ATCL kuanza safari Mkoa wa Dodoma January 16 2017

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,870


Sasa ni rasmi kuwa Januari 16 2017,ndege aina ya Dash8-Q400 itatua kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Dodoma.Hii ni hatua ya muendelezo wa ATCL kujitanua katika soko la ndani.

ATCL ambayo imeanzisha safari zake ktk miji ya Arusha,Mwanza,Kigoma na Zanzibar sasa itaanza kwenda mkoani Dodoma mara mbili tu kwa juma(Kwa kuanzia).Na nauli yake kwa kuanzia ni Tsh 165000 kwa daraja la kawaida na itabadilika kulingana na daraja mteja analokata.

Ndege pekee iliyokuwa inafanya safari kati ya Dsm na Dodoma ni ndege za kampuni ya Auric Air ambao walikuwa wanapeleka ndege aina ya C208-Grand Caravan yenye uwezo wa kuchukua abiria 12.Kampuni ya Flight link hupeleka ndege mara nyingi katika msimu wa vikao vya bunge.

Hivyo kwa kuanza na siku mbili kwa juma kuelekea mkoa wa Dodoma,ATCL inaenda kufungua fursa ya ushindani wa safari za anga katika mkoa wa Dodoma na kanda ya Kati.

[HASHTAG]#ATCL[/HASHTAG] [HASHTAG]#TheWingOfTheKilimanjaro[/HASHTAG]
 
Dah kwa bei hiyo sio mbaya. mimi na wife safiii ila sijajua kwa mtoto wa miaka 3 imekaaje
 
Dar-Arusha wamesimamisha wakisema sababu za kitaalam.Nachojua kutua Arusha kunataka special skills si kila rubani anaweza tua pale.
 
Tulishaamua nchi iende mbele na itaenda, anayedhani atakwamisha atakwama yeye -------Rais Magufuli.

Hamna namna watetea mafisadi chadema wajinyonge tu.
 
Bombadia Q 400 Safi sana wame fanya timing maana na vikao vya bunge ni ndani ya wiki mbili zijazo. Wabunge wengi watapanda bila shaka. Unaenda jtatu asbuhi na kurudi Dar ijumaa. Wiki endi kama kawaida wanavinjari Dar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…