Askofu Kilaini atakiwa kumfunda Rais Magufuli

nivoj.sued

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
221
190


Askofu Kilaini ametakiwa kumfunda JPM kuhusu matumizi ya kanuni ya siasa ya ujamaa na kujitegemea. Kwa maelezo zaidi soma hapa chini:

==============================================
Askofu Kilaini Atakiwa Kumfunda JPM Kuhusu Kanuni ya Sera Auni, kwa Maana ya,“The Principle Of Subsidiarity”

Akiwa mkoani Kagera, Rais John Pombe Magufuli, baada ya kuhudhuria ibada ya mwaka mpya, alianza ziara ya kukutana na wananchi waliothiriwa na tetemeko la ardhi la Septemba 10, 2015. Katika ziara hizo, Rais Magufuli alisikika akisema yafuatayo, kati ya mambo mengine:

"Nimekuja kuwapa ujumbe huu, na mwenye kusikia asikie: Panapotokea janga kama vile tetemeko, jukumu la serikali ni kurejesha miundombinu ya umma, siyo kujenga nyumba za wananchi. Asitokee mtu kuwadanganya kwamba serikali itagawa chakula, kwani hatuwezi kugawa chakula kwa watu wanaoishi katika mazingira ya kijani. Ndugu Mkuu wa Wilaya nataka nikueleze hapa, sitaleta chakula hapa Bukoba, kwani serikali haina shamba. Kwa hiyo kila mmoja katika upande wake abebe msalaba wake mwenyewe. Tuachane na mambo ya kwenda kwenye ‘kijiji cha katerero,’ ‘kuogelea kwenye mto ngono,’ na ‘kuzurura kwenye kijiji cha Luterangoma,’ na badala yake tuchape kazi” (Paraphrased).

Pia unaweza kusikiliza audio clip hapa:
Maneno haya yamelalamikiwa sana na watu wengi kwenye mitandao ya kijamii. Kila mmoja anatoa sababu yuke. Baadhi wanalaumu ukavu wa kauli. Wengine maudhui. Lakini, mimi siushangai ukavu wa maneno ya Rais Magufuli. Nina shida na maudhui yake kwa sehemu fulani. Nataka kuonyesha hilo.

Nimefanya kazi kama mhadhiri katika vyuo vya LearnIT na IIT, ambako nilikuwa na jukumu la kusimamia tasnifu za utafiiti wa wanafunzi wangu, kati ya majukumu mengine.

Mara zote nilipokuwa nasimamia dissertations za wanafunzi wangu, niligombana nao sana kuhusu sura ya tatu, inayohusu utaratibu wa utafiti (methodology). Nilikuwa nawauliza swali: What is your research philosophy? Wengi walikuwa hawajui jawabu.

Ilibidi kuwaongoza taratibu. Kwa kuanzia nilikuwa nawambia wakasome tena sura ya nne juu ya “Understanding research philosophies and approaches,” katika kitabu kifuatacho: Mark Saunders, Philip Lewis and Adrian Thornhill, RESEARCH METHODS FOR BUSINESS STUDENTS, 5th Edition(London: Pearson Professional Limited, 2009)

Kwa mujibu wa kitabu hiki, kuna kambi kuu mbili za research philosophies: kambi ya Realism / Postitivism dhidi ya kambi ya Phenomenology / Constructionism. Kambi ya kwanza wanasema koleo ni koleo, sio kijiko. Yaani, ukweli unagunduliwa, hauchongwi na msemaji. Na kambi ya pili wanasema koleo inaweza kuitwa kijiko bila tatizo kubwa. Yaani, ukweli unaweza kuchongwa, 2+2 ikawa tano, kwa sababu kura zilizopigwa zinasema hivyo!

Kwa ujumla, tangu tupate uhuru tulikuwa na marais wanafenomena. Sasa kwa mara ya kwanza tunaye rais mwanasayansi. Tuukubali ukweli huo. He is a positivist, fullstop. Hivyo, tunapojadili kauli zake tuzijadili tukiwa tumevaa miwani ya positivism. Ni kwa njia hii, tunaweza kumwelewa, japo sio lazima tukubaliani naye. Katika hili ninalolisema, hoja yangu ni hii:

Kwanza lazima tujiulize: “Ukweli ni kitu gani, na tunaweza kuupataje?”

