya Awamu ya Tano ilianza kujenga hospitali mpya 67 za wilaya na sasa imeongeza ujenzi wa hospitali zingine 32 mpya na hivyo kuweka historia ya kipekee hapa nchini katika uimarishaji wa Sekta ya Afya hapa nchini.

3. Ujenzi wa hospitali za rufaa na hospitali za kanda zaidi ya 11 hapa nchini

4. Upelekeaji wa dawa na vifaa tiba ambapo bajeti yake imeongezeka kutoka bilion 31 kwa mwaka 2015 hadi bilion 270 kwasasa

5. Usambazaji wa magari ya wagonjwa

6. Ongezeko la watumishi kwani zaidi ya watumishi elfu 12 wameajiriwa na kusambazwa katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma ya afya.

Juhudi hizi zilizofanywa na Rais DKT. JOHN POMBE MAGUFULI zimesaidia kuokoa maisha ya kinamama mengi wajawazito pamoja na watoto kwani ikumbukwe wananchi wengi walikuwa wanazifuata huduma mbali sana wengine walikuwa wanasafiri zaidi ya kilometa 140 kufuata huduma ya upasuaji pindi mama mjamzito anaposhindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.

UBORESHAJI WA MIJI YETU
Katika kipindi cha miaka 5 tumeshuhudia uboreshaji wa hali ya juu katika miji yetu hapa nchini. Zaidi ya shilingi Trilion 2.1 zinatumika. Tumeshuhudia Jiji la DSM, Tanga, Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma, Manispaa zote, na halmashauri za miji yote ikifanyiwa mapinduzi makubwa. Mambo makubwa yaliyo fanyika ndani ya kipindi hiki cha miaka 5 ni pamoja na yafuatayo;

1. Ujenzi wa mtandao wa barabara za Lami za kisasa zaidi zilizowekwa mataa

2. Ujenzi wa mifereji ya kusafirishia maji

3. Ujenzi wa standi za Kisasa na masomo ya kisasa zaidi

4. Ujenzi wa madampo ya Kisasa na ununuzi wa mitambo ya kuzolea taka

5. Miji yote imeandalia Master Plan ikilinganishwa na hapo awali

UJENZI WA MIUNDOMBINU
Tanzania inashuhudia mapinduzi makubwa sana kwasasa. Ujenzi wa barabara za Lami kila eneo unaendelea. Miongoni mwa miradi mikubwa inayo endelea ni pamoja na

1. Ujenzi wa barabara ya Mpanda hadi Tabora, Mpanda kwenda Kigoma, Tabora kwenda Kigoma, Kigoma kwenda Nyakanazi.

2. Ujenzi wa barabara ya Mbinga kwenda Bambabay na Tabora kwenda Itigi.

3. Kukamilishwa kwa barabara ya Iringa kwenda Dodoma, Dodoma kwenda Babati

4. Ujenzi wa barabara katika mikoa yote hapa nchini

5. Ujenzi wa barabara 8 ya Ubungo hadi Kibaha

6. Upanuzi wa barabara ya mwenge, Mwanza kati kwenda airport, Iringa kwemda Mbeya.

7. Ujenzi wa madaraja makubwa yakiwemo Thibiti, Kilombero, Nyerere, Magala, Tanzanite, na daraja la Busisi-Kigongo, daraja la Mfugale, na njia za juu za Ubungo.

8. Upanuzi wa bandari za DSM, Tanga, Mtwara, Kigoma na bandari zingine katika maziwa yetu

9. Ununuzi wa ndege mpya 11 kwa fedha za watanzania

10. Ujenzi wa meli mpya na ukarabati wa meli kadhaa pamoja na ujenzi na ukarabati wa vivuko vingi
Ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege vikiwemo DSM Terminal III, Tabora, Mtwara, Katavi, Dodoma, na Mwanza

11. Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR kutoka DSM hadi Makotopora Wilayani Manyoni ambapo zaidi ya shilingi Trilion 7 zinatumika.

12. Ujenzi wa mradi mkubwa wa Umeme wa Nyerere ambapo zaidi ya shilingi Trilion 6.5 fedha za walipa kodi wa Tanzania zinatumika. Mradi utakao zalisha Megawat 2115 ikilinganushwa MW.1560 tunazo zalisha sasa.

