Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 289
- 484
Askofu wa AICT Dayosisi ya Pwani, Philipo Mafuja ametoa wito kwa viongozi wa Dini kipindi hiki cha uchaguzi kuwa makini katika nyumba zao za Ibada ili kuepuka kutoa kauli za uchochezi ambazo zinaweza kupelekea uvunjifu wa amani nchini.
Akizungumza katika Kongamano la amani kwa viongozi wa dini kuelekea uchaguzi Mkuu, ambalo limefanyika leo April 23, 2024 Jijini Dar es salaam kwa kuwakutanisha baadhi ya viongozi wa dini, amesema viongozi wa dini wanaaminika sana hivyo wanatakiwa kuwa makini wanapopata fursa ya kuzungumza.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Aidha Askofu Philipo Mafuja, amewahasa viongozi wa dini kuacha kuingilia mamlaka za kisheria kwenye masuala ambayo yanagusia Sheria hasa kipindi hiki cha uchaguzi.
Amesema kwamba katika kipindi hiki cha uchaguzi wapo wanasiasa wataanza kwenda kwenye nyumba za Ibada pamoja na kuwakaribisha viongozi wa dini kwenye majukwaa yao, amewahasa kuwa makini nao, pamoja na wao wenyewe kuwa makini wanapozungumza.