Pili, yafaa tujue kuwa, “Ama ukweli uko mahali fulani nje ya vichwa vyetu na unasubiri kugunduliwa, au ukweli unachongwa kwa kutumia ndimi zetu.”

Tatu, tukumbuke kuwa, “Kama ukweli unagunduliwa, basi tunaweza kubishana kwa ufanisi, lakini kama ukweli unachongwa, basi mabishano yote juu ya kauli yoyote ni kupoteza juda.”

Hivyo, “kabla ya kuzihakiki kauli za JPM's lazima tkubaliane juu ya msimamo wa pamoja juu ya masuala haya ya kiepistemolojia na kiontolojia.”

Tunafahamu kuwa, “JPM mwanasayansi, yaani "positivist.” Na kwa hiyo, “yafaa kuhakiki kauli zake kwa kutumia miwani ya kisayansi.” Ni kwa njia hiyo, tutaepuka kuanguka katika mtaro wa upendeleo (subjectivism/bias).

Kwa kutumia mtazamo huu, hebu sasa tuchunguze baadhi ya kauli za JPM kwa mujibu wa hotuba yake ya Bukoba, wakati akiwahutubia waanchi katika viwanja vya shule ya Ihungo.

Niwazi kwamba, ujumbe wa JPM una ukakasi kwa kuwa ni mkavu. Lakini, ni maoni yangu kuwa, kwa vile JPM ni Rais Mwanasayansi, ukavu wa maneno yake halipaswi kuwa tatizo. Badala yake, tatizo linapaswa kutafutwa katika udhati (objectivity) wa kauli zenyewe.

Na udhati huo unatafutwa kwa kuzingatia kuwa, anayeongea ni Mkuu wa nchi, anayeongoza nchi kwa mujibu wa katiba na sheria. Hivyo, kauli zake zinapimwa kwa kutumia mizania hiyo. Nitaonyesha mfano wa namna ya kuhakiki maneno ya JPM, na hivyo kuyakosoa kwa kuzingatia kiwango cha udhati wake.

JPM, kama mkuu wa nchi, anapaswa kusimamia utekelezaji wa shughuli za serikali kwa kuzingatia “kanuni ya siasa ya ujamaa na kujitegemea.” Hivyo ndivyo ibara ya 9 ya katiba ya Tanzania(1977) aliyoahidi kulinda inavyosema.

Yaani, “Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya Muungano… kutokana na kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ambayo inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano (ib.9)”

Katika mtazamo wa kifalsafa, kuongelea “kanuni ya siasa ya ujamaa na kujitegemea,” ni kuongelea “PRINCIPLE OF SUBSIDIARITY.” Siku moja, Mwalimu Nyerere, alikuwa na haya ya kusema kuhusu kanuni hii, ya Ujamaa na Kujitegemea:

“The first and the most important distinction should be drawn between the negative concept of socialism and self-reliance and the positive concept of it."

"Basically the negative concept of socialism and self-reliance refers to the limitation of competences of the 'higher' organization in relation to the 'lower' entity, whilst its positive concept represents the possibility or even the obligation of interventions from the higher organization. We can clarify this distinction in the following way."

“The negative concept of socialism and self-reliance states that: (1) the higher entity cannot intervene if the lower entity can satisfactorily accomplish its aims, or (2) the higher entity should not intervene if the lower entity alone can accomplish its aims, or (3) the higher entity must not intervene if it is not assigned to do so."

“The positive concept of socialism and self-reliance states that: (1) the higher entity can intervene if the lower entity cannot satisfactorily accomplish its aims, or (2) the higher entity should intervene if the lower entity alone cannot accomplish its aims, or 3) the higher entity must intervene if it is assigned to do so.”


Kwa sababu hii, kanuni ya siasa ya ujamaa na kujitegemea ni kanuni inayoongelea mfumo wa mkamilishano uliopo kati ya serikali kuu, serikali ya mkoa, serikali ya wilaya, serikali ya kata, serikali ya kijiji, serikali ya kitongoji mpaka kaya. Zote nizi ni “entities” zinazoongelewa.

Kwa hiyo, kauli ya JPM kwamba, “kila mmoja katika upande wake abebe msalaba wake mwenyewe,” inaeleweka na kukubalika.

