Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 519
- 1,246
Askofu Malasusa akiwa katika sherehe ya kuingizwa kazini amesema;
"Tukio hili la kuingizwa kazini linatokea wakati Dunia inashuhudia vita mbalimbali ikiwa ni pamoja na vita kule Ukraine, sasa tunasikia Gaza na Israel, lakini pia nchi ya Kongo bado napitia katika masikitiko makubwa na mitikisiko mikubwa, watu hawana uhakika na usalama wao na maisha hayo.
"Hali inayofanya wananchi wengi kukosa utulivu na wanaendelea kuwa mafukura. Moja ya kundi la viongozi wa kiroho lilipita kule KOngo na kuona jinsi ambavyo nchi hizi za maziwa makuu zinavyopitia katika hali mbaya sana.
"Niwasihi sisi watanzania yeyote ambaye anatamani kuleta machafuko katika nchi tumsihi na kumuombea kabisa ili ashindwe katika jina la Yesu, tunahitaji sana amani na utulivu katika nchi yetu.
"Sisi ambao tmepata fursa ya kuona na kuishi katika maeneo ambayo watu hawana amani ni jambo ambalo halikubaliki.
"Kila mchungaji anajukumu la kudumisha amani, niwaombe ndugu zangu kama kuna jambo zuri katika lolote, ili tusiingie katika jambo lolote ambalo litatuharibia tanzania yetu tuendelee kuwa na mazungumzo, mazungumzo ni kitu muhimu sana hata Mungu mwenyewe wa Nabii Isaya aliruhusu mazungumzo, njooni tusemezane.
"Sisi sote tusikakae mazungumzo iwe ndani ya kaya, ndani ya familia, katika maisha na hasa sisi wanasiasa tusikatae mazungumzo. Ndani ya mazungumzo Mungu anaonekana, tusichukue hatua nyingine zaidi ya Mazungumzo."