AU yaridhia pendekezo la Kenyatta kutaka kujitoa ICC

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Viongozi wa Afrika wameridhia pendekezo la Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta la kutaka kuondolewa kwa mataifa ya Afrika katika Mkataba wa Roma uliyoiunda Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC mjini The Hague, Uholanzi. Pendekezo hilo lilipitishwa pamoja na ripoti ya kamati ya mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Afrika katika mkutano wa kilele wa umoja huo uliomalizika jana mjini Addis Ababa, Ethiopia, inayoitaka mahakama ya ICC kufuta kesi inayomkabili Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto na mtangazaji wa redio, Joshua Sang, wakidai kuwa kesi hiyo imekosa ushahidi unaoaminika.

CHANZO: DW KISWAHILI (DEUSTCHE WELLE)

 
Hiyo kwao ndio agenda muhimu kuliko zote kisa inawagusa!!!!Pamoja na mapungufu ya mahakama hii,ilikuwa ni msaada mkubwa kwa mwananchi wa kawaida wa kiafrika.Ya Zanzibar yanaweza kuja kutufanya tuone umuhimu wa hii mahakama.Tusubiri.
 
Sasa wataendelea kubakia madarakani Mpaka hapo Mungu atapowaita kuungana na "malaika" wengine....

Refer Mugabe Speech
 
Mahakama hii iliegemea kwa viongozi wa kiafrica huo ndio udhaifu wake lakini kwa upande wa pili ilikuwa kitisho kwa viongozi wasiojali haki za binadamu na kuwa msaada kwa raia masikini

Mataifa ya Africa yaliyo mengi yanaendeshwa kwa msaada ya wazungu sidhani kama wazungu wakikaza namba wana uwezo wa kuhimili.
Umuhimu wa mahakama bado upo hata kama ina udhaifu wake
 
AU ni KIJIWE cha madikteta wenye uchu wa madaraka hakuna la maana pale!
 
Kwa hali hiyo tutauwawa kama kuku na watawala wa Afrika ili wao na familia zao kwa mgongo wa vyama vyao waendelee kusalia madarakani,uvumilivu kwa wanaouwawa ukifika kikomo itakuwa ni vita ya wenyewe kwa wenyewe na hapo hakuna maendeleo tena tutabaki tukisuluhishana kwa migogoro tuliyoitengeneza wenyewe kwa uroho wa madaraka.

Nnaamini hata mmbuyu ulianza kama uyoga ,bara la Afrika mpaka sasa tumeshafeli katika mambo mengi.Hata katika hili tumeshafeli ,tunasubiri kuishi kwa mkono wa chuma tu..
 
Yani inamaana kati ya matatizo yote yanayoikumba afrika wao wameona ICC ndio la muhimu?burundi watu wanauwana kila uchwao wanashindwa kupata suluhisho alafu wanatupigia kelele tu.
 
Duuu lazima tupukutike kama BURUNDI wameshindwa kwa uroho wao wa madaraka (ZENJ)
 
Kujitoa mpaka wananchi wa nchi hizo waitisha kura ya maoni na bunge liridhie .maana viongozi wa kiafrika wengi ni madiktete wanaopenda madaraka hata jama wananchi hawawataki.wanatumia majeshi kubaki madarakani .
 

Ni Botswana peke yake iliyokataa kuunga mkono wazo hilo la kipuuzi la viongozi wa Africa
 
Mfano ni kama zanzibar wapiga kura hawaheshimiwi .haki zao hawapewi wanapewa walioshindwa
 
Na mimi najitoa katika mfumo wa mahakama wa Tanzania.
 
Naunga mkono hoja ya AU. ICC imeshindwa kuagiza kukamatwa kwa J. Bush na T. Blair kwa mauaji ya kimbali huko Iraq tena kukiwa na ushaidi wa waxi dhidi yao. Ni sahihi kujitoa. Matatizo yetu tuyamalize wenyewe!
 

Mimi nadhani hawa viongozi wetu wa Afrika wamechoka kufikiri. Azimio hilo kiukweli ni la kulinda serikali kandamizi zifanyazo mauaji kwa raia wake na kuwatesa pasipo chembe ya huruma kwa kujua kuwa wakijitoa ICC hakuna chombo kitakachowashughulikia kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake. Na kwa jinsi viongozi hawa wa Afrika wanavyojua kulindana itakuwa ni vigumu AU kuchukua hatua zozote dhidi ya nchi hizo. Viongozi hawa hawaambiani ukweli. Mfano, angalia viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanavyoshindwa kushughulikia mgogoro wa Burundi. Hakuna kiongozi hata mmoja kati yao aliyethubutu kusimama na kumkemea Rais Kurunzinza pale alipoanza mchakato wa kubadilisha katiba ya Burundi ili agombee kwa muhula wa tatu kama ambavyo Mwalimu J.K Nyerere alivyokuwa akifanya pale alipobaini mambo hayaendi sawa. Ni aibu kwa Bara letu mama la Afrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…