Lakini, tatizo liko katika kujua "upande" wa serikali kuu ni upi na "upande" wa serikali ya mkoa/wilaya/kata/kijiji/kaya ni upi. Kanuni ya siasa ya ujamaa na kujitegemea inatoa mwongozo katika hili.

Hata hivyo, ni maoni yangu kwamba, JPM haonekani kuizingatia kanuni hii. Kwa mfano, JPM anaharibu umantiki wa kanuni hii, pale anapoongea maneno haya:

"Panapotokea janga kama vile tetemeko, jukumu la serikali siyo kujenga nyumba za wananchi. Asitokee mtu kuwadanganya kwamba serikali itagawa chakula, kwani serikali haina shamba.”

Kupitia maneno haya, na kadiri kanuni ya siasa ya ujamaa na kujitegemea inavyohusika, napendekeza kwamba, Rais ameonyesha dhamira ya kuvunja Katiba aliyoapa kuilinda.

Kwa ujumla, katika eneo hili la kisiasa, bado JPM anapwaya sana. Hivyo, Namshauri JPM afanye hima kutafuta mshauri wa kisiasa.

Najua fika kuwa, Askofu Dk. Methodius Kilaini ni mtaalam sana katika eneo hilo. Juzi nilimwona JPM akibusu pete yake ya Kiaskofu.

Hivyo, hapa pia namwomba Askofu Kilaini kumnong'oneza JPM juu ya umuhimu wa kuheshimu kanuni ya siasa ya ujamaa na kujitegema, kwa maana ya “the principle of subsidiarity.”

Mwaka 1931, Papa Pius XI, kupiti waraka uitwao “Quadragesimo Anno,” aliongela “Kanuni ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea” kama ifuatavyo:

“It is a fundamental principle of social philosophy, fixed and unchangeable, that one should not withdraw from individuals and commit to the community what they can accomplish by their own enterprise and industry. So, too, it is an injustice and at the same time a grave evil and a disturbance to right order to transfer to the larger and higher collectivity functions which can be performed and provided for by lesser and subordinate bodies. Inasmuch as every social activity should, by its very nature, prove a help to members of the body social, it should never destroy or absorb them.”

Namtakia utendaji mwema JPM.

Deusdedith Jovin Kahangwa
January 04, 2017.
===========================
Chanzo: www.facebook.com/deus.jovin
 
Kwa Pomb@ hatoweza ..labda awe na Bunduki maana wasukum@ wanaogopa hiyo kitu sana tu. ...
 
Ni ushauri mzuri, najiuliza atakusikiliza kwl na kuufanyia kazi ushauri huu? Hotuba za raisi wangu zimekuwa ngumu kusikiliza hadi huwa naaona aibu kwa niaba yke akishamaliza tu kuongea.
 
Nakushukuru sana mkuu kwa kuamua kumchambua JPM kisomi. Binafsi nafikiri kuna mambo mawili pia ni lazima tukubali juu ya aina ya approach ya utawala wa huyu rais.

Mosi ni suala zima la matumizi ya lugha. Namwangalia mkuu kama mtu asiye na uwezo wa lugha katika ama mazingira ( contextual ) au ujumbe (textual) lugha inatakiwa kutumika vipi. Kwa kiongozi kutokuweza kuwasilisha kwa usahihi unachotaka kifikisha inaweza ikawa na matokeo hasi, hisia kinzani na upotevu wa maana nzima. Na hili linadhihirika wazi kwa raisi huyu, watu wanaoumia, kulia na kujutia wengi wao si kwasababu ya maamuzi yake bali ni kwa namna anavyowasilisha alichotaka kipokewe. Hii imemletea ugomvi mkubwa na waliokuwa wakimsikiliza na kumtizama, hofu inajengeka mno kuliko matumaini machoni na masikioni mwa watu. Sidhani kama kueleweka ni lazima uwe aggressive, wanadamu ni kweli tunatofautiana lakini kwasababu ya tofauti zetu ndo maana tunakuwa na mafunzo (training) pia kwenye maeneo fulani, hii inatusaidia tuweze kufiti zaidi

