Askofu Malasusa: Mikoa ya Lindi, Mtwara, Singida, Shinyanga na Mwanza imeathirika Sana kimazingira, Eden yetu ni Tanzania Tuitunze!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
93,961
164,208
Mkuu wa KKKT Askofu Dr Malasusa amewataka Watanzania kutunza Mazingira kwani hii Ndio Aden yetu tuliyorithishwa na Mungu wa Mbinguni

Askofu Malasusa amesema Utunzaji wa Mazingira ni swala la kiroho na hii Dunia ni yetu sote hivyo tuitunze

Mikoa ya Lindi Mtwara Singida Shinyanga na Mwanza imeathirika Sana kimazingira, amesema baba askofu

Source Upendo TV

Nawatakia Dominica Njema 😄
 
Nawatakia Dominica Njema
Askofu wa mchongo changono mkubwa
 
Ndo yule anaevaaga kikofia flan kidogo kama ganda la chungwa?
 
Vijana wanalalamika maisha magumu hata kupanda TU miti wapate pesa za bure toka carbon credit hili nalo hatuwezi.
KAZI Simba na yanga diamond na zuchu tu
 
Lindi??????????????????? Kvp ilihali Lindi ipo kwenye top ya mikoa iliyohifadhi uoto wa asili
Hayo yalisemwa kwenye siku ya kupanda miti 2023.. Asilimia kubwa ni selous yako maeneo machache Kilwa njia ya liwale yaliyovamiwa na wafugaj ila sio sana Lindi iko vzr na uhakika naishi Lindi labda singida ndo kweli miti imekatwa sana ila uoto wake ni forest fupi za itigi mfano
 
Mkuu wa KKKT Askofu Dr Malasusa amewataka Watanzania kutunza Mazingira kwani hii Ndio Aden yetu tuliyorithishwa na Mungu wa Mbinguni

Askofu Malasusa amesema Utunzaji wa Mazingira ni swala la kiroho na hii Dunia ni yetu sote hivyo tuitunze

Mikoa ya Lindi Mtwara Singida Shinyanga na Mwanza imeathirika Sana kimazingira, amesema baba askofu

Source Upendo TV

Nawatakia Dominica Njema 😄
Aseme tu ukweli kuwa wananchi wa hii mikoa hawajasoma zaidi ya kupata elimu ya kukariri Qur'an na ndiyo maana hawana maendeleo yeyote.
 
Mkuu wa KKKT Askofu Dr Malasusa amewataka Watanzania kutunza Mazingira kwani hii Ndio Aden yetu tuliyorithishwa na Mungu wa Mbinguni

Askofu Malasusa amesema Utunzaji wa Mazingira ni swala la kiroho na hii Dunia ni yetu sote hivyo tuitunze

Mikoa ya Lindi Mtwara Singida Shinyanga na Mwanza imeathirika Sana kimazingira, amesema baba askofu

Source Upendo TV

Nawatakia Dominica Njema 😄

Huyu naye ni chawa mtukufu.

Kanisa la KKKT zamani ndilo lililokuwa linagawa miche ya liti bure kwenye mashule ili kila mwanafunzi apande miti lakini siku hizi hali ni tofauti kabisa kila mtu anawaza mambo yake.
Kanisa linahamsisha waumini kujenga mahoteli na magest lakini mapato ya hayo mahoteli hatuoni wakitoa malimbiko wala fungu la kumi wala gawio kwenye mausharika waliotoa michango yao . Miradi mingi ya makanisa inatumiwa vibaya na inabaki kama midoli sebuleni kwa ajili ya fahari ya Macho.

Angalau kanisa Katoliki wanajitahidi kulinda na kutunza maeneo yao . Hata ukifika kwenye maeneo ya parokia zao zina mazingira mazuri na ya kupendeza sana. Lakini pia kwenye miradi inayotokana na michango ya watu hatuoni ikiwanufaisha waumini kivile .
Tulitegemea shule na hospitali za kaniza ziwe na gharama nafuu ili kuwabeba waumini maskini kama sehemu ya sadaka mana michango inatolewa na waumini wote bila kujali uwezo.

Safari za nje ndio zinazidi tu lakini kwenye michango waumini wa ndani ndio wawezeshaji zaidi..

Ulaya hakuna waumini na hawana habari labisa na mambo ya dini sasa sijui hizo safari hua ni kwa ajili ya kuwarudishia dini zao au ni vipi?😂😂

Ndio maana Viongozi wengi wa dini ni machawa wa watawala madhalimu kwa sababu wanafanana katika matendo yao. Ufisadi umewaunganisha kuwa kitu kimoja .

Kanisa linapaswa kuwa mfano katika kutunza mazingira lakini pia kutunza roho za watu katika kweli na maadili mema kwenye jamii.

Huwezi kutunza mazingira ya miti wakati watu wana njaa. Watalima kwenye vyanzo vya mito badala ya kulima pembezoni mwa mito mbali na vyanzo ili wanunue pampu wamwagilie. Mafuta yakiwa ghali kwa sababu ya kodi na tozo hawatamudu kumwagilia badala yake watachimba mifereji kienyeji na kuharibu mito ya maji.

Wakulima maskini watalima kilimo cha kuhamahama kama wafugaji kwa kuchoma misitu na kuwahamisha wafugaji ambao kiuhalisia hawachomi misitu zaidi ya ngombe wao kuongeza mbolea.

Kanisa lionyeshe namna bora ya si tu kutunza mazingira bali pia kutunza mapato ya kanisa kupitia michango na sadaka za waumini na si tu kushindana na fahari za dunia.

Hospitali za KKKT kama KCMC zimekuwa zikilaumiwa kwa huduma mbovu sana pamoja na ukubwa wake.
Tulitegemea pawe na usimamizi mkubwa wa kichungaji na kiroho. Wapo madaktari wenye roho mbaya na wenye roho nzuri bila kujali dini zao hao wanapaswa kuhudumia watu na kulipwa vizuri . Wale wakorofi wakatafute kazi huko kwenye hospitali za kijeshi huko Kongo na Burundi😂😂😂.

Lakini shida inatokana na ajira za kupeana.
Hili nalo Maaskofu Mliangalie kwenye dayosisi zenu na majimbo yenu.

Mkinichagua nitahakikisha serikali inakua na jukumu la kujenga misikiti na makanisa nchi nzima kulingana na mahitaji ili nyumba za ibada zisiwe ni mali ya mtu na kichaka cha kukwepa kodi na kutakatisha fedha.

Tanzania mpya inakuja yenye Muungano wa nchi mbili ,Tanganyika na Zanzibar.
 
W
Lindi??????????????????? Kvp ilihali Lindi ipo kwenye top ya mikoa iliyohifadhi uoto wa asili
Hayo yalisemwa kwenye siku ya kupanda miti 2023.. Asilimia kubwa ni selous yako maeneo machache Kilwa njia ya liwale yaliyovamiwa na wafugaj ila sio sana Lindi iko vzr na uhakika naishi Lindi labda singida ndo kweli miti imekatwa sana ila uoto wake ni forest fupi za itigi mfano
Wafugaji hawaharibu mazingira.
Ngombe zinatoa samadi hazitoi sumu.

Wakulima ndio wanaoharibu mazingira na kukata miti ili walime na kuchoma miti.
 
Back
Top Bottom