Askofu Desmond Mpilo Tutu wa Afrika ya Kusini hakukaa kimya kuwatetea watu weusi (Dini vs Siasa)

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
25,126
74,987
Kumekuwa na discussion kuhusu kuchanganya dini na siasa. Kusema kweli jambo hili limafikirisha sana.

Askofu Desmond Tutu wa Afrika ya kusini alisimama na waafrika kupinga sera za ubaguzi wa rangi huko Afrika ya kusini. Ukombozi wa mtu mweusi umekuwa ukipiganiwa na maaskofu miaka mingi.

Hapa ndipo kwenye akili na ufahamu. Tunapoongelea siasa maana yake ni nini? Je, siasa ni kuongea uongo na kufanya mambo yasiyofaa kwa kutumia madaraka uliyonayo na kukandamiza wengine? Je, siasa inatakiwa izungumziwe wapi? Kwenye ofisi za umma? Kwenye kaya au zinatakiwa kuzungumziwa kokote?

Kwa namna ninavyojua mimi siasa ni sehemu ya maisha ya kila binadamu. Tunafanya siasa kuanzia kwenye familia mpaka kimataifa.

Siasa ni namna ya kuleta ushawishi kwenye jamii au watu fulani. Siasa siyo kufanya uongo na uzandiki. Siasa ni kukaa na kushindana kwa hoja. Ukiulizwa maswali unatakiwa uyajibu pasipo kujificha.

Desmond Tutu alikuwa ni Askofu alitimiza wajibu wake kama askofu wa kuitetea jamii dhidi ya wanyonyaji.

Nchi hii siyo monarch, eti familia moja ndiyo iweze kuongea kwaajili ya watanzania wote!!! Nchi yetu ni republic tunapata uongozi kwa kupitia jamii.

HOJA HAIPIGWI NYUNDO, INAJIBIWA KWA HOJA.

Pia, Soma
 
Naomba title isomeke:-

Askofu Desmond Mpilo Tutu wa Afrika ya Kusini Hakukaa kimya kuwatetea watu weusi (Dini vs Siasa)​

Innovator
 
Mchungaji Martin Luther King Jr wa Marekani hakukaa kimya katika kutetea watu weusi.

Iweje leo inakuwa nongwa kwa Maaskofu wa Baraza Kuu la Katoliki kutetea Tanzania?

Tanzania hii ni yetu sote, na wao ni sehemu ya Tanzania. Wajibu wa kanisa ni kusaidia jamii katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kijamii.

Martin Luther King Jr. Aliwatetea watu wanyonge na impact yake ipo mpaka leo.

Hoja nzito nzito lazima zijibiwe kwa uzito huo huo. Huwezi ukasimama kwa dharau na kuanza kuwakebehi, eti tu kwa sababu wewe umewahi kushika wadhifa fulani sehemu fulani.

Mambo ya dynasty yaliwashinda akina Khan kipindi kile cha ujima je, yanaweza kufanyika leo kipindi cha sayansi na teknolojia?

HOJA NZITO HAZIJIBIWI KWA MATAMSHI MEPESI MEPESI.
 
Kadinali Laurent Monsengwo Pasinya wa Congo DRC

Pale Joseph Kabila alipolewa madaraka na kutaka kuiendesha nchi anavyotaka yeye. Aliweza kusimama na maaskofu wenzake kupinga nakutoa waraka juu ya unyanyasaji wa serikali ya Congo.

Tunapojadiliana haya mambo tusijadili kama watu tuliojifungia kwenye kijiji kisicho na internet. Dunia sasa ni kijiji taarifa zinasambaa kila kona. Mtu anaweza kuingia kwenye mitandao na kupata taarifa.

Kutumia mabavu na kulazimisha jambo lako lionekane linafaa mbele ya jamii kwa sasa nafasi hiyo hakuna. Dunia ilishaamka kila mmoja anayohaki ya kushiriki mambo ya kisiasa. Siyo kundi la watu fulani tu ndio wanastahili.


Hoja zijibiwe kwa hoja.
 
Kadinali John Olorunfemi Onaiyekan wa Nigeria

Tunaposimama kupinga tamko tuwe na elimu ya kutosha kujua dunia kwa sasa ipo inaelekea wapi. Baada ya vita vya pili vya dunia utawala wa mabavu na kujificha kwa misemo myepesi myepesi ilishapitwa na wakati.

Sasa hivi tupo kwenye zama za facts. Tunaona huyu kadinali wa Nigeria na yeye alisimama na kuleta mabadiliko makubwa huko Nigeria.

Kazi alizofanya
The shariah in Nigeria: a Christian view", Bulletin on Islam & Christian-Muslim Relations in Africa.

During the administration of Nigerian President Olusegun Obasanjo, and especially during his second term between 2004 and 2007, Onaiyekan spoke out against the regime for its failure to support democratic principles and its corruption.
 
Siasa ni maisha ya kila siku uwezi kuwa kiongo wa dini ukiongoza watu wanaonewa na kundi la watu fulani eti wakae kimya lazima wakemee mapepo.

Hili la udini limeshindwa kabla ya kuanza watafute kituko kingine huku wakingojewa kujibu hoja za bandari.
 
Kadinali Berhaneyesus Demerew Souraphiel wa Ethiopia

Huyu aliweza kufungwa na serikali na Ethiopia kutokana na kutetea watu wa Ethiopia.

Kabla ya kuwa kadinali amewahi kushika nyadhifa:-
President of Council of the Ethiopian Church

President of the Ethiopian and Eritrean Episcopal Conference

Cardinal-Priest of San Romano Martire

Sasa utalitenganishaje kanisa na siasa?
 
Kadinali Philippe Nakellentuba Ouédraogo wa Burkina Faso

Naona tunayaona yanayoendelea kwa sasa huko Burkinabe. Kila mtu anaona. Viongozi waliojisahau kwenye madaraka walikuwa wakitoa matamshi ya dharau. Kuwaona viongozi wa dini hawahusiki na siasa.

Lazima tukae kama nchi tukubaliane. Lakini kuwakandamiza wananchi eti kwasababu tu wewe hupendi kuambiwa ukweli siyo vyema.
 
Congo Maasikofu waliongoza maandamano barabarani ya kupinga Joseph Kabila mkatoliki kupisha madarakani,ccm jibu hoja za bandari acha kucheza na maneno.
 
Back
Top Bottom