Atakaekiri 2025 awe kutoka CCM au Upinzani kutenda kama Hayati Magufuli atajihakikishia ushindi kwenye udiwani na Ubunge lakini kwenye Urais ni Samia

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,216
1,848
Kuna kijisauti nakisikia na kinaniambia niwafikishie sauti hiyo wote wenye kutamani Udiwani na Ubunge wawe ni kutoka CCM au Upinzani.

Sauti inaniambia na imenihakikishia mambo makubwa matatu:

Jambo la kwanza, Mwaka 2025 Rais ni Samia na ushindi wake utaonekana 2024 kuelekea 2025 na kuna mambo muhimu sana atayakamilisha na kufanya "approval rate " yake kupanda sana.

Jambo la pili, kuelekea 2025 ataibuka mwanasiasa mwenye ushawishi lakini atatumia ushawishi wake kumsaidia Mama Samia lakini baadae atatumia ushawishi wake kujiinua. Ushawishi wake utakuwa ni zaidi ya wa Mrema na Lowassa.

Jambo la tatu, kuelekea 2025 jina la Hayati Magufuli litatumika na litatumiwa sana kama mtaji wa kura na hapa kila atakayekiri na kuahidi kutenda kama Hayati atajihakikishia ushindi wa kishindo kwenye udiwani na Ubunge iwe ni Upinzani au CCM.

Baada ya hapo kisauti kikapotea
 
Nimekukumbuka hizo mambo.

Yule mzee bora tulifanikiwa kummaliza na sasa analiwa na funza.
 
Back
Top Bottom