13. Upanuzi wa Kinyerezi 1 na Kinyerezi 2

14. Vijiji vyenye umeme vimeongezeka kutoka wastani wa vijiji 2000 kwa mwaka 2015 hadi zaidi ya vijiji 9000 hadi Juni, 2020.

MAKUSANYO YA SERIKALI
Kama mnavyo fahamu serikali yetu hadi mwaka 2015 tulikuwa tunakusanya wastani wa shilingi bilion 800 kwa mwezi. Lakini kwasasa makusanyo yameweza kuimarika kufikia wastan wa shilingi trillion 1.5 kwa mwezi. Makusanyo haya yameweza kuelekezwa katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali kama ilivyo elezwa hapo juu ili kukuza Uchumi wa Nchi yetu. Kwasasa Nchi yetu imepata heshima kwa kuingia katika nchi ya Uchumi wa kipato cha kati(wa hali ya chini) kama ilivyo ainishwa na Bank ya Dunia mnamo tarehe 01 July, 2020. Kinacho takiwa kwasasa ni kwakila Mtanzania kuchapa kazi ili pato letu lizidi kuongezeka kwa kufikia Nchi yenye Uchimi wa Kipato cha kati ulio imarika.

Haya ni baadhi ya mambo mengi yaliyo fanyika ndani ya miaka 5 ambayo mengine kwa Sekta za Utalii, Viwanda, Mifugo, Uvuvi, Sanaa, na Utamaduni ambayo ni mengi zaidi ambayo sikuweza kuyaeleza hapa.

Safari hii yenye kutia matumaini makubwa ni safari ya watanzania wote. Tunapaswa kuungana na maono makubwa ya Rais wetu ambaye amejipambanua katika kuwatumikia wananchi kwa moyo wake wote.

Mungu akubariki sana Rais wetu DR. JOHN POMBE MAGUFULI
Mungu tubariki watanzania
Screenshot_20200730-133113_1.jpg
Screenshot_20200730-132910_1.jpg
 
JK ameshaweka rekodi sawa ile jana, kwamba ni mambo yaliyopangiliwa kwa awamu kuanzia utawala wa Mzee Mkapa
Raisi Mstaafu Kikwete, ni muungwana mno, na ndivyo alivyo! Kuweka wazi hivyo ni Jambo jema, lakini unajiuliza, ni kivipi awamu zao zote maraisi wanne wapite waache pato la mtu ni $980 tu na kumwschia mwenzao mpango wa kufikisha $3000 Kwa kipindi cha miaka kumi pekee ili Hali wao waliishia $900+ huku wakiwa na Uongozi wa zaidi ya miaka 50+

Huoni kwamba aliyekabidhiwa waliuona Uwezo wake?

Lazima na Sisi tuwe tunajiuliza maswali bhana, tusiwe washabiki wa kuzomea pekee

Ingawa mafanikio yote yakiwepo ni lazima sifa zote ziwaendee viongozi wetu Kwa pamoja, Ila pia mtu mwenye akiri hawezi kuchukua maendeleo ya kiongozi mmoja aliyedumu Kwa miaka kumi, ulinganishie na Uongozi wa miaka minne na, huko ni kumuonea

Na kama kweli pia, kama amefanya makubwa kushinda ya miaka kumi iliyopita, kuna sabb za mtu kuzuwiwa kumpongeza huyo kiongozi?
 
Mtabumba bumba mengi ila pia msisahau pana barabara kuu kupo kama hivi na ajali ni kila leo.

Hii ni Rusahunga - rusumo 90km njia kuu kwenda Burundi, Uganda, Rwanda na DRC kama ilivyo sasa:

Nitaendelea kuongeza picha zaidi za hali ilivyo kwenye bandiko hili. Nichape kazi kwanza.

IMG_20200710_105850.jpg

IMG_20200730_150916_004.jpg
 
Raisi Mstaafu Kikwete, ni muungwana mno, na ndivyo alivyo! Kuweka wazi hivyo ni Jambo jema, lakini unajiuliza, ni kivipi awamu zao zote maraisi wanne wapite waache pato la mtu ni $980 tu na kumwschia mwenzao mpango wa kufikisha $3000 Kwa kipindi cha miaka kumi pekee ili Hali wao waliishia $900+ huku wakiwa na Uongozi wa zaidi ya miaka 50+

Huoni kwamba aliyekabidhiwa waliuona Uwezo wake?