Pili ni mitizamo iliyopo kati ya management theories na approach zake. Hili sitaliongelea sana kwani bado naendelea kupitia makabrasha lakini kuna kitu nakiona. Mh. huyu anaonekana kuwa mfuasi wa mbinu za kiuongozi za kisayansi na si zile za kijamii zaidi. Sasa ninachokijua ni kwamba kuna tofauti kubwa ya approach ya kushughurika na matatizo ya kijamii kati ya makundi haya mawili. Msingi mkubwa ni kwamba wakati mmoja atajaribu kuyatatua kijamii zaidi (diplomatically), mwingine atakuwa katika upande wa kuamini katika kutumia njia fupi zaidi (short cuts) ilimradi yeye afikie lengo.
Ijapo kila kundi lina misingi yake mikuu, binafsi naamini kuongoza watu ama kuwa kiongozi ni kushughurika na jamii zaidi. Kama ndivyo basi ni, lazima kwanza uisome na kuishiba, uichambue kwa mazuri vs madhaifu yake, uiishi wakati unaibadirisha (if so) na mwisho uendelee kuiweka jamii ikiwa moja na iliyo imara zaidi. i.e usiiache jamii ikiwa na hofu kila panapo na uwepo wako.

Yangu ndo hayo
 
.
Umeandika vema.

Labda tu niongeze kidogo. Nimefanya kazi kama mhadhiri wa technical communication pia. Nimewafundisha wanafunzi wangu kwamba, ukitaka kutoa hotuba au presentation yoyote iwayo, unafanya yafuatayo:

1. Soma hadhira yajo (audience analysis)-age, sex, political orientations, income levels, education levels, current neeads, current expectations, nk
2. Amua juu ya ujumbe wa msingi kuelekea hadhira hiyo (message content).
3. Amua juu ya toni (tone)--aggressive vs polite
4. Amua juu ya mkakati wa makabiliano (delivery approach)-direct vs indirect
5. Amua juu ya staili ya kushawisi (persuasion style)--logical vs emotional or both
6. Andika hotuba yako
7. Fanya mazoezi (rehearsal)
8. Wasilisha ujumbe siku ikifika.

JPM kama msomi, tena ngazi ya PHD, atakuwa anayafahamu haya, au anao watu wa kumsaidia kuyafahamu haya.

Swali langu ni moja: Je, katika kutekeleza hatua hizi amefanikiwa kwa kiasi gani, au amefeli kwa kiasi gani, na kwa nini?

Kwa jinsi nilivyomsikiliza akiwa Ihungo, nilipata shida moja: Alikuwa kama yule kipofu aliyekuwa anajua kuwa kitu kikubwa pekee hapa duniani ni tembo. Na hivyo, baadye, kila alipsikia wenzake wanasema kitu kikubwa, kitu kile kikubwa, n.k, yeye alikuwa akidakia kwa kidahizi kimoja "eeeh, kama tembo!"

Kauli mbiu ya "hapa kazi tu" ni nzuri.
Lakini, ukienda msibani, kuhani msiba, hapo sio mahali pake!
At least, that is my disappointment with him in this regard...

NB: Umeongelea scientfic theories of management.
Nimefundisha kidogo haya pia.
Mfano, kanuni ya Management by Objectives (MBO) ina msingi wake huko kwenye Scientific Management.
Ikisimamiwa vema ni nzuri tu.

Tatizo langu kwa sasa: Tuna Tanzania Development Vision 2025 (TDV2025), lakini hakuna ministerial/sectoral strategic plans kuelekea 2025.
Ni vivyo hivyo kwa LGAs zote zilizo chini ya Waziri Simbachawene.
Hakuna scientific management hapo.

Pale REPOA kuna reserachers wazuri, waliokuwa wanatusaidia kusuka MKUKUTAi&II.
Angewachukua na kuwaweka TUME YA MIPANGO WANA MSAADA MKUBWA.

Ukiangala MKUKUTAi&II dhidi ya Huu mpango wa Maendeleo wa 2016-2021, kuna tofauti kubwa. REPOA's are somehow superior!

Hata Mh Januari Makamba aliyejipambanua kama mtu anayejua umuhimu wa kufanya documentation ya mawazo yake, mpaka leo anaongoza Wizara isiyo na Staregic Plan ya 2025.

The nation has no latest govt owned ETOA Report (Environmental Threats and Opportunities Assessment Report).

Without it no strategic intervention is possible.

Tunazidiwa na Rwanda!

Naongelea "Wizara ya Mazingira," bila kuijumlisha na Mambo ya Muungano.

Who is going to tell JPM and subordinates all this?
Bado "Askofu Kaneno" anaweza...
Let him try...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…