Athari za kuweka ukomo wa mtu kushika Uenyekiti wa Chama cha Siasa

Fundi Mchundo

Platinum Member
Nov 9, 2007
9,975
8,275
Kitu kimoja ambacho wengi wanamlaumu Mbowe ni kuwa amekuwa Mwenyekiti kwa muda mrefu sana. Wanasema hiyo imemfanya akose mbinu za kupambana katika mazingira ambayo ni tofauti sana na alipochaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mwenyekiti. Kwa sababu hiyo inahitajika damu mpya. Ili kuzuia jambo hilo kujirudia tena Lissu ameahidi kuwa akichaguliwa atabadilisha Katiba ya Chadema ili pawe na ukomo wa kuhudumia katika nafasi ya Uenyekiti, ubunge wa kuteuliwa na nyingine. Yeye amesema atahudumu sio kwa zaidi ya miaka 10. Mwaka 2035 CDM itakuwa na Mwenyekiti mwingine. Kwa vile hajaondoa lile tamko lake la kutaka kugombea urais tena, naamini atagombea tena nafasi hiyo. Na nadhani anaamini kuwa akiwa Mwenyekiti atahakikisha kuwa nafasi yake ya kushinda itakuwa kubwa kwa sababu atahakikisha kutakuwa na Tume Huru haswa ya uchaguzi. Mimi sidhani kama atafanikiwa katika hili maana hamna Mwenyekiti wa CCM ambae pia ni Rais wa nchi atakubali chama chake kishindwe.
Kwa sababu hiyo nadhani atakuwa na nafasi nzuri kuwa Rais wa JMT mwaka 2030. Akifanya vizuri katika urais wake atachaguliwa kwa mara ya mwisho kuwa Rais mwaka 2035. Ila wakati huo hataweza kugogombea Uenyekiti wa CHADEMA. Mtu mwingine atakuwa Boss wake ndani ya chama. Kama wataelewana, hapatakuwa na tatizo. Lakini wakitofautiana ndio shida itaanza. Mwenyekiti Mpya anaweza kumhujumu wazi wazi na hatakuwa na la kumfanya hasa kama atakuwa amejijenga kwenye chama. Nchi haitatawalika. Ndio maana CCM waliondokana na hilo na kuhakikisha kuwa Rais pia ni Mwenyekiti wa Chama chake. Ili kuhakikisha hili halitokei Lissu itabidi amaze watu wake katika Kamati Kuu ili Mwenyekiti awe mtiifu kwake tu. Tunarudi tulikotoka. Hili ni wazo baya na limeletwa ili kufurahisha umma.

Amandla...

Nguruvi3
 
Nimeona mahali bandiko linalosemekana kuwa ni li Wakili Jebra Kambole kuwa Mbowe akiwa Mwenyekiti itakuwa vigumu kunadi wagombea wa CDM mwaka 2025. Sijui kama anamaanisha kuwa itakuwa vigumu pia kumnadi mgombea wa urais Tundu Antipas Lissu maana mpaka sasa hivi hajabadilisha uamuzi wa kugombea nafasi hiyo! Aidha, anasahau kuwa hata Lissu anakiri kuwa hao wanaotamba sasa hivi walijengwa na Mbowe. Kama aliweza kwao, kwa nini asiweze tena?

Amandla...
 
Back
Top Bottom