Askofu Katoliki ataka viongozi wanaoamini Taifa halina uhaba wa chakula waombewe

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,950
Sunday, January 15, 2017
Wana jf
Salaam.

Askofu mkuu wa jimbo la Mwanza Mhashamu Thadeus Ruwaichi amewataka waumini wafunge lovena kuliombea taifa juu ya baa la ukame na njaa pia kuwaombea viongozi watambue kuwa BALAA HILO LIPO NCHINI KWA SASA.
Amesema hayo katika Parokia ya Pansiasi katika ibada ya kutoa kipaimara kwa vijana wa kikristo.
Kauli hii inatutaka waumini na raia kuwaombea wale viongozi wanaosema hakuna ukame wala njaa kwa vile wameona majani ni ya kijani.
 
Mods UNGANISHA hii na ile ya Askofu Ruwaichi: Waumini waombeeni Viongozi watambue kuna Njaa..... Ni stori ile ile!
 
Hawa mababa Askofu wanataka kutugombanisha wananchi na serikali yetu hii haivumiliki.
 
Huyo askofu atakua amenunuliwa na wapinzani na wapiga dili wenye matani ya mahindi bandarini wanaotaka kuyapitisha bila kulipia kodi.

Kwa maelezo ya Mh. Rais njaa haipo katika nchi hii, wanaosema kuna njaa ni waongo.
 
Credibility ya askofu nchi ina uhaba wa chakula inaanzia wapi.

Idadi ya watu wanaolishwa na kanisa imeongezeka, wanao omba misaada kwao? uwezi kujiropekea tu

Ni mfanyakazi wa national bureau of statics ya Tanzania? or what exctactly is the premise of his suggestion.

Hawa watu wanaviherere kupita akiulizwa atupe sababu za uhaba wa chakula kwa facts anazo au ndio kujiropokea tu.
 
Mbona anaendaga kwao mara kwa mara na anapiga magoti na Pete zao ana busu,kwa nini wasimtoe pepo hapo hapo kama wanaona anastaili kuombewa.
 
Hivi hata nyumbani kwenu kijijini wanasubiri mpaka TAKWIMU waseme kuwa kuna upungufu wa chakula ndio nao wakupigie simu wakueleze kuwa mwaka huu wana hali mbaya ya chakula? Hamchoki kuwaziba midomo wananchi?
 
Hivi hata nyumbani kwenu kijijini wanasubiri mpaka TAKWIMU waseme kuwa kuna upungufu wa chakula ndio nao wakupigie simu wakueleze kuwa mwaka huu wana hali mbaya ya chakula? Hamchoki kuwaziba midomo wananchi?
 
 
Hivi hata nyumbani kwenu kijijini wanasubiri mpaka TAKWIMU waseme kuwa kuna upungufu wa chakula ndio nao wakupigie simu wakueleze kuwa mwaka huu wana hali mbaya ya chakula? Hamchoki kuwaziba midomo wananchi?
Tatizo lenu upuuzi umeshawai kuisikia taasisi inayoitwa About FAO | FAO | Food and Agriculture Organization of the United Nations embu jaribu kuwasoma wana deal na mambo gani na wanatoa update za famine how often, potential risk nations etc na angalia kama Tanzania ipo humo. Kabla ya kuja kuropoka humu ndani.

Umeenda soko gani ukaona hakuna chakula?
 
Super fool
How exactly?

Kwa sababu nataka kujua credibility ya muhamisishaji ama?

to me a fool is somewhat complex definition, but I am not ignorant I can assure you leta data za sehemu zenye utapia mlo ndio tukusikilize sio hadithi za mifugo kufa.
 
wakamuambia huyo siyo paka ni nunda mla watu hakuamini. alisisitiza yule ni paka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…