Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,488
- 7,021
Wakuu!
Ibada ya Ijumaa Kuu Kitaifa imefanyika katika Kanisa la KKKT Ushirika wa Ifakara Mjini, Dayosisi ya Ulanga Kilombero, ambapo imetumia nafasi hiyo kueleza kuhusu hali ya kisiasa na kijamii nchini, wakati huu Taifa likielekea kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 2025.
Akihubiria waumini na wageni waliohudhuria ibada hiyo, Askofu Mameo ameeleza kuwa kukamata watu na kuwaweka ndani si suluhisho la kupunguza malalamiko, bali ni kuongeza hofu na kutoaminiana.
Amesema Waafrika wengi, hasa viongozi, hawapendi kukosolewa na badala yake huishia kushambulia wakosoaji wao. Aidha, watendaji wa Serikali wametakiwa kuacha tabia ya kumdanganya Rais, kwani ni wajibu wa Serikali kusikiliza na kuchukua hatua juu ya malalamiko yanayohusu uchaguzi na kuwepo kwa manung’uniko dhidi ya Tume Huru ya Uchaguzi.
Viongozi wa kisiasa na vyama vyao wametakiwa watangaze sera zao badala ya kutegemea mihemko ya kisiasa, huku akionya kuwa Ikulu imegeuka kuwa sehemu ya lawama badala ya kuwa kitovu cha suluhisho.