BARAZA la Vijana wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT, Dayosisi ya Konde, limemtupia lawama Mkuu wa kanisa hilo nchini, Askofu Dk. Fredrick Shoo, likidai kuongoza mkutano wa kumwondoa Askofu wa dayosisi hiyo, Dk. Edward Mwaikali, badala ya kutafuta njia sahihi ya kumaliza mgogoro ....
[
https://res]
unaofukuta.
Akisoma taarifa ya msimamo wa vijana wa dayosisi hiyo jana, Marko Mahenge, alidai Askofu Dk. Shoo amekuwa sehemu ya kukuza mgogoro huo badala ya kutafuta njia sahihi ya kujadili namna ya kushughulika na jambo hilo ambalo linaendelea kuyumbisha Dayosisi ya Konde.
Alisema kwa muda mrefu vijana walikuwa kimya wakifuatilia mwenendo ya mgogoro huo huku wakitarajia kufanyika kwa hekima na busara katika kushughulikia maridhiano ya kuhamisha makao makuu ya dayosisi hiyo kutoka mjini Tukuyu katika Wilaya ya Rungwe na kupelekwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
“Sisi vijana wa Jimbo hili la Mbeya na maeneo mengine ya dayosisi hii tunapinga vikali uamuzi wa Mkuu wa Kanisa kumwondoa Askofu Mwaikali kwenye kiti chake kwa sababu mkutano uliofanyika Machi 22, katika Ushirika wa Uyole ulikuwa batili, tunamtambua Dk. Mwaikali kuwa ndiye askofu wetu na hapa jimboni haondoka wala mchungaji au Mkuu wa Jimbo,” alisema Mahenge.
Aidha, Mahenge aliliomba Baraza la Maaskofu wa kanisa hilo nchini kuingilia kati mgogoro huo kwa kuiita halmashauri kuu ya dayosisi na viongozi wengine ili kukubaliana mambo ya kufanya.
Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Ruanda, yalipo makao makuu ya Dayosisi ya Konde, Mkuu wa Jimbo, Mchungaji Nyibuko Mwambola, alisema Halmashauri Kuu haitambui mkutano ulioitishwa na Askofu Dk. Fredrick Shoo kwa madai kuwa ulikuwa batili.
Alimtupia lawama Askofu Dk. Shoo kama mkuu wa kanisa kwa kushindwa kusuluhisha mgogoro huo na kuwa sehemu ya kuchochea hali ambayo alidai inazidi kuongeza chuki na mfarakano.
Kadhalika, alisema baada ya mkutano wa kumchagua askofu mwingine, Geofrey Mwakihaba, Askofu Dk. Shoo alituma waraka kwa taasisi zote za kifedha kufunga akaunti za dayosisi.
Alisema hatua hiyo imewasababishia kushindwa kufanya malipo yoyote ikiwamo mishahara ya wachungaji na watumishi wengine wa dayosisi hiyo.
Vile vile, alidai kuwa Dk. Shoo amewatumia barua wachungaji wote wa Dayosisi ya Konde kuhudhuria kikao kinachofanyika kesho jijini Dodoma, bila kumpa taarifa Askofu wa Jimbo Dk. Mwaikali, na kwamba Halmashauri Kuu imesema naye atashiriki kikao hicho.
“Mkuu wa Kanisa ameonyesha dhahiri upande alipo kwa sababu ameshindwa kutukutanisha pamoja viongozi wa dayosisi na kujadili pamoja namna bora ya kumaliza huu mgogoro badala yake ameonesha wazi kushindwa kusimamia jambo hilo na kuchangia kuchochea suala hili, sisi tunamtambua bado Askofu Mwaikali ndiyo anasimamia dayosisi yetu ya Konde,” alisisitiza.
“Haiwezekani Mkuu wa Kanisa aitishe mkutano na kufanya uchaguzi wa kumchagua askofu mwingine, tena kwa siku moja, inaonyesha dhahiri kuna chuki binafsi na sio suala la kuhamisha makao mkuu ya dayosisi.”
Machi 22 mwaka huu Mkuu wa Kanisa la KKKT nchini, Askofu Dk Fredrick Shoo, pamoja na wajumbe 201 walifanya mkutano katika Usharika wa Uyole jijini Mbeya kwa lengo la kumaliza mgogoro huo ambapo liliibuka suala la wajumbe kutokuwa na imani na Askofu Dk. Edward Mwaikali.
Katika mkutano huo ambao uliendeshwa na Askofu Dk. Shoo na kudumu kwa saa 10, ulitumika kumchagua Askofu mwingine Mchungaji Geofrey Mwakihaba, ambaye alitangazwa mbele ya wajumbe wa mkutano.
Kutokana na uamuzi huo baadhi ya vijana wa KKKT mkoani Mbeya walieleza kuwa mchakato uliotumika kuwa ulikuwa batili.
Hata hivyo, Askofu Dk. Shoo alipotafutwa na Nipashe kwa simu jana, muda wote hakupatikana kuzungumzia suala hilo.
Mgogoro wa kwanini yahamishwe makao makuu ya dayosisi kutoka mjini Tukuyu katika Wilaya ya Rungwe na kwenda Halmashauri ya Jiji la Mbeya, ulianza kufukuta tangu mwaka 2017 hadi sasa.
Askofu Dk Shoo na Bagonza wanajitambulisha kama vinara wa kupenda haki na kutii katiba, katika Jimbo la Konde, wamedhihirisha rangi yao, wamevunja katiba ya kanisa ili kumuondoa Askofu Dk. Mwakitali.
Dk Mwakitali ni moja ya maaskofu wa KKKT ambao wamejikita katika kazi ya kichungaji zaidi na sio udalali wa kisiasa wa kutafutia wanasiasa nafasi za uongozi.
Kuna madai kwamba Bagonza na Dk Shoo wameandaa mkakati wa "kufagia" viongozi wa dini katika kanisa Hilo ambao wanajifanya wanashughulika na kazi ya uchungaji zaidi kuliko Siasa. Na wanataka wanasiasa, hasa viongozi wa CHADEMA, wapate nafasi ya kuhubiri Siasa Kila jumapili katika makanisa yote nchini ili chama hicho kichukue dola, na kisaidie kanisa Hilo kujiimarisha dhidi ya makanisa mengine.
Kama wanashindwa kutii katiba ndani ya kanisa, hawana mamlaka ya kusemea katiba ya nchi, charity begins at home. Hata katiba mpya wanayosemea Kila siku, wakipewa uongozi wa nchi pamoja na wenzao wa chadema, wataikiuka tu.