Askofu Gwajima ahofia wahuni ku-edit kinasaba cha mtu

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,956
5,324
Mbunge wa Jimbo la Kawe Dar es Salaam, Askofu Josephat Gwajima amehoji serikali imejipangaje pale itakapopokea tiba ya ‘CRISPR Cas 9 Gene Editing’ kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa seli mundu (sickle cell), kuhakikisha kwamba mtu atakapoingia kwenye chumba cha tiba hahaririwi vitu vingine kwa maana ya kubadilisha vinasaba vyake ambavyo vitamfanya atoke kwenye matibabu akiwa mtu mwingine. Askofu Gwajima pia amehoji kama serikali italeta muswada wa sheria ya kudhibiti watu wasifanye hilo.

Akijibu, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema ni kweli jambo hilo linaweza kutokea lakini amesema si rahisi kwa serikali ya Jemedari Samia Suluhu Hassan ambayo iko makini kufuatilia afya ya Watanzania na ndio maana akapewa tuzo ya “The Gates Goalkeepers Award” kama kielelezo cha matokeo makubwa ambayo yamepatikana kwenye uongozi wake kufuatia ripoti ya utafiti wa demografia na afya ya mwaka 2022 inayoonesha kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 80, tuzo ambayo ni ya kwanza kwa Rais Mwafrika.

Dkt. Mollel, amesimulia kisa cha mtu aliyefanyia uhariri kinasaba cha mama mmoja na kuzaa watoto wawili ambao hawapati ukimwi, amewatoa wasiwasi Watanzania akisema ana hakika tiba hiyo ikianzia kutumika, sheria ya kudhibiti wahuni kuitumia vibaya itatungwa.

Hata hivyo amesema tiba hiyo haijaanza kutumika rasmi duniani.
 
Back
Top Bottom