Frank Wanjiru
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 22,626
- 40,526
Wakati wa 'zama zilizotimu' ulinitafuta sana na ukataka kuonana nami lakini ukaishia kuonana na 'itifaki ya Askofu' iliyokueleza mazingira ya Askofu, uliridhika ila juhudi zako za kumtafuta Askofu hazikukoma - uliendelea hasa ukitaka kumuelewa zaidi Askofu huyu.
Ulipokuwa ukitafuta kupanda ngazi kati ya zile alizoziainisha Maslow, Maslow's Hierarchy of Needs', ulijitahidi kujenga hoja zilizonakshiwa na kutiwa manukato katika harakati za Askofu. Ingawa hukuweza kutafsiri vizuri taarifa kutoka kwa Prof Mpoki Mafwenga (RIP) juu ya Askofu, lakini andishi lako la Oktoba 2020 liliwasaidia vijana kutoka 'Ngudu' na 'Kamachumu' kutafuta kumfahamu zaidi Askofu ili waoanishe kati ya kile kilichokuwa katika andiko lako na taarifa za kutoka 'Ukerewe'!
Wakati wa harakati katika zama zilizotimu na zama zinazopumua tulishindana kwa hoja na fikra. Utofauti katika mitazamo yetu havikuwa sehemu ya majaribu yetu - wote tulilishinda lile jaribu la kushambuliana kwa mambo binafsi. Pale tulipojibizana kwa hoja tukawa sehemu ya chakula cha ubongo, hisia na fikra kwa vijana wengi wakiwemo wale wa Ufipa, Lumumba na Mwembe Chai!
Hoja zako katika zama hizi juu ya DP World zilisaidia kupooza mashambulizi dhidi ya Timu ya Chamwino ikiongozwa Mh.Jerry Slaa et al. Hakuna upande usiohitaji vijana wenye fikra. Na wewe ulikuwa ni mmoja wa vijana wa fikra katika taasisi ya mbindipindi! Prof. Mwandosya anaweza kuwaeleza maana ya mbindipindi! Ila, kusema kweli ulichangia kuleta algebra katika mzozo ule na algebra ikatengeneza 'Pembetatu ya Pasukali' - Wafipa huita 'Paschal's Triangle'!
Ingawa tulitofautiana katika kufikia utimilifu wa jamii, lakini wakati wa shida, kama binadamu tuliungana na tukatiana moyo. Kile ambacho ulikipambania hukuwahi kukifaidi ndani ya huo mfumo ingawa kulikuwa na dalili kuwa ulikuwa unaandaliwa na benchi la ufundi ili uitwe katika timu inapojiandaa katika michuano ijayo. Je, ni nani atapuuza mchango wako katika taasisi ile iliyozaliwa Februari 5, 1977?
Umeondoka ukiwa katika mapambano. Ndiyo! Hukutaka kushindwa na ugonjwa kama vile pia hukutaka kushindwa na hoja za mlengo ule wa kushoto. Wakati wa ugonjwa wako, vijana wote waliungana kukupambania wakiongozwa hasa na Malisa GJ na Yericko Nyerere! Najua kuwa na hata vijana wa Lumumba walikupambania. Mapambano yao wote kwa pamoja na sauti zao zikafika kwa Umwehe Mkuu na wasaidizi wake.
Umeondoka Thadei Ole Mushi! Mimi sina hadhi hata themuni au sudusu ya kuandika wasifu wako! Yule Mkuu wa Itifaki ya Askofu, ambaye ulikuwa unawasiliana naye wakati unamtafuta Askofu, anakulilia! Askofu anakulilia pia! Vijana wote wanakulilia na Tanzania imeinama baada ya kusikia taarifa kuwa umefarakana na dunia hii yenye utamu, uchungu na changamoto.
Natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na hata marafiki. Natoa pole kwa Mwenyekiti wa CCM ambaye amempoteza kijana aliyekuwa mstari wa mbele kumpambania hasa miaka miwili ya maisha yake. Natoa pole kwa watu wote kutoka Kilimanjaro kwani huyu 'mwanahija' mwenzao amewatoka. Requiescat in Pace! Lala salama! Safiri salama 'Mangi'! Mungu akayakumbuke mema yako na akayape kisogo mapungufu yako! Tarokisha! Ugonege! Adios!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 4 Februari 2024; 8:08 mchana.