Lazima na Sisi tuwe tunajiuliza maswali bhana, tusiwe washabiki wa kuzomea pekee

Ingawa mafanikio yote yakiwepo ni lazima sifa zote ziwaendee viongozi wetu Kwa pamoja, Ila pia mtu mwenye akiri hawezi kuchukua maendeleo ya kiongozi mmoja aliyedumu Kwa miaka kumi, ulinganishie na Uongozi wa miaka minne na, huko ni kumuonea

Na kama kweli pia, kama amefanya makubwa kushinda ya miaka kumi iliyopita, kuna sabb za mtu kuzuwiwa kumpongeza huyo kiongozi?
Mkuu mpango ulianza kipindi Cha mkapa na akaweka miundombinu ya kuwezesha hilo. Jk akamalizia,so ilitegemewa Rais wa awamu ya tano atakuwa anaendesha kwenye lami na hivyo kwenda speed zaidi kuliko watangulizi wake,bahati ujuaji wake mwingi umemtoa kwenye reli kiasi Cha kuongeza USD 100 in five good years huku akiwa ameua na kuharibu mifumo iliyowekwa na watangulizi wake
 
Hospitali saizi wamama wajawazito wanajifungulia pesa wakati kipindi cha nyuma walikatiwa bima Tena bure ,watoto chini ya miaka mitano wanatibiwa na pesa wakati nao walikuwa na bima na kutibiwa bila gharama . Na sasa madaktari na manesi wanapambana kusaka ajira.

Shule, elimu bure lakini kila siku watu wanachangishwa michango , mdogo wa mke wangu kaacha shule kwa sababu ya kukosa michango ya kupeleka shule. Ajira walimu kwa miaka mitano yote wako kitaa wanahusle.

Jamaa kibao waliacha mpaka ualimu wakaenda jeshini lakini wakarudishwa kitaa bila kuajiriwa.

Nenda kawadanganye wenzio. Na hii ni mipango ya mda mrefu tokea miaka ya nyuma.
 
Mkuu mpango ulianza kipindi Cha mkapa na akaweka miundombinu ya kuwezesha hilo. Jk akamalizia,so ilitegemewa Rais wa awamu ya tano atakuwa anaendesha kwenye lami na hivyo kwenda speed zaidi kuliko watangulizi wake,bahati ujuaji wake mwingi umemtoa kwenye reli kiasi Cha kuongeza USD 100 in five good years huku akiwa ameua na kuharibu mifumo iliyowekwa na watangulizi wake
Angalia pia migogoro waliomwachia huyo ambaye wakidhani wamemwachia kwenye mteremko aliyoshughurika Nayo

Ufisadi Rushwa na mikataba mibovu, hiyo kwako unaona ni mteremko?

Ni misingi ipi iliyokuwa imewekwa ili Kwa awamu hii kuwe mteremko?

Kwenye utalii kulikuwa na miluba iliyokuwa imeng'ang'ania Uchumi wetu, kwenye madini nako usiseme, Taifa halikuwa hata na ndege moja tu, mifumo ya ulipaji kodi ilikuwa ni ya kijinga tu, utasemaje kulikuwa ni mteremko mkuu
 
Raisi Mstaafu Kikwete, ni muungwana mno, na ndivyo alivyo! Kuweka wazi hivyo ni Jambo jema, lakini unajiuliza, ni kivipi awamu zao zote maraisi wanne wapite waache pato la mtu ni $980 tu na kumwschia mwenzao mpango wa kufikisha $3000 Kwa kipindi cha miaka kumi pekee ili Hali wao waliishia $900+ huku wakiwa na Uongozi wa zaidi ya miaka 50+

Huoni kwamba aliyekabidhiwa waliuona Uwezo wake?

Lazima na Sisi tuwe tunajiuliza maswali bhana, tusiwe washabiki wa kuzomea pekee

Ingawa mafanikio yote yakiwepo ni lazima sifa zote ziwaendee viongozi wetu Kwa pamoja, Ila pia mtu mwenye akiri hawezi kuchukua maendeleo ya kiongozi mmoja aliyedumu Kwa miaka kumi, ulinganishie na Uongozi wa miaka minne na, huko ni kumuonea

Na kama kweli pia, kama amefanya makubwa kushinda ya miaka kumi iliyopita, kuna sabb za mtu kuzuwiwa kumpongeza huyo kiongozi?
Ilo Pato la $900 liliendana na maisha ya wakati huo na kukidhi mahitaji. Lakini sasa ili pato $3000 ambalo bado unaendelea kudaiwa dola $2500 linatia shaka sana. Hii imesababisha walimu wengi wastafu wanatapeliwa na kukopa mikopo yenye mikataba ya ovyo kabisa na yenye riba ya 120%.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angalia pia migogoro waliomwachia huyo ambaye wakidhani wamemwachia kwenye mteremko aliyoshughurika Nayo

Ufisadi Rushwa na mikataba mibovu, hiyo kwako unaona ni mteremko?

Ni misingi ipi iliyokuwa imewekwa ili Kwa awamu hii kuwe mteremko?

Kwenye utalii kulikuwa na miluba iliyokuwa imeng'ang'ania Uchumi wetu, kwenye madini nako usiseme, Taifa halikuwa hata na ndege moja tu, mifumo ya ulipaji kodi ilikuwa ni ya kijinga tu, utasemaje kulikuwa ni mteremko mkuu
Hakuna mgogoro alioachiwa, Ila uwezo wake mdogo kwenye kuhandle,kuanalyse na kudeal na issues ndo kumepelekea hiyo migogoro isiyo na tija kwa nchi yetu.Hata familia ukiiendesha kwa mihemko lazima ikushinde
 
Ilo Pato la $900 liliendana na maisha ya wakati huo na kukidhi mahitaji. Lakini sasa ili pato $3000 ambalo bado unaendelea kudaiwa dola $2500 linatia shaka sana. Hii imesababisha walimu wengi wastafu wanatapeliwa na kukopa mikopo yenye mikataba ya ovyo kabisa na yenye riba ya 120%.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huna hoja kaa kimya Acha wenye upeo Wautendee haki Ubongo wao
 
Hakuna mgogoro alioachiwa, Ila uwezo wake mdogo kwenye kuhandle,kuanalyse na kudeal na issues ndo kumepelekea hiyo migogoro isiyo na tija kwa nchi yetu.Hata familia ukiiendesha kwa mihemko lazima ikushinde
Mkuu, Kwa namna ilivyokuwa, ili kuondoka kwenye mkwamo huo, ilikuwa imebaki njia hiyo pekee ya kushughurikia hayo

Huwezi kuwabembeleza wauza nyara za serikali, twiga na n.k

Huwezi kuwa rafiki wa watoa Rushwa halafu ukaendelea kufanya vizuri mkuu
 
Wewe utakuwa msukuma,umejazwa propoganda uchwara nawe umezibeba na unashupaza shingo,pole sana
 
Kilimo kwanza

Big results now

Ilikuwa ni mipango iliyolenga kutekeleza mpango wa dira 2025

JPM badala ya kurekebisha mapungufu na kuboresha yeye kafuta hivyo vitu, vitu ambavyo tayari vilishatumia mabilion ya heka kuvianzisha

Sasa sijui na yeye atajisikiaje akija rais mwingine na kupiga chini mipango yake na kuleta mingine mipya kabisaa.

Nchi inahitaji continuity ya mipango
 
Watendaji wa vijiji wanahaa usiku kucha kutekekeza miradi ya ujenzi wa zahanati, na madarasa kwa kuchangisha wananchi pamoja na kutafuta wahisani hakuna pesa inayotoka serikalini zaidi ya nguvu ya wananchi wenyewe.

Barabara ya kutoka Kilombero mpaka Ifakara ni kipande kidogo tu lakini tokea ajinadi kwa wananchi alipotembea Ifakara mwaka 2016 kuwa utawajengea kwa kiwango cha lami lakini mpaka leo barabara hiyo hakuna hata cha lami.
 
Back
Top Bottom