Askofu Gamanywa: Kama ni taa za barabarani kwa sasa Nchi yetu tupo kwenye taa ya njano, tunaona matumizi ya 'hard power'

Nyakijooga

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
289
484
Askofu Mkuu Dk. Sylvester Gamanywa wa Wapo Mission Tanzania, ameshauri mamlaka kutumia mbinu ya 'soft power' katika kuthibiti masuala mbalimbali hususani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi ili kuendelea kustawisha amani ya Nchi.
images (2) (28).jpeg

Amesema kwamba kwa uzoefu wake anaelewa kuwa kuna mbinu tatu ambazo hutumiwa Serikali mbalimbali katika kushughulikia au kuthibiti 'uasi', amesema mbinu hizo ni 'Hard Power' (kutumia nguvu) soft power (mashauriano, mazungumzo), pamoja na 'smart power' ambayo ni mchanganyiko wa kutumia nguvu pamoja na mazungumzo.

"Tuitumie 'soft power' kwa sasa hivi, kabla hatujafika kwenye hatari, kama ni kwenye taa za barabarani kwa sasa tupo ya njano (taa hiyo uonesha tahadhari)"

Anaongeza "Tanzania tulipofikia katika Bara la Afrika sio kwamba tunaongozwa tu kwa ajili ya Nchi kuwa ya amani, lakini amani inakuwepo kwa sababu ya Hekima ya jamii husika, sasa tusijichanganye"

Amesisitiza kwamba inapotokea mamlaka zikatumia nguvu kubwa kuthibiti 'uasi' ni nadra amani hiyo kustawi, ambapo amesema kwamba hakuna shaka 'hard power' inaonekana kutumika.

"Hard power' inaweza hisifanye kazi kwa kuleta matokeo chanya"amesema Askofu Gamanywa

Ameyasema hayo katika Kongamano la amani kwa viongozi wa dini kuelekea uchaguzi Mkuu, ambalo limefanyika leo April 23, 2024 Jijini Dar es salaam.
 
View attachment 3313129

Mpaka na huyu Mzee wao amesema basi ngoja tuone
 
Back
Top Bottom