Lord OSAGYEFO
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 3,085
- 4,888
Hotuba ya bajeti ya 2022/2023 imetufumbua macho watu wengi jinsi mambo ya hovyo yaliyokuwa yanafanyika serikalini.
Hayati Magufuli na tawala zilizopita walikuwa hawabani kabisa matumizi ya serikali zaidi ya kuwa na matumizi ya hovyo.
Mtu ni Katibu Mkuu ametenguliwa na kupewa ukurugenzi wa manispaa lakini analipwa mshahara ule ule alipokuwa Katibu Mkuu.
Huu ni uhujumu uchumi wa kiwango cha juu sana. na bado inawezekana hata waliokaa benchi baada ya kutenguliwa waliendelea kulipwa mishahara ya nafasi walizotenguliwa vila kujali kuwa wapo benchi.
Magufuli akiwa waziri wa ujenzi aliwahi kumlaumu jk kwa serikali yake kununua magari ya kifahari na gharama kubwa, nilitarajia yeye alipokuwa rais serikali yake isingefanya hivyo lakini amenunua ma v8 mengi sana kwa ma DED, DC, DAS, RC, Manaibu Makatibu Wakuu, Makatibu Wakuu, Naibu Mawaziri na Mawaziri na viongozi wa CCM mpaka helikopta za kusindikiza misafara yake yenye magari ma v8 zaidi ya 50.
Ukweli uzalendo wa mwendazake ulikuwa wa kiini macho kwa Watanzania alikuwa hana uchungu na mali za umma.
Nampongeza sana rais samia kwa kuharibu kubana matumizi serikalini ila namshauri hizi nafasi nazo zitangazwe watu washindanishwe sio teuzi nazo ni DAS, DED, DC, RC naibu Katibu Mkuu na Katibu Mkuu kuna Watanzania wenye sifa na waadilifu wa kufanya kazi yenye tija kwa